Bondia
Kutoka Ufilipino Manny Pacquiao amefanyiwa upasuaji wa bega lake
alilodai kuwa ndiyo iliyopelekea yeye kushindwa na Floyd Mayweather
jumapili iliyopita.
Bondia huyo tayari anakabiliwa na kesi moja huko Nevada kwa kutosema ukweli kuhusiana na hali yake ya afya kabla ya pigano.
Hata
hivyo daktari wake Neal ElAttrache, amesema kuwa amefurahia matokeo ya
upasuaji huo licha ya ripoti kudokeza kuwa Pacquiao anahitaji muda wa
mwaka mmoja kuuguza jeraha hilo.

Mayweather amesema hana pingamizi ya kuzichapa dhidi ya Pacquiao
Pacquiao mwenye umri wa miaka 36 alinyimwa dawa ya kupunguza maumivu kabla ya mechi alipokuwa akilalama kuteguka bega.
Hata
hivyo imebainika kuwa kabla ya pigano hilo shirikisho la riadha na
masumbwi ya kulipwa katika jimbo la Nevada lilipuzilia mbali ombi la
shindano hiyo kwani haikuwa imearifiwa awali.
NAC
inapendekeza kushtakiwa kwa bondia huyo mfilipino kwani hakusajili
maumivu ya aina yeyote katika fomu maalum siku moja kabla ya pigano.

Manny anakabiliwa na kesi moja huko Nevada kwa kutosema ukweli kuhusiana na hali yake ya afya kabla ya pigano.
Kutokana
na masaibu yake, mwanamasumbwi wa kulipwa Floyd Mayweather,
38,amejitokeza na kusema kuwa hana pingamizi ya kuchuana tena dhidi ya
Pacquiao ila katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Awali mwanadondi huyo alikuwa amesema yuko tayari kuzichapa dhidi ya Muingereza Amir Khan miongoni mwa wanandondi wengine.
No comments:
Post a Comment