Wednesday, March 25, 2015

PAN AFRICA FC NA CHANGANYIKENI FC KUSAKA NAFASI YA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA WA MKOA


MSEMAJI WA DRFA, OMAR KATANGA (KUSHOTO)...
Baada ya kumalizika kwa michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam na timu za FFU na Zakhem kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye makundi yao,kesho 20/03/2015 utapigwa mchezo mmoja wa kusaka nafasi ya kuungana na mabingwa hao kushiriki michuano ya ligi ya mikoa.


Mchezo huo wa mtoano utakaopigwa katika uwanja wa Mizinga Kigamboni,utazikutanisha timu za Pan Africa dhidi ya Changanyikeni ambazo zimemaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi yao.

Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam,DRFA,baada ya kumpata mshindi katika mchezo huo, majina ya timu hizo tatu yatapelekwa shirikisho la soka la Tanzania TFF.


Aidha, kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake Kenny Mwaisabula,imewashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja mbalimbali kushuhudua michuano ya ligi mkoa wa Dar es salam tangu ilipoanza kutimua vumbi.

MOURIHNO NDIYE MWENYE MKWANJA MREFU ZAIDI




Kocha Jose  Mourinho wa Chelsea ndiye kocha anaingiza fedha nyingi zaidi duniani.


Mourinho ameweza kuingiza hadi kitita cha pauni milioni 13.2 kwa mwaka huku akifuatiwa na Carlo Ancelotti wa Real Madrid aliyeingiza pauni milioni 11.

10 BORA YA MAKOCHA WENYE UTAJIRI MKUBWA
1. Jose Mourinho £13.2m
2. Carlo Ancelotti £11.4m
3. Pep Guardiola £11.2m
4. Arsene Wenger £8.3m
5. Louis van Gaal £7.3m
6. Fabio Capello £6.6m
7. Andre Villas-Boas £6.2m
8. Sven-Goran Eriksson £5.9m
9. Jurgen Klopp £5.3m
10. David Moyes na Laurent Blanc £5.1m

Source: France Football Rich List

YANGA YAWAUA JKT RUVU TAIFA



MPIRA UMEKWISHA
Yanga wanaonekana kupoteza muda huku JKT angalau wakijitahidi kutafuta angalau bao la pili
DK 90+2
DK 90 Javu anajaribu shuti lake la kwanza baada ya kupokea pasi ya Nizar, hata hivyo mpira unapaa juuu

Dk 88 Nizar anaingia kuchukua nafasi ya Niyonzima aliyeumia

Dk 83 Haruna Shamte anapewa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Ngassa.


Dk 80, Kamuntu anaruka mbele ya Twite na kupiga kichwa lakini kinakuwa hakina madhara. Wakati anainuka anafanya kitendo ambacho si cha kiungwana kwa kumpiga kiwigo.


Dk 75, Magulu anapiga shuti kali lakini Barthez anaonyesha ujuzi kwa kudaka kwa ufundi mkubwa.


Dk 74 Yanga wanamtoa Tellela anaingia Hassan Dilunga, wanamtoa Mrwanda anaingia Hussein Javu na JKT wanamuiniza Najib Maguku kuchukua nafasi ya Alex Abel. 

Dk 70, Niyonzima anapiga shuti safi lakini kipa Haule anaonyesha ujuzi kuokoa.
Dk 64, JKT wanaingia eneo la hatari lakini Makwaya anakuwa na haraka na mpira unaishia kwa Cannavaro anayeondoka hatari.

Dk 60, Ally Bilal anaingia kuchukua nafasi ya Amos Mgisa kwa upande wa JKT
Dk 59, Kamutu analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia Ngassa rafu ya makusudi kabisa.


GOOOOOO Dk 56 Msuva anafunga bao la tatu baada ya Telela kugongeana na Ngassa aliyempa pasi safi mfungaji.


Dk 53 Damas Makwaya analambwa kadi ya njano kwa kujiangusha.Dk 51, kama kawaida, Msuva anapewa pasi nzuri na Mrwanda lakini anashindwa kufunga kwa kupaisha juu.


Kipindi cha pili kinaanza kwa kasi kila timu ikiwa imepania kushinda. Kidogo JKT wanaonekana kuchangamka.
MAPUMZIKO:

Dk 45, Samuel Kamuntu anaifungia JKT bao safi kwa shuti kali baada ya mabeki wa Yanga kuzubaa.

Dk 43 Yanga wanaonekana kumiliki mpira zaidi huku JKT wakitumia muda mwingi kukaba.


GOOOOOOOO Dk 41, Mrwanda anaifungia Yanga bao la pili baada ya kuwatoka mabeki wawili, akatoa pasi kwa Msuva ambaye anapiga krosi safi kwa mfungaji.

Dk 39, Mbaga naye anapata nafasi baada ya kuingia kwenye box, lakini anashindwa kutulia na kupiga shuti hovyooo

Dk 35, Msuva anapata krosi nzuri ya Juma Abdul, akiwa yeye na kipa hatua nne kutola langoni, anapiga kichwa lakini anashindwa kulenga.


GOOOOOOOO Dk 33 Msuva anafunga penalti hiyo vizuri kabisa na kumfikia mshambuliaji Didier Kavumbagu....


PENAAAAAT Dk 33 beki Makwaya anashika eneo la hatari na mwamuzi anaamuru penati ipigwe
Dk 29&32, JKT wanaonekana kubaki nyuma zaidi na hakuna mashambulizi yoyote wanayofanya huku wakibakiza mabeki wanne nyuma na kushambulia kwa kushitukiza lakini hawana shambulizi lolote kali.


Dk 28, Ngassa naye anapewa kupiga mpira wa faulo, vilevile naye anapaisha juuu
Dk 25, Joshua anapiga mkwaju wa faulo lakini anapaisha juuuu..
Dk 22, Ngassa anapoteza nafasi ya wazi akiwa yeye na kipa baada ya krosi nzuri ya Juma Abdul aliyekuwa amewatoka mabeki wa JKT.


Dk 20, Ngassa anawatoka mabeki wa JKT na kupiga shuti ambako linapanguliwa na kipa Benjamin Haule na mabeki wake wanaondosha hatari.

DAKIKA YA 1 hadi 15 Yanga ndiyo wanaonekana kujipanga zaidi kwa kufanya mashambulizi mengi.


Hata hivyo inaonekana wachezaji wa Yanga pia hawako makini sana katika umaliziaji. Bado mchezo pia haujachangamka kwa kiasi kikubw

msuva ampiku kavumbagu kwa mabao

Kiungo mwenye kasi wa Yanga, Simon Happygod Msuva amefikisha mabao 11 baada ya kufunga mawili leo.

Msuva amefunga bao lake la 11 katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Msuva alianza kufunga bao la katika dakika 34 kwa mkwaju wa penalti na kufanikiwa kumfikia mshambuliaji Didier Kavumbagu wa Azam FC. Lakini baadaye akafunga bao la tatu kwa Yanga leo na la pili kwake hivyo kufikisha mabao 11.


Kavumbagu raia wa Burundi amekuwa akiongoza kwa ufungaji tokea kuanza kwa ligi hiyo.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif