JACKSON Mayanja Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa sare tasa waliyoipata mbele ya AS Kigali ya Rwanda itajibiwa kibabe Dar. Jana KMC, ilitupa karata yake ya kwanza kwa kucheza na AS Kigali na ubao kusoma 0 kwa wenyeji AS Kigali pamoja na wageni KMC. Mchezo wa marudio unatarajiwa kuwa kati ya Agosti 23-25 jiji Dar. Akizungumza na
Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa wachezaji walijituma kutafuta matokeo
wamekutana na ushindani mkubwa hivyo wanajipanga mchezo ujao.
“Mchezo ulikuwa
mgumu na kila mchezaji amefanya kile ambacho nimemuelekeza licha ya
kutopata matokeo jambo jema ni kwamba hatujafungwa. "Kwenye marudio tutapambana kupata matokeo chanya kwani tutakuwa nyumbani na sapoti kubwa ya mashabiki," amesema.
USHINDI ni matokeo ya juhudi na kujituma kwa wachezaji ambao wamepewa jukumu la kupeperusha Bendera ya Taifa kimataifa.
Timu ya Taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ imefikia hatua yake ya kwanza kwenye michuano ya
Chan baada ya kupata ushindi mbele ya wapinzani wao wakubwa Kenya.
Haikuwa kazi
rahisi kupenya hatua hii kwani mwanzo kwenye mchezo wa nyumbani hakuna
ambaye alipata matokeo chanya hata mchezo wa marudio pia dakika tisini
zilikamilika kwa timu zote kumaliza bila kufungana.
Ni dua za
mashabiki na umakini wa wachezaji kutumia vema nafasi ya matuta kupata
ushindi hatimaye wamepenya hatua ya kwanza kwenye michuano hii mikubwa.
Shukrani kubwa
zinarudi kwa mashabiki ambao wapo bega kwa bega na timu licha ya kupitia
changamoto za kutopata matokeo mchezo wa kwanza.
Mashabiki wamekuwa na timu kwa kuipa sapoti jambo ambalo limeongeza nguvu za kutosha kwa wachezaji kutimiza wajibu wao uwanjani.
Kitu cha msingi
kwa wachezaji ilikuwa ni kutimiza majukumu yao uwanjani hicho ndicho
wamekifanya na mashabiki wamekuwa wakiwapa sapoti wachezaji jambo ambalo
limeongeza nguvu.
Ikumbukwe kuwa mashabiki wa timu ni muhimili kwa kupata matokeo kutokana na sapoti ambayo wanaitoa uwanjani.
Uwepo wao ni sawa
na mchezaji wa 12 jambo ambalo linaongeza nguvu kwa wachezaji kupambana
kwa ajili ya Taifa pia kuona ile shauku ya mashabiki inakatika.
Pongezi kubwa
kwao licha ya wengi kushindwa kujitokeza nchini Kenya ila bado walikuwa
wakiishi kwenye vichwa vya wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Kwenye mchezo wa
kwanza ambao ulichezwa uwanja wa Taifa mashabiki wengi kutoka pande
mbalimbali za Tanzania waliwasili uwanja wa Taifa kuipa sapoti timu ya
Taifa.
Licha ya
kushindwa kupata matokeo chanya bado mashabiki waliendelea kuungana na
timu hiyo mazoezini mpaka siku inaondoka kwenda Kenya ni moyo wa upendo.
Serikali pia
haijaiacha timu ya Taifa kwenye mazingira ya unyonge kwani wamekuwa nao
bega kwa bega kupitia viongozi ambao wametoa sapoti kubwa.
Hili ni jambo la
kujivunia kwa hapa ambapo tupo kwa sasa kuna kitu ambacho ,mashabiki
wanapaswa waongeze ni kushangilia hata pale timu inapokosa matokeo.
Kasumba hii
imekuwa ikiwasumbua mashabiki wengi kwani wamekuwa wakitazama ni muda
gani wa kushangilia mpaka mchezaji apige chenga ama awe na mpira hapo
watashangilia ila kama hakuna tukio basi kushangilia kunakoma.
Kuna umuhimu wa
kuwa na mabadiliko makubwa kwa upande wa ushangiliaji kwa mashabiki
wakati ujao ili kuendelea kupata matokeo hata wakati ule timu inapokuwa
nyuma kwa kufungwa.
Shabiki yeye ni
mchezaji wa 12 hivyo kama atakaa kimya anamaliza nguvu za mchezaji wa 11
ndio maana kuna timu ambazo zimekuwa zikipewa adhabu kwa kutoruhusu
mashabiki kuingia uwanjani zimekuwa zikishindwa kupata matokeo chanya.
Muda wetu sasa
kubadilika huku tuliko na kufanya mengine makubwa kwenye masuala ya
ushangiliaji pamoja na kutoa sapoti kwa timu zetu.
Stars bado kazi
inaendelea kwani mchezo unaofuata ni dhidi ya Sudan hapo ni lazima
kupambana kwa juhudi kabla ya kumenyana na Rwanda ndipo kuibukia kwenye
michuano ya Chan.
Kila kitu
kinawezekana kwa kujipanga na kujiamini wakati wa kufikia mafanikio
ambayo tumeyakosa kwa muda mrefu ni sasa mashabiki enedeleeni kutoa
sapoti bila kuchoka.
Kwa kufanya hivyo kutaongeza msukukumo kwa wachezaji kucheza kwa juhudi na kutimiza majukumu yao kwa wakati.
KOCHA
Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa bado kikosi chake hakijawa na
maelewano mazuri jambo ambalo liliwapa taabu kupata matokeo kwenye
mchezo wao wa kwanza dhidi ya Township Rollers. Yanga jana imelazimisha sare dhidi ya Township Rollers, mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa kwa kufungana bao 1-1. Mchezo wa marudiano wa kimataifa unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana. "Wachezaji
wangu bado wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kuelewana wakiwa ndani
ya uwanja jambo ambalo linaleta ugumu kwenye kupata matokeo uwanjani. "Kwa
sasa hesabu ni kuona kwamba tunakuwa na kikosi imara ambacho kitapata
matokeo kwenye mchezo wetu wa marudio, mashabiki waendelee kutupa sapoti
katika hili, nami nitafanyia kazi makosa yote," amesema
UONGOZI
wa Simba umesema kuwa Yanga wanastaihili pongezi ila wamewaangusha
wananchi kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Township
Rollers jana uwanja wa Taifa. Ofisa
Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa, kazi kubwa ambayo Yanga
walipaswa waifanye ni kupata matokeo chanya kwa kuwa walikuwa nyumbani. "Hongereni
Yanga kwa kupata sare ya nyumbani ila haijawa sawa kwa Wananchi kwa
kuwa mlikuwa na sapoti ya mashabiki na imekuwa ngumu kuitumia. "Raha ya mchezo wa nyumbani ni kuwa na mashabiki, hivyo tutawaonyesha namna ya kufanya kwenye mchezo wetu wa marudio," amesema. Simba
jana ililazimisha sare tasa dhidi ya UD Songo ya Msumbiji mchezo wao
marudio unatarajiwa kuwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Taifa na Yanga
nao watakuwa ugenini nchini Botswana.
MSIMU
uliopita, kikosi cha Ndanda FC kilinusurika kuteremka daraja hadi la
kwanza “kimkandamkanda” kwa kuwa mambo yalikuwa mabaya kupita kiasi.
Licha
ya kuwa kati ya timu zinazoonekana zinakwenda kuteremka daraja. Ndanda
FC ndiyo ilikuwa timu ambayo imepoteza mwelekeo zaidi baada ya uongozi
wake kuonekana umepotea njia.
Kibaya
zaidi, wachezaji wake wengi nao walionekana wamepotea na wamekata tamaa
na hata kufikia kulalamika kwenye vyombo vya habari.
Baadhi
ya mambo waliyolalamika ni kukosa hata fedha kwa ajili ya mlo. Yaani
walikuwa kambini na walikuwa wakishinda njaa, kitu ambacho ni kibaya
zaidi cha mwisho unapozungumzia kundi la wanadamu.
Mnaweza
kukosa jambo jingine lakini si chakula ambayo ni huduma namba moja kwa
mwanadamu. Lakini wachezaji hao walisema nafuu yao ilikuwa ni mlo mmoja
kwa siku, jambo ambalo si zuri hata kulisikia na sikuwahi kusikia
kiongozi wa Ndanda FC akilikanusha.
Waliokuwa
wakilalamika ni kati ya wachezaji wakongwe kabisa wa Ndanda FC na hata
watu wa benchi la ufundi. Hili halikuwa jambo zuri lakini hongera kwao
kwa kuwa walijitutumua na mwisho Ndanda FC ikabaki Ligi Kuu Bara.
Baada
ya hapo, nilitegemea kuona wanajipanga. Ingawa jambo hilo halikufanyika
mapema sana kwa kuwa inaonyesha hata usajili wa Ndanda FC haukuwa ule
unaoonyesha kuna mabadiliko makubwa.
Huenda
uongozi haukuwa na fedha na mipango haikuwa bora kuhakikisha fedha
nyingi zinapatikana. Lakini baada ya dirisha la usajili kufungwa,
nimeona kuna Kampuni Motsun Group Ltd kupitia ya bidhaa yake ya mabati
ya Kiboko imejitokeza kuidhamini Ndanda FC.
Ndanda
FC wamepata udhamini wa mwaka mmoja kuitangaza Kiboko. Hawakusema kiasi
gani lakini tayari wameongeza kitu mfukoni mwao ambacho kitawasaidia
kuwa tofauti na awali.
Lakini
lazima ukumbuke kuwa Ndanda FC wanaingiza fedha kupitia wadhamini wa
Ligi Kuu Bara, Vodacom pia Azam TV ambazo zinaweza zisiwe nyingi sana
lakini zinasaidia gharama kadhaa za uendeshaji tofauti na zamani.
Msimu
uliopita pia walipokea fedha kutoka Vodacom na Azam TV lakini
wakashindwa kusimama na kufanya vizuri. Ujio wa Kiboko ni jambo jingine
bora wanalopaswa kulitumia kama chachu ya mabadiliko.
Ninaamini
Kiboko wangeweza kutodhamini katika soka na kwenda kwingine
kujitangaza. Uamuzi wao kuingia kwenye soka lazima wapate faida na
mafanikio yao na ikiwezekana wanaongeza mkataba ni kuona Ndanda FC
inafanya vizuri.
Ndanda
FC wasifurahie fedha tu wanazopata, badala yake wanapaswa kujua kwamba
wadhamini wao pia kuna jambo wanategemea kutoka kwao na wakifurahia
zaidi basi wataweza kuendelea na udhamini na ikiwezekana kuongeza zaidi,
hili ninaamini linaweza kutokea.
Lakini
anayeweza kulifanya litokee, ni Ndanda wenyewe ukianza na viongozi na
wachezaji pia. Wanaposaidia lazima wajue wana deni la kumtangaza
mdhamini wakiwa na mafanikio na ikiwezekana suala la nidhamu linapaswa
kuwa juu zaidi ukilinganisha na msimu uliopita.
Kesho
kama Ndanda FC itateremka daraja, maana yake watakuwa pia wamemshusha
mdhamini wao kwa maana ya kwamba hatakuwa na nafasi ya kuongeza mkataba
tena. Lakini wakifanya vema na ikiwezekana kufikia angalau ule uwezo
waliouonyesha Mbao FC ya Mwanza msimu uliopita, huenda hata wadhamini
wenye donge nono wanaweza kujitokeza zaidi.
Ndanda
FC mna deni kubwa la kuonyesha tofauti kwa kuwa mwanadamu bora ni yule
anayejifunza kupitia makosa yake. Kama msimu unaoanza wiki chache zijazo
utaendelea kuwa wa shida kwenu, basi lawama zibaki kwenu na mtaonyesha
ni watu wa kubahatisha mambo.
Fanyeni
vizuri ili muwe sehemu ya kuwashawishi wadhamini wengine kwamba hata
timu ndogo zinaweza kudhaminiwa na kuwatangaza vizuri wadhamini.
Xabi Alonso na Phillip Lahm walikuwa moja ya nguzo za
mafanikio katika klabu ya Bayern Munich lakini msimu huu Bayern
wanaingia bila wazoefu hao wawili ambao wametundika daluga.
Lakini bado Bayern wana matumaini kuchukua ubingwa kwa mara ya 6
mfululizo huku maingizo mapya haswa la James Rodriguez na Corentin
Tolliso yakiwapa matumaini ya kutetea ubingwa wao na leo watakuwa
dimbani kufungua ligi dhidi ya Bayern Leverkusen.
Msimu huu Borussia Dortmund wanaweza kuwa wapinzani wakubwa wa Bayern
tofauti na ule uliopita ambapo klabu ya Rb Leizpg ndio walionekana
kuitishia Bayern na kumaliza katika nafasi ya pili.
Lakini Dortmund wanaweza kuwa vizuri kama watafanikiwa kuwabakisha
Osmane Dembele na Pierre Aubemayang ambao wako kwenye tishio la kuihama
klabu hiyo katika dirisha hili la usajili na kocha wao mpya Peter Bosz
anategemewa kuwa mhimili mpya BvB.
Rb Leizpg wamefanikiwa sana katika dirisha hili la usajili kubakisha
nyota wao wakubwa Emil Forsberg na Naby Keita aliyekuwa akiwinda sana na
Liverpool na hii inatoa tumaini kwa mashabiki wao.
Lakini Rb Leizpg watakuwa na Champions League hii inaweza kuwafanya
wachoke na kiwatokee kilichowatokea klabu ya Leicester City msimu
uliopita ambapo wingi wa michuano uliwafanya wapwaye sana.
Maingizo mapya ndani ya Rb Leizpg akiwemo mshambuliaji toka PSG Kevin
Augustin na Bruma aliyesajiliwa toka Galatasaray inaweza kwa kiasi
fulani kuipa nguvu Leizpg katika msimu huu wa ligi.
Bayern Leverkusen wamepoteza wachezaji wawili muhimu Javier Hernandez
Chicharito aliyekwenda West Ham na Calhanoglu aliyetimkia Ac Milan ni
pigo kwao lakini kocha moya Heiko Herlich anatarajiwa kutoa mbinu mpya
kuibeba Leverkusen.
Hoffeinman bado hawana uhakika wa kufudhu Champions League na
wasipofudhu watabaki Europa League msimu ujao wakiungana na Hertha
Berlin pamoja na Cologne na hii itazifanya timu hizo kuwa na michuano ya
ziada inayoweza kuwapa mzigo wa ziada katika ligi.
Stuttgart na Hannover wamepanda ligi msimu huu lakini Stuttgart sio
wageni sana kwenye ligi kwani mwaka 2015/2016 ndio walishuka daraja na
mwaka huu wamerudi, kimbembe kipo kwa Hannover ambao tayari wameanza
kutabiriwa kushuka daraja.
Real
Madrid imeendelea kutawala katika duniani baada ya kuingiza wachezaji
saba kati ya 24 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Shirikisho la Soka
la Kimataifa (Fifa).
Kutoka Real Madrid, wachezaji waliongia kwenye tuzo bora ya mchezaji bora Fifa ni
Cristiano Ronaldo, Dani Carvajal, Toni Kroos, Luka Modric, Keylor Navas na Sergio Ramos.
Hiyo inaifanya Madrid kuwa timu iliyoingiza watu wengi zaidi katika listi hiyo.
Everton
imeitwanga Hajduk Spilit kwa mabao 2-0 na kujiweka katika hatua nzuri
ya kufuzu katika hatua ya makundi ya Europa League.
Mabao
ya Everton yamefungwa na Michael Keane na Idrissa Gueye katika mechi
hiyo ambayo kipindi cha kwanza ilikabiliwa na tafrani kutoka kwa
mashabiki wa Hadjuk hadi kusababisha mpira kusimama.
Kipindi
cha pili kilikwenda vizuri na hakikuwa na bao hata moja kwa kuwa
Everton hawakuweza kuongeza na wageni nao hawakupata bao. Mechi ya
marudiano ni Alhamisi ijayo, Everton inayodhaminiwa na SportPesa,
itakuwa ugenini.
KWA NYIMBO MPYA NA MATUKIO YOTE YA KIMICHEZO
,SIASA N.K, NENDA YOUTUBE NA UTAFUTE MBEGEZE TV KISHA BONYEZA NENO
SUBSCRIBE USPIITWE NA KILA KITU
Siku zinakwenda tu na masaa yanakatika kuelekea ufunguzi wa
ligi kuu nchini Uingereza Epl hapo mwezi wa 8 na kila timu inapambana
kuhakikisha inakuwa tayari kwa ajili ya mapambano hayo.
Chelsea bado wanachechemea kusaini striker namba 9 nafasi ambayo ni
lazima wasajili kama Diego Costa ataondoka kama inavyoonekana, japokuwa
tayari wamefanya sajili kadhaa ila hii ni lazima kwao.
Alvaro Morata anawindwa na Chelsea, pamoja na kutoanza michezo mingi
msimu uliopita lakini alifunga magoli 15 na kuassist 8 na ni kati ya
washambuliaji ambao wakipewa nafasi anaweza kucheka na nyavu mara nyingi
zaidi lakini dau lake sio la kitoto inabidi uwe na pesa kuanzia £70m.
Andrea Belotti, kwa watu wanaoangalia sana Serie A wataelewa unyama
ulioko ndani ya Muitalia huyu,michezo 34 kapasia kamba mara 26 na
kuassist mara 7 hii inaonesha kila mchezo amefanya jambo, na kwa uwezo
wa Belotti hakika Conte anafaa kumsimamisha namba 9.
Pierre Aubemayang, kati ya wachezaji ambao ukimuelezea ubora wake
hutumii nguvu nyingi ni Mgabon huyu, namba hazidanganyi na mabao 31
aliyofunga toka ajiunge na BVB yanAeleza ubora wake na msimu uliopita
alikuwa ndio kinara wa mabao katika Bundesliga.
Sergio Kun Aguero, inasemekana City wako tayari kumuuza Aguero ili
kuongeza pesa za kumpata Sanchez, msimu uliopita Kun alimaliza akiwa na
mabao 20 na assist 3 huku wastani wa kufunga kila baada ya dakika 120
dakika ambazo ni Harry Kane tu mwenye chache zaidi inaonesha jinsi Kun
anavyoweza kuziba pengo la Costa.
All in All Chelsea inabidi wajipange haswa maana mastriker hao wote
kuwapata ni mbinde kubwa sana kwani kila unayemgusa klabu yake inataka
kuanzia £60m na huku Conte analalamika kuhusu bajeti ya usajili iliyopo,
kama Chelsea wakishindwa kununua striker ni bora wakae chini na Costa
wayamalize.
KWA NYIMBO MPYA NA MATUKIO YOTE YA KIMICHEZO ,SIASA N.K, NENDA YOUTUBE NA UTAFUTE MBEGEZE TV KISHA BONYEZA NENO SUBSCRIBE USPIITWE NA KILA KITU
Emmanuel Adebayor aliitumikia Real Madrid kwa kipindi kifupi
mwaka 2011. Lakini hakuendelea kubaki Santiago Bernabeu, pamoja na
kumvutia kocha Jose Mourinho, japokuwa mchezaji mwenyewe alikuwa anataka
kubaki na Los Blancos.
Akiongea katika mazungumzo na kituo cha BBC cha Uingereza, Adebayor
amefunguka kwamba moja ya sababu zilizopelekea Real Madrid kutoendelea
nae ilikuwa ni barua iliyotumwa na ndugu yake wa kiume kwenda kwa maboss
wa Bernabeu, ikiwashauri viongozi wa Real kutomsajili nahodha huyo wa
Togo.
Adebayor anasema alifanya kila kitu ili aweze kuendelea kubaki Madrid. “Nilifanya
kila kitu ili niweze kubaki jijini Madrid, lakini kwasababu ya kaka
yangu sikuweza kubaki pale kwasababu alituma barua ….. barua rasmi
kutoka kwa familia ya Adebayor ikiwaeleza Madrid kwanini hawatakiwi
kunisajili. Hii ilichangia sana kuniharibia mipango yangu Santiago
Bernabeu,” alieleza Adebayor, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Basakhesir.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na Tottenham ana uhusiano mbaya
sana na familia yake, familia ambayo anasema hata kuzungumza nao ni mara
chache sana.
Anasema familia yake huwa haimtafuti hata kumsalimu pale anapopata
majeruhi au matatizo mengine, kipindi pekee wanachowasiliana nae ni
wakati wanahitaji msaada wa kifedha tu.
Katika kuonesha jeuri ya pesa matajiri wa kiarabu
wanaoimiliki klabu ya PSG wamepiga hodi katika klabu ya Barcelona tayari
kwa ajili ya kuvunja rekodi ya dunia kumtwaa mshambuliaji wa klabu hiyo
Neymar.
Taarifa zinasema kiasi cha zaidi ya £200m ambayo ni mara mbili na
zaidi ya pesa zilizotumika kumnunua Paul Pogba ambaye kwa sasa ndio
anashikilia rekodi ya usajili ya dunia kwa sasa.
Ripoti zinasema klabu ya PSG inataka kutumia mwanya wa Neymar kukosa
uhuru wa kucheza free mbele ya Messi hivyo wanataka kutuma ofa ya
karibia £222m ambayo ni wazi itawashawishi Barcelona kumuuza.
Katika dili hiyo Neymar atakula £30m kila mwaka na uwepo wa Dani
Alves katika kikosi cha PSG unaweza kuwa ushawishi mkubwa kwa Neymar na
PSG wanaweza kumtumia mlinzi huyo kumshawishi Neymar.
Habari zinasema Neymar hana furaha na Barcelona kwani ni ngumu
kuchukua tuzo ya Ballon D’Or ukicheza mbele ya Suarez na Messi ambapo
washambuliaji hao wanaminya uhuru wa Neymar akiwa uwanjani.
Lakini klabu ya Barcelona yenyewe wamesema hawana mashaka hata kidogo
kuhusu kuondoka kwa Neymar kwani suala hilo katika soko la usajili ni
gumu kutokea na wao wanapuuza uvumi wote kuhusu Neymar.
Josep Vives msemaji wa klabu ya Barcelona amesema “hata hatuwazi
kuhusu hilo kwani ni ngumu kutokea, ni mchezaji wetu muhimu sana na
sidhani kama tunaweza kupokea ofa yoyote juu yake.”
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesisitiza kikosi chake kitafanya
vizuri msimu ujao licha ya kutokuwa na usajili wa mbwembwe.
Bwire amesema Shooting hawafanyi mambo kutaka kujionyesha badala yake ni mipango sahihi.
Tuesday, July 4, 2017
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 04.07.2017 na RAM MBEGEZE
TADHALI SUBSCRIBE MBEGEZE TV YOUTUBE KWA HABARI MBALIMBALI ZA KIMICHEZO
Mshambuliaji wa
Uhispania na Chelsea Diego Costa, 28, anataka kuondoka Stamford Bridge
kwa wakati anaotaka yeye, na jambo hilo linachelewesha hatua ya Chelsea
kumsajili Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton (Daily Mirror).
Antonio
Conte anataka Chelsea watoe hata pauni milioni 100 kumsajili Romelu
Lukaku, kama Everton wanataka kiasi hicho ili kumuuza (The Telegraph).
Mshambuliaji
kutoka Argentina Lionel Messi, 30, atasaini mkataba mpya Barcelona mara
tu atakaporejea kutoka kwenye fungate yake baadaye mwezi huu (Goal).
Paris
Saint-Germain wanajiandaa kupanda dau jipya la kumtaka mshambuliaji wa
Monaco Kylian Mbappe, 18, na wamewasiliana na wawakilishi wa mchezaji
huyo (L'Equipe).
Arsenal wanapanga kutoa pauni milioni 70
kuwasajili viungo wawili kutoka Sporting Lisbon ya Ureno, William
Carvahlo, 25, na Gelson Martins, 22 (A Bola).
Arsene Wenger atakutana na Alexis Sanchez, 28, na
Hector Bellerin, 22, wiki hii kujaribu kuwashawishi wasiondoke Emirates
(The Sun).
Everton wana uhakika wa kumrejesha Goodison Park Wayne Rooney, 31, kutoka Manchester United msimu huu (TalkSport).
West
Ham United wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester
United Javier Hernandez "Chicharito" , 29, kutoka Bayer Leverkusen
(Telegraph).
Liverpool wanapanga kutoa euro milioni 12 kumsajili kipa wa Sevilla Sergio Rico (ABC Sevilla).
Chelsea
wameonesha dalili kuwa wapo tayari kutoa pauni milioni 60 kumsajili
beki wa kushoto Alex Sandro kutoka Juventus (Telegraph).
Barcelona
wanaongoza katika mbio za kumsajili beki wa Juventus Leonardo Bonucci.
Chelsea wanataka kumsajili beki huyo, lakini yeye angependa kwenda
Barcelona (Daily Mirror).
Inter Milan wanataka kupanda dau la kumtaka mshambuliaji wa PSG Angel di Maria (Tuttosport).
Kipa wa zamani wa Arsenal Jens Lehmann anatarajia kurejea Emirates kama mmoja wa makocha wa kikosi cha kwanza (Guardian).
Gianluigi Donnarumma amekataa kuhamia Paris-Saint-Germain na amekubali kusaini mkataba mpya kusalia AC Milan (Sky Sport Italia).
Kiungo
wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, 24, amefanya mazoezi na
Birmingham City, akitaka kuhamia klabu hiyo kutoka Lazio (Daily Mirror).
Southampton
wanataka kukamilisha usajili wa pauni milioni 8.75 wa mshambuliaji Yann
Karamoh, 18, ambaye ana mzozo na klabu yake ya Caen ya Ufaransa (Sun).
Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya utakaompeleka hadi mwaka 2020 (AS).
Meneja
wa Manchester United Jose Mpurinho anakasirishwa na hatua ya klabu hiyo
kutosajili wachezaji zaidi ya Victor Lindelof, 22, peke yake mpaka sasa
(Daily Mirror).
Jose Mourinho anataka mshambuliaji Alvaro Morata,
24, kutoka Real Madrid na kiungo Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea
wajiunge na kikosi chake kabla ya Jumapili watakapoanza safari ya
Marekani ya mechi za maandalizi (Daily Star).
Real Madrid 'wamekomaa' na Alvaro Morata hadi Manchester United watakapotoa pauni milioni 79 (Marca).
Kiungo
kutoka Guinea Naby Keita, 22, anataka kuhamia Liverpool, lakini klabu
yake RB Leipzig inataka pauni milioni 70 (Daily Mirror).
Crystal Palace wameshindwa kulipa pauni milioni 30 wanazotaka Liverpool kwa ajili ya beki wa kati Mamadou Sakho, 27 (Guardian).
Manchester United wanajiandaa kupanda dau kumsajili beki Marc Bartra, 26, kutoka Borussia Dortmund (Manchester Evening News).
Newcastle bado hawajafanikiwa kumsajili kipa Pepe
Reina, 34, kwa kuwa Napoli hawajapata mtu wa kuziba nafasi yake
(Newcastle Chronicle).
Leicester City wamefanya mazungumzo ya awali na Sevilla kuhusu usajili wa kiungo Vicente Iborra (Sky Sports).
Kipa Wojciech Szczesny amerejea Arsenal kutoka Roma alipokuwa kwa mkopo kwa miaka mwili (Instagram).
Habari
zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha
kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii
(Kiingereza): Tetesi kuhusu uhamisho Ulaya
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.
WINGA Jamal Mnyate aliyekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha
Simba amefunguka na kusema kuwa bado ataendelea kuwemo katika klabu hiyo
kutokana na kuwa na mkataba na timu hiyo.
Mnyate alisajiliwa na Simba akitokea katika klabu ya Mwadui kwa
mkataba wa miaka miwili lakini tangu alivyosajiliwa alifanikiwa kucheza
mechi kadhaa kutokana na mara nyingi akiwa anasumbuliwa na majeruhi.
“Kwa hivi sasa ni ngumu kusema msimu ujao nitakuwa wapi, kwasababu
bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Simba kikubwa mimi na wasikiliza wao
waajiri wangu watakavyonambia kuhusu hatima yangu,”alisema.
Mnyate alisema hawezi kuzungumza chochote kwa sasa kutokana na kuwa
bado yupo chini ya mkataba na timu hiyo, lakini angekuwa ameshamaliza
nao mkataba angekuwa huru kusema msimu ujao angeenda timu gani.
Aidha,Mnyate amewapongeza Viongozi wake kwa usajili walioufanya kwa
kuwarudisha wachezaji wao wa Zamani kama Emmanuel Okwi,Shomary Kapombe
ambao walikuwa tishio ligi kuu.
Kiungo nyota wa Simba, Muzamiru Yasin amegeuka lulu kwa baadhi ya timu za Afrika Kusini.
Muzamiru
yuko Afrika Kusini akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
katika michuano ya Cosafa ambayo imetinga nusu fainali kwa kuwatwanga
wenyeji Afrika Kusini.
Taarifa zinaeleza, mawakala kadhaa wameanza kumfuatilia kwa karibu baada ya kuwa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri zaidi.
Moja
ya magazeti ya Afrika Kusini yameeleza kuwa Muzamiru ni lulu kutokana
na uwezo aliouinyesha katika mechi zote hadi taifa Stars inafikia nusu
fainali ya michuano ya Cosafa.
Imeelezwa
moja ya timu zilizovutiwa ni Bidvest na Mpumalanga Black Ace lakini
wataalamu wanaofuatilia wachezaji au mawakala wanaweza kuwapeleka
wachezaji katika timu hata za nje ya Afrika Kusini.
Katika michuano hiyo Muzamiru amekuwa injini kuu ya kuendesha kiungo cha Stars na kusababisha mvuto huo.
Kauli
iliyotolewa na Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali kuwa wameachana
na kipa wao Deogratius Munish ‘Dida’ imeonyesha kuwashitua mashabiki
wengi wa klabu hiyo.
Wengi wamekuwa wakihoji sababu ya Dida kuondoka na wengine wakimtaka kuvuta subira.
Lakini wako mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiutaka uongozi wa Yanga kukaa na kumalizana naye vizuri.
Wengine wameshauri kama amepata timu nje aende lakini si hapa Tanzania.
Pondamali alisema Dida aliwaambia hatasaini mkataba na juhudi za kumbembeleza zimekwama.
Hivyo kips African Lyon waliyemsajili, Beno Kakolanya waliyenaye na watasajili kipa mwingine chipukizi.
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inakutana leo saa 7 mchana.
Inakutana kujadili suala la uchaguzi baada ya kamati ya uchaguzi kuahirisha mchakato wa uchaguzi.
Kamati hiyo iliahirisha mchakato wa
uchaguzi baada ya mwenyekiti wake kutofautiana na wajumbe waliokuwa
wakitaka Jamal Malinzi lazima afanyiwe usaili licha ya kuwa mahabusu.
Kama haitoshi, Mwenyekiti wake, Waikili
Revocatus Kuuli alisema wajumbe walitaka kuwakata baadhi ya wagombea
bila sababu za msingi.
Hivyo akaona hakukuwa na suala la weledi na kuamua kusimamisha mchakato wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.
Hivyo, kamati ya utendaji ya TFF italisikiliza hilo na kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kuamsha mchakato huo wa uchaguzi.
Everton
inayodhaminiwa na SportPesa imeonyesha imepania kujiimarisha msimu ujao
baada ya kumwaga pauni million 30 kumnasa beki kisiki Michael Keane kwa
mkataba wa miaka mitano.
Keane
alikuwa kisiki katika kikosi cha Burnley na klabu kadhaa kubwa
zilionekana kumtolea “mimacho” lakini Everton imefanya kweli mapemaa.
Maana
yake, Keane atakuwa kati ya wachezaji watakaotua nchini na kucheza
mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia Alhamisi ya Julai 13 kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.