MWADUI YAVUNJA UKIMYA JUU YA KOCHA WAO.
Uongozi wa timu ya Mwadui ya mkoani Shinyanga umefunguka juu ya taarifa za kuachana na kocha wake.
Taarifa mbalimbali zilidai kuwa kuna uwezekano wa wageni
hao kwenye ligi kuu msimu ujao kuachana na Jamhuri kiwelu na kusaka
kocha mwingine.
Lakini Mpenja blog ilibisha hodi kwenye mgodi huo wa almasi
na kuzungumza na katibu kuu wa timu hiyo Ramadhani Kilao ili kujua
ukweli na undani wa taarifa hiyo, ambapo katibu huyo alikanusha taarifa
hizo.
"Hizi taarifa hata sijui zinatokea wapi,kwetu hatuna hizo
taarifa lakini nashangaa kuona zinazungumzwa kila siku,Julio ni kocha
wetu labda yeye atuache ".Alisema Kilao.
Alipoulizwa kuhusiana na taarifa za kuwepo mpango wa kuleta
kocha wa kigeni,katibu huyo amesema hawajalifikiria hilo lakini alidai
kwamba uwezo wanao wa kumchukua kocha yeyote awe wa ndani au nje ya
nchi.
"Uwezo wa kuleta kocha tunao tena hata tukitaka watatu,lakini kwasasa hilo hatujalifikiri"Alisema.
Kocha mkuu wa Mwadui Jamhuri kiwelu alifanikiwa kuipandisha
daraja timu hiyo na baada ya kufanya hivyo aliekea kukinoa kikosi kama
kocha msaidizi wa muda lakini baada ya kuondoka kwa kocha James Nandwa
kikosini hapo Julio sasa ndiye kocha mkuu wa wagasi wa kaya Coastal
Union.
No comments:
Post a Comment