Wakati bado wakiwa na
kumbukumbu ya kudhalilishwa nyumbani na mahasimu wao Barcelona, kisha
jana wakaondolewa kwenye michuano ya Copa Del Rey, leo hii kocha aliye
kwenye presha Rafael Benitez ataiongoza klabu yake ya Real Madrid
kuikaribisha Getafe Santiago Bernabeu. Getafe
ndio wageni wanaokaribishwa Bernabeu usiku wa leo na kwa namna hali
ilivyo hakuna mjadala wa kuwazungumzia – kwa sababu Madrid wamekuwa
wakiandamwa na sakata la kuondolewa kwenye Copa Del Rey baada ya hukumu
iliyotolewa jana – na leo mashabiki wa timu hiyo wanatarajia kuonyesha
hasira zao kwa kocha Rafael Benitez kwa kile kinachoitwa uzembe wa
kumpanga mchezaji ambaye alikuwa kafungiwa.
Madrid/Benitez wanaingia kwenye mchezo wa leo huku baadhi ya
mashabiki na wanachama wa klabu ambao kimsingi ndio wamiliki wa timu
wameonyesha nia ya kuchukua hatua za kisheria kwa klabu.
Katika mechi ya leo, James Rodriguez ambaye alikuwa kwenye ubora wake katika mechi vs Cadiz, anatarajia kuanza.
Jana ilitangazwa kwamba Benitez hakumuweka Marcelo katika kikosi cha
mechi ya leo kutokana na majeruhi lakini cha kushangaza mchezaji huyo
aliandika kwenye mitandao ya kijamii – “Nimepona kabisa na nipo tayari
kucheza.” – jambo hili limezidi kuongeza sintofahamu baina ya Benitez na
wachezaji wake. Leo
pia tunaweza kuona ‘BBC’ wakicheza kwa pamoja tena. Benzema alifunga
magoli 6 katika mechi 6 za kwanza za ligi lakini akaumia na akaanza
kuandamwa na kesi ya ulaghai dhidi ya Mathieu Valbuena – na sikza hivi
karibuni amekuwa ‘off form’. Cristiano, kwa upande mwingine anaonekana
kurudi kwenye mstari baada ya kufunga magoli matatu katika mechi 2
zilizopita. Usiku wa leo Ronaldo anakutana na timu ambayo ameshaifunga
magoli 18 katika mechi 10 zilizopita – zikiwemo hat trick 3 na magoli
mawili mawili mara 4.
Vikosi vinavyotegemewa kuanza leo na mifumo Getafe hawana rekodi nzuri ugenini maimu huu – wameambuliwa kupata sare
moja na magoli mawili tu katika mechi 6 zilizopita – rekodi mbaya zaidi
ya ugenini kwenye La Liga. Leo usiku wa leo watakuwa bila Juan
RodrÃguez na hivyo wanategemewa kucheza kwa mfumo wa 4-1-4-1
Na Simon Chimbo
Magoli mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Gonzalo Higuain dhidi ya
Inter Milan katika ligi kuu soka nchini Italia juma hili yalitosha kuipa
usukani wa ligi Napoli kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka
25, na hayo yote yamewezekana kwa mchango mkubwa wa mshambuliaji Gonzalo
Higuain, raia wa Argentina.
Katika mechi iliyokua ya kujua nani ataibuka farasi mshindi katika
mbio hizo Napoli kupitia Gonzalo Higuain ilijipatia goli lake la
kuongoza katika sekunde ya 65 tu kabla ya kuongeza lingine la pili na la
ushindi na kuwaacha vijana wa Roberto Mancini wakitweta katika vita
hiyo.
Gonzalo Higuain ameshaweka kambani mara 12 katika michezo 14 ya serie
A hadi sasa na kuifanya Napoli kuwa juu ya ligi huku pia wakiwa
hawajapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi walipocheza na
Sasuollo.
Muargentina huyo anawakilisha vyema falsafa mpya aliyokuja mayo kocha
Sarri huku wakicheza mpira wa kasi na kuvutia hususan katika eneo la
mwisho la kiwanja, ambapo Higuain amekua akiongoza vyema safu ya
ushambuliaji.
Achilia mbali magoli 12 katika michezo 14 lakini pia katoa assists 22
kwa wachezaji wenzake na kuwa na wastani wa asilimia 53 shot accuracy
huku Messi akiwa na 59% na Ronaldo 50% ni rekodi adhimu.
Lakini yote haya yamekuja kutokana na ukweli kuwa ujio wa kocha Sarri
katika klabu hii umeleta ari na mbinu mpya za ushindi wa Napoli sanjari
na fomu ya mshambuliaji Gonzalo Higuain tofauti na kipindi cha kocha
Rafael Benitez.
Kocha Rafael Benitez alikua akitumia mfumo wa 4-2-3-1 na kumfanya
Higuain awe peke yake muda mwingi mbele na hivyo kushindwa kupata sapoti
kubwa ya wenzake, wakati hivi sasa kocha Sarri amekuja na mfumo wa
4-3-3 unaowafanya washambuliaji wa pembeni ya Higuain kushirikiana naye
vizuri kutengeneza nafasi za kufunga.
Ujio wa kocha Sarri ni neema kwa Napoli na sasa wanaongoza ligi kwa
mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25, itakua ni ndoto kwa
mashabiki wa Napoli siku wanatwaa ubingwa wa ligi hiyo ‘Scudeto’
Mashabiki wanafurahia soka zuri la kuvutia tofauti na misimu
iliyopita, Higuain anafunga magoli, timu inapata ushindi, ni msimu mzuri
sana kwa Napoli kama tu wataendelea na kasi hii.
Ivo Mapunda hivi sasa ni mchezaji wa Azam FC akiwa anaongeza safu ya
kikosi hicho kwenye sehemu ya ulinzi wa lango lao. Kupitia Azam FC Ivo
Mapunda alisema haya kuhusu yeye kujiunga na Azam FC’ “Naamini Azam ni timu bora, sawa timu bora Afrika Mashariki
na Kati, hata kama ningeenda kucheza Kenya nadhani huenda nisingepata
timu nzuri kama Azam, naamini kabisa ni professional klabu tofauti na
klabu nyingine ambazo nimewahi kucheza kwa hapa Afrika Mashariki na Kati
na ndio maana nikaona bora nibaki hapa niweze kucheza.”
Sababu za Messi kupewa Tuzo ya Mshambuliaji Bora La Liga na Kwanini Naamini Neymar na CR7 hawastahili kuwemo Top 3 Ballon D’Or
kama tunavyojua wiki hii kulitolewa tuzo mbalimbali za Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ kwa msimu
uliopita. Mojawapo ni ile ya mshambuliaji bora wa msimu ambayo
ilichukuliwa na staa wa Barcelona, Lionel Messi.
Kati ya tuzo zilizotolewa, kipa bora, beki bora na kocha bora na
nyinginezo, lakini kidogo hii ya Messi imezua mjadala wa aina yake.
Wapo wanaoamini ilimfaa mpinzani wake wa karibu, Cristiano Ronaldo wa
Real Madrid, wakiegemea katika hoja ya kutwaa tuzo ya ufungaji ambapo
alimzidi Messi. Ni kweli, Ronaldo alifanya kweli katika ishu ya kucheka
na nyavu, kwani alimaliza msimu akiwa na hat trick nane, dhidi ya tano
za Messi.
Ni dhahiri unapozungumzia sekta ya ufungaji bora, Ronaldo ama CR7 kama
anavyofahamika, alistahili kuchukua tuzo hiyo, lakini kuna kitu
kinachowachanganya wengi. Unapozungumzia mfungaji bora na mshambualiji
bora ni vitu viwili, ingawa wote wanaweza kuwa na jukumu la kufunga.
Mshambuliaji bora ni aina ya mchezaji anayetegemea mfumo wa timu na
mfumo wa kocha na ili afunge lazima awe kwenye muunganiko wa timu na
kushiriki katika mipango yote ya kupatikana kwa bao. Hii ni sifa kuu
inayowatofautisha watu hawa. Mfungaji bora yeye anaweza kujitegemea
katika kulitafuta bao na asishiriki katika upatikanaji wa mpira hadi
kufika langoni mwa mpinzani.
Ni kutokana na aina hizo, tunapata aina mbalimbali za washambualiji.
Kuna wale ambao huitwa washambuliaji waliokamilika ‘complete strikers’,
hawa hufanya kazi zote kulingana na mfumo na hushiriki kikamilifu katika
kuisaidia timu kuanzia kuitafuta mipira mpaka kupatikana kwa bao. Hapa
utakutana na watu kama Luis Suarez, Messi, Sergio Aguero.
Takwimu za Ufungaji za Messi na Ronaldo msimu uliopita
Wapo wale waitwao waviziaji (poachers), hapa unakutana na kina Javier
Hernandez ‘Chicharito’ Filippo Inzaghi, Ruud van Nistelrooy. Pia kuna
kundi la washambuliaji wao kazi yao ni kumalizia mipira langoni (target
man) hapa wamo kina Oliver Giroud, Peter Crouch, Fernando Torres,
Gonzalo Higuain na wengineo. Matumizi yao uwanjani ni tofauti na kariba
ya ushambuliaji wa kina Messi. Kuna
vitu vya kumuangalia mshambuliaji bora kama straika nini majukumu yake
uwanjani kama kufunga. Kulingana soka la kisasa (modern football),
straika kwa sasa ni zaidi ya kufunga. Kuna wakati eneo ambalo upo
unaangalia jinsi ya kuisaidia timu yako na siyo suala la kufunga mabao
wewe mwenyewe, ila mchango wako kikosini kwa jumla, achilia mbali
kufunga kwako.
Ndiyo maana Jose Mourinho amekuwa akilumbana na Diego Costa, siyo
kusema anashindwa kufunga tu, ila anaangalia mchango wake uwanjani
katika kuisaidia Chelsea hasa kipindi hiki kigumu kwao.
Majukumu ya Messi si kuwa kama straika tu ndani ya Barcelona, ila
uwezo wa kutoa asisti na uwepo wake kwenye safu ya ushambuliaji husaidia
sana wenzake kufunga kiurahisi.
Mathalan angalia bao linalowania tuzo ya Puskas, anatoka katikati ya
uwanja, anachambua mchezaji hadi mchezaji na kutupia mpira kambani. Hayo
ndiyo mahitaji ya mshambuliaji katika soka la kisasa.
Matokeo ya kura zilizompa Messi tuzo ya Ushambuliaji Bora
Hivyo, Messi amekamilika, kulinganisha na CR7 ambaye kweli anajua
kufunga lakini hajakamilika kwa mantiki ya mahitaji ya soka la kisasa.
Hata takwimu zinaonyesha Messi alimaliza msimu akiwa na asisti 18 dhidi
ya 16 za CR7
Pia nigusie kuhusu tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Messi, CR7 na
Neymar. Kwa mtazamo wangu, sioni kama CR7 alitakiwa kuingia safari hii,
ukilinganisha na wengine walivyofanya vizuri. Ninaamini ilikuwa ni fursa
kwa mmoja wa Juventus alitakiwa kuwemo katika majina haya.
Hakuna aliyekubali kuwa msimu uliopita Juve ilikuwa katika ubora wake
na kweli walistahili kutoa mchezaji mmojawapo katika kinyanganyiro
hiki. kati ya Paul Pogba ama Arturo Vidal mmojawapo alitakiwa kuingia. Mimi ni shabiki mkubwa wa Ronaldo, sidhani kama alistahili kuingia kulinganisha na wenzake walivyofanya mengi mazuri.
Niliwaangalia Neymar na Luis Suarez, siamini kama Neymar alitakiwa
kuwemo mbele ya Suarez, labda pengine kwa kuwa Suarez alikuwa na adhabu
kwa timu ya taifa. Suarez ana mchango mkubwa tena sana kuliko Neymar
ambaye naweza kusema wanajaribu kupewa promo na makampuni makubwa kwa
ajili ya kujitangaza kwa tija ya biashara nchini Brazil, lakini
vinginevyo hakustahili mbele ya Mruguay huyo.
Ila kama ilikuwa sababu ya adhabu ya kinidhamu kwa Suarez, Neymar
anastahili kuwemo lakini kwa mtazamo wangu, Ronaldo angetoka na kuingiza
jina mojawapo kati ya Vidal ama Pogba kutokana na mafanikio makubwa
waliyokuwa nayo msimu uliopita.
Nyota wa Simba SC Raphael Kiongera ameanza mazoezi mara moja mara
baada ya jana kutua visiwani Zanzibar ambako Simba imekita kambi
kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Azam FC utakaopigwa December 12, 2015
kwenye uwanja wa Taifa.
Kiongera amejiunga na Simba akitokea Kenya ambako alikuwa kwenye
klabu ya KCB kwa mkopo mara baada ya kupona majeraha ya mguu
yaliyomsumbua kwa muda mrefu.
Simba imeamua kumrejesha mshambuliaji huyo baada ya kufanya vizuri
kwenye klabu ya KCB ambapo mwezi August mwaka huu alitwaa tuzo ya
mchezaji bora wa mwezi huo.
Kurejea kwake ni habari njema kwani Simba imekuwa ikimtegemea zaidi
Hamisi Kiiza huku washambuliaji wengine wakioneka kutomshawishi kocha
Dylan Kerr.