Wakati
pazia la usajili likiwa limefunguliwa juzi Jumatano, uongozi wa Azam
umetamka hadharani kuwa hautakuwa na muda wa kufanya usajili wa ndani
kama ambavyo wamekuwa wakifanya na badala yake watajikita katika kuibua
vipaji vya wachezaji wao vijana kutoka kikosi B kwa ajili ya kuwapa
uzoefu.
Kwa
kipindi kirefu Azam imekuwa ikifanya usajili wa wachezaji ambao tayari
wana uzoefu na ligi kuu ambapo msimu uliopita waliwanasa Ramadhan
Singano ‘Messi’ kutoka Simba na Ame Ali ‘Zungu’ kutoka Mtibwa.
Msemaji
wa Azam, Jaffar Idd, amesema kuwa maamuzi hayo yameamuliwa na viongozi
wa timu hiyo baada ya kuona kuwa wachezaji hao hawana msaada mkubwa
ndani ya kikosi hicho kutokana na wengi kucheza bila ya mapenzi.
“Kwa
msimu huu tumeazimia kutofanya usajili wa wachezaji wa ndani, badala
yake tutajikita zaidi katika kupandisha wachezaji kutoka kikosi B ambao
tumeona sasa ni muda wao muafaka kuwatangaza.
“Maamuzi
hayo yamekuja baada ya kuona kuwa hawa tunaowasajili mara nyingi
wamekuwa wakicheza bila kujituma kuipigania timu na mwishowe tunakuja
kuwaacha tu,” alisema Jaffar.
No comments:
Post a Comment