Baada Ya Kuondolewa Copa Del Rey Jana – Nini Hatma Ya Benitez/Madrid Dhidi Ya Getafe Leo Hii
Wakati bado wakiwa na
kumbukumbu ya kudhalilishwa nyumbani na mahasimu wao Barcelona, kisha
jana wakaondolewa kwenye michuano ya Copa Del Rey, leo hii kocha aliye
kwenye presha Rafael Benitez ataiongoza klabu yake ya Real Madrid
kuikaribisha Getafe Santiago Bernabeu. Getafe
ndio wageni wanaokaribishwa Bernabeu usiku wa leo na kwa namna hali
ilivyo hakuna mjadala wa kuwazungumzia – kwa sababu Madrid wamekuwa
wakiandamwa na sakata la kuondolewa kwenye Copa Del Rey baada ya hukumu
iliyotolewa jana – na leo mashabiki wa timu hiyo wanatarajia kuonyesha
hasira zao kwa kocha Rafael Benitez kwa kile kinachoitwa uzembe wa
kumpanga mchezaji ambaye alikuwa kafungiwa.
Madrid/Benitez wanaingia kwenye mchezo wa leo huku baadhi ya
mashabiki na wanachama wa klabu ambao kimsingi ndio wamiliki wa timu
wameonyesha nia ya kuchukua hatua za kisheria kwa klabu.
Katika mechi ya leo, James Rodriguez ambaye alikuwa kwenye ubora wake katika mechi vs Cadiz, anatarajia kuanza.
Jana ilitangazwa kwamba Benitez hakumuweka Marcelo katika kikosi cha
mechi ya leo kutokana na majeruhi lakini cha kushangaza mchezaji huyo
aliandika kwenye mitandao ya kijamii – “Nimepona kabisa na nipo tayari
kucheza.” – jambo hili limezidi kuongeza sintofahamu baina ya Benitez na
wachezaji wake. Leo
pia tunaweza kuona ‘BBC’ wakicheza kwa pamoja tena. Benzema alifunga
magoli 6 katika mechi 6 za kwanza za ligi lakini akaumia na akaanza
kuandamwa na kesi ya ulaghai dhidi ya Mathieu Valbuena – na sikza hivi
karibuni amekuwa ‘off form’. Cristiano, kwa upande mwingine anaonekana
kurudi kwenye mstari baada ya kufunga magoli matatu katika mechi 2
zilizopita. Usiku wa leo Ronaldo anakutana na timu ambayo ameshaifunga
magoli 18 katika mechi 10 zilizopita – zikiwemo hat trick 3 na magoli
mawili mawili mara 4.
Vikosi vinavyotegemewa kuanza leo na mifumo Getafe hawana rekodi nzuri ugenini maimu huu – wameambuliwa kupata sare
moja na magoli mawili tu katika mechi 6 zilizopita – rekodi mbaya zaidi
ya ugenini kwenye La Liga. Leo usiku wa leo watakuwa bila Juan
Rodríguez na hivyo wanategemewa kucheza kwa mfumo wa 4-1-4-1
No comments:
Post a Comment