Nyota
wa kikapu LeBron James amekamilisha ndoto yake ya kuiwezesha timu yake
ya Cavaliers kubeba ubingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani
maarufu kama NBA.
Cavaliers
wamewatwanga wapinzani wao wakubwa Golden State Warriors kwa point
93-89 na kufanikiwa kushinda mchezo wa mwisho wakiwa ugenini.
Ilikuwa
ni mechi ya kukata na shoka na Cavaliers walionyesha wamepania kufanya
makubwa ugenini licha ya nyota Stephen Curry kuonekana kikwako kwao.
Kwa mara nyongine, James aliibuka bora katika mechi hiyo baada ya kumaliza akiwa na pointi 27 points, asisti 11 na ribaundi 11.
No comments:
Post a Comment