Sababu za Messi kupewa Tuzo ya Mshambuliaji Bora La Liga na Kwanini Naamini Neymar na CR7 hawastahili kuwemo Top 3 Ballon D’Or
Sababu za Messi kupewa Tuzo ya Mshambuliaji Bora La Liga na Kwanini Naamini Neymar na CR7 hawastahili kuwemo Top 3 Ballon D’Or
kama tunavyojua wiki hii kulitolewa tuzo mbalimbali za Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ kwa msimu
uliopita. Mojawapo ni ile ya mshambuliaji bora wa msimu ambayo
ilichukuliwa na staa wa Barcelona, Lionel Messi.
Kati ya tuzo zilizotolewa, kipa bora, beki bora na kocha bora na
nyinginezo, lakini kidogo hii ya Messi imezua mjadala wa aina yake.
Wapo wanaoamini ilimfaa mpinzani wake wa karibu, Cristiano Ronaldo wa
Real Madrid, wakiegemea katika hoja ya kutwaa tuzo ya ufungaji ambapo
alimzidi Messi. Ni kweli, Ronaldo alifanya kweli katika ishu ya kucheka
na nyavu, kwani alimaliza msimu akiwa na hat trick nane, dhidi ya tano
za Messi.
Ni dhahiri unapozungumzia sekta ya ufungaji bora, Ronaldo ama CR7 kama
anavyofahamika, alistahili kuchukua tuzo hiyo, lakini kuna kitu
kinachowachanganya wengi. Unapozungumzia mfungaji bora na mshambualiji
bora ni vitu viwili, ingawa wote wanaweza kuwa na jukumu la kufunga.
Mshambuliaji bora ni aina ya mchezaji anayetegemea mfumo wa timu na
mfumo wa kocha na ili afunge lazima awe kwenye muunganiko wa timu na
kushiriki katika mipango yote ya kupatikana kwa bao. Hii ni sifa kuu
inayowatofautisha watu hawa. Mfungaji bora yeye anaweza kujitegemea
katika kulitafuta bao na asishiriki katika upatikanaji wa mpira hadi
kufika langoni mwa mpinzani.
Ni kutokana na aina hizo, tunapata aina mbalimbali za washambualiji.
Kuna wale ambao huitwa washambuliaji waliokamilika ‘complete strikers’,
hawa hufanya kazi zote kulingana na mfumo na hushiriki kikamilifu katika
kuisaidia timu kuanzia kuitafuta mipira mpaka kupatikana kwa bao. Hapa
utakutana na watu kama Luis Suarez, Messi, Sergio Aguero.
Takwimu za Ufungaji za Messi na Ronaldo msimu uliopita
Wapo wale waitwao waviziaji (poachers), hapa unakutana na kina Javier
Hernandez ‘Chicharito’ Filippo Inzaghi, Ruud van Nistelrooy. Pia kuna
kundi la washambuliaji wao kazi yao ni kumalizia mipira langoni (target
man) hapa wamo kina Oliver Giroud, Peter Crouch, Fernando Torres,
Gonzalo Higuain na wengineo. Matumizi yao uwanjani ni tofauti na kariba
ya ushambuliaji wa kina Messi. Kuna
vitu vya kumuangalia mshambuliaji bora kama straika nini majukumu yake
uwanjani kama kufunga. Kulingana soka la kisasa (modern football),
straika kwa sasa ni zaidi ya kufunga. Kuna wakati eneo ambalo upo
unaangalia jinsi ya kuisaidia timu yako na siyo suala la kufunga mabao
wewe mwenyewe, ila mchango wako kikosini kwa jumla, achilia mbali
kufunga kwako.
Ndiyo maana Jose Mourinho amekuwa akilumbana na Diego Costa, siyo
kusema anashindwa kufunga tu, ila anaangalia mchango wake uwanjani
katika kuisaidia Chelsea hasa kipindi hiki kigumu kwao.
Majukumu ya Messi si kuwa kama straika tu ndani ya Barcelona, ila
uwezo wa kutoa asisti na uwepo wake kwenye safu ya ushambuliaji husaidia
sana wenzake kufunga kiurahisi.
Mathalan angalia bao linalowania tuzo ya Puskas, anatoka katikati ya
uwanja, anachambua mchezaji hadi mchezaji na kutupia mpira kambani. Hayo
ndiyo mahitaji ya mshambuliaji katika soka la kisasa.
Matokeo ya kura zilizompa Messi tuzo ya Ushambuliaji Bora
Hivyo, Messi amekamilika, kulinganisha na CR7 ambaye kweli anajua
kufunga lakini hajakamilika kwa mantiki ya mahitaji ya soka la kisasa.
Hata takwimu zinaonyesha Messi alimaliza msimu akiwa na asisti 18 dhidi
ya 16 za CR7
Pia nigusie kuhusu tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Messi, CR7 na
Neymar. Kwa mtazamo wangu, sioni kama CR7 alitakiwa kuingia safari hii,
ukilinganisha na wengine walivyofanya vizuri. Ninaamini ilikuwa ni fursa
kwa mmoja wa Juventus alitakiwa kuwemo katika majina haya.
Hakuna aliyekubali kuwa msimu uliopita Juve ilikuwa katika ubora wake
na kweli walistahili kutoa mchezaji mmojawapo katika kinyanganyiro
hiki. kati ya Paul Pogba ama Arturo Vidal mmojawapo alitakiwa kuingia. Mimi ni shabiki mkubwa wa Ronaldo, sidhani kama alistahili kuingia kulinganisha na wenzake walivyofanya mengi mazuri.
Niliwaangalia Neymar na Luis Suarez, siamini kama Neymar alitakiwa
kuwemo mbele ya Suarez, labda pengine kwa kuwa Suarez alikuwa na adhabu
kwa timu ya taifa. Suarez ana mchango mkubwa tena sana kuliko Neymar
ambaye naweza kusema wanajaribu kupewa promo na makampuni makubwa kwa
ajili ya kujitangaza kwa tija ya biashara nchini Brazil, lakini
vinginevyo hakustahili mbele ya Mruguay huyo.
Ila kama ilikuwa sababu ya adhabu ya kinidhamu kwa Suarez, Neymar
anastahili kuwemo lakini kwa mtazamo wangu, Ronaldo angetoka na kuingiza
jina mojawapo kati ya Vidal ama Pogba kutokana na mafanikio makubwa
waliyokuwa nayo msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment