CARLO ANCELOTTI AFUNGIWA MPAKA MWISHO WA MSIMU
KOCHA
wa timu ya Real Madrid atakosa michezo yote iliyobakia ya msimu huu
baada ya kufungiwa na shirikisho la soka la Hispania {RFEF}.
Kufungiwa
huko kunahusishwa na makofi ya dharau aliyompigia refa wa mchezo kati
ya Real Madrid na Valencia waliyotoka sare ya goli 2-2 jumamosi
iliyopita.
Ancelotti
alikutwa na makosa hayo baada ya kuvunja sheria ya kifungu namba namba
117 cha nidhamu ambayo inasema “kwa wote ambao watashughulika na waamuzi
awe meneja au maafisa wengine kwa hali yoyote ile awe na hasira au
mitazamo ya dharau au kupuuza … adhabu yao ni kusimamishwa ” .
Mwamuzi
Carlos Clos Gomez aliandika katika ripoti yake ya mchezo” Mwisho wa
mchezo kocha Ancelotti kutoka umbali wa mita 30,aligeuka na kunipigia
makofi ambayo ni ya dharau na yanapingana na maamuzi yangu katika
mchezo ule”
Kocha
huyo mwenye umri wa miaka 55 atakosa mechi hizo hadi msimu huu unaisha
dhidi ya Espanyol na Getafe,katika harakati za kupunguza pengo la pointi
4 dhidi ya vinara wa ligi hiyo Barcelona.
Real
Madrid wanakutana na Juventus leo katika usiku wa ulaya na kujaribu
kubadili matokeo ya 2-1 baada ya kupoteza mechi ya kwanza,Barcelona
tayari wameshafuzu kwa fainali ya juni 6 pale Berlin.
No comments:
Post a Comment