Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
NYOTA wa kikosi cha Mbeya City, Steven Mazanda na Yusuph Abdalah Sisalo watalazimika kusubiri mpaka msimu ujao ili kurejea uwanjani kukitumikia tena kikosi chao kutokana na majereha makubwa waliyokuta nayo mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Daktari mkuu wa City, Dk Joshua Kaseko, amekaririwa katika mtandao rasmi wa klabu hiyo akieleza kuwa nyota hao wawili wameshindwa kupona majeraha yao katika muda uliotarajiwa hivyo waatalazimika kusubiri msimu mpya ili kurejea uwanjani.
“Awali kulikuwa na dalili njema kuwa huenda wangepona haraka na kurejea kumalizia michezo ya mwisho, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu, lakini imeshindikana na kama unavyofahamu si jambo nzuri kumlazimisha mchezaji kucheza wakati vipimo vinaonesha bado hayuko sawa. Kwa sasa hakuna namna nyingine zaidi ya wao kuendelea na matibabu ili wapone kabaisa tayari kwa msimu ujao”, amesema Dk Kaseko.
Mazanda aliumia goti la mguu wa kulia akiwa mazoezini siku moja kabla City haijashuka dimbani Sokoine kuivaa Stand United ya Shinyanga kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliomalika kwa City kushinda bao 2-0 huku Sisalo akiumia goti la mguu wa kulia dk ya 15 ya kipindi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Ndanda Fc ulichezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Ndanda FC.

No comments:
Post a Comment