Thursday, May 7, 2015

IVO MAPUNDA AOMBA MKATABA MPYA SIMBA


Na Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Mkataba wa Ivo na Simba umebakisha siku 13 kumalizika.'
KIPA mkongwe wa Simba, Ivo Mapunda, amesema ana matumaini ya kuendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao licha ya kutokuwapo kwa dalili zozote za mazungumzo na viongozi wa timu hiyo.
Ivo mwenye mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba tangu atue kwenye mzunguko wa pili msimu uliopita akitokea Gor Mahia ya Kenya, ameuambia mtandao huu kuwa angependa kuendelea kuichezea timu hiyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya, lakini ameuachia uongozi na benchi la ufundi uamue.
“Ninaamini nimefanya kazi nzuri katika msimu mmoja na nusu niliofanya kazi hapa Simba, lakini kama mchezaji siwezi kulazimisha nimewaachia viongozi na benchi la ufundi kama wataona ninafaa, watanifuata tuzungumze. Ninadhani hatutoshindwa kufikia makubaliano kwa sababu tumefanya kazi kwa pamoja na tunajuana,”amesema Ivo.
Mkataba wa Ivo mwenye umri wa miaka 31, utamalizika Mei 20, mwaka huu na kiwango chake kimekuwa msaada kwa Simba, licha ya makosa machache yaliyoigharimu timu yake msimu huu na kusababisha kupoteza baadhi ya mechi ikiwamo ile ya Kagera Sugar FC iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo alimtemea Atupele Green mpira uliorushwa na Salum Kanoni na kumweka katika utata.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif