Friday, August 18, 2017

HUU UDHAMINI WA KIBOKO, UIANYE NDANDA IANZE KUISHI MAISHA MAPYA



MSIMU uliopita, kikosi cha Ndanda FC kilinusurika kuteremka daraja hadi la kwanza “kimkandamkanda” kwa kuwa mambo yalikuwa mabaya kupita kiasi.

Licha ya kuwa kati ya timu zinazoonekana zinakwenda kuteremka daraja. Ndanda FC ndiyo ilikuwa timu ambayo imepoteza mwelekeo zaidi baada ya uongozi wake kuonekana umepotea njia.

Kibaya zaidi, wachezaji wake wengi nao walionekana wamepotea na wamekata tamaa na hata kufikia kulalamika kwenye vyombo vya habari.

Baadhi ya mambo waliyolalamika ni kukosa hata fedha kwa ajili ya mlo. Yaani walikuwa kambini na walikuwa wakishinda njaa, kitu ambacho ni kibaya zaidi cha mwisho unapozungumzia kundi la wanadamu.

Mnaweza kukosa jambo jingine lakini si chakula ambayo ni huduma namba moja kwa mwanadamu. Lakini wachezaji hao walisema nafuu yao ilikuwa ni mlo mmoja kwa siku, jambo ambalo si zuri hata kulisikia na sikuwahi kusikia kiongozi wa Ndanda FC akilikanusha.

 Waliokuwa wakilalamika ni kati ya wachezaji wakongwe kabisa wa Ndanda FC na hata watu wa benchi la ufundi. Hili halikuwa jambo zuri lakini hongera kwao kwa kuwa walijitutumua na mwisho Ndanda FC ikabaki Ligi Kuu Bara.

Baada ya hapo, nilitegemea kuona wanajipanga. Ingawa jambo hilo halikufanyika mapema sana kwa kuwa inaonyesha hata usajili wa Ndanda FC haukuwa ule unaoonyesha kuna mabadiliko makubwa.

Huenda uongozi haukuwa na fedha na mipango haikuwa bora kuhakikisha fedha nyingi zinapatikana. Lakini baada ya dirisha la usajili kufungwa, nimeona kuna Kampuni Motsun Group Ltd kupitia ya bidhaa yake ya mabati ya Kiboko imejitokeza kuidhamini Ndanda FC.

Ndanda FC wamepata udhamini wa mwaka mmoja kuitangaza Kiboko. Hawakusema kiasi gani lakini tayari wameongeza kitu mfukoni mwao ambacho kitawasaidia kuwa tofauti na awali.

Lakini lazima ukumbuke kuwa Ndanda FC wanaingiza fedha kupitia wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom pia Azam TV ambazo zinaweza zisiwe nyingi sana lakini zinasaidia gharama kadhaa za uendeshaji tofauti na zamani.

Msimu uliopita pia walipokea fedha kutoka Vodacom na Azam TV lakini wakashindwa kusimama na kufanya vizuri. Ujio wa Kiboko ni jambo jingine bora wanalopaswa kulitumia kama chachu ya mabadiliko.

Ninaamini Kiboko wangeweza kutodhamini katika soka na kwenda kwingine kujitangaza. Uamuzi wao kuingia kwenye soka lazima wapate faida na mafanikio yao na ikiwezekana wanaongeza mkataba ni kuona Ndanda FC inafanya vizuri.

Ndanda FC wasifurahie fedha tu wanazopata, badala yake wanapaswa kujua kwamba wadhamini wao pia kuna jambo wanategemea kutoka kwao na wakifurahia zaidi basi wataweza kuendelea na udhamini na ikiwezekana kuongeza zaidi, hili ninaamini linaweza kutokea.

Lakini anayeweza kulifanya litokee, ni Ndanda wenyewe ukianza na viongozi na wachezaji pia. Wanaposaidia lazima wajue wana deni la kumtangaza mdhamini wakiwa na mafanikio na ikiwezekana suala la nidhamu linapaswa kuwa juu zaidi ukilinganisha na msimu uliopita.

Kesho kama Ndanda FC itateremka daraja, maana yake watakuwa pia wamemshusha mdhamini wao kwa maana ya kwamba hatakuwa na nafasi ya kuongeza mkataba tena. Lakini wakifanya vema na ikiwezekana kufikia angalau ule uwezo waliouonyesha Mbao FC ya Mwanza msimu uliopita, huenda hata wadhamini wenye donge nono wanaweza kujitokeza zaidi.

Ndanda FC mna deni kubwa la kuonyesha tofauti kwa kuwa mwanadamu bora ni yule anayejifunza kupitia makosa yake. Kama msimu unaoanza wiki chache zijazo utaendelea kuwa wa shida kwenu, basi lawama zibaki kwenu na mtaonyesha ni watu wa kubahatisha mambo.


Fanyeni vizuri ili muwe sehemu ya kuwashawishi wadhamini wengine kwamba hata timu ndogo zinaweza kudhaminiwa na kuwatangaza vizuri wadhamini.

Moto wa Bundesliga kuanza kuwaka leo, Rb Leizpg au Borussia Dortmund nani ataweza kumsimamisha Bayern Munich?


Xabi Alonso na Phillip Lahm walikuwa moja ya nguzo za mafanikio katika klabu ya Bayern Munich lakini msimu huu Bayern wanaingia bila wazoefu hao wawili ambao wametundika daluga.
Lakini bado Bayern wana matumaini kuchukua ubingwa kwa mara ya 6 mfululizo huku maingizo mapya haswa la James Rodriguez na Corentin Tolliso yakiwapa matumaini ya kutetea ubingwa wao na leo watakuwa dimbani kufungua ligi dhidi ya Bayern Leverkusen.
Msimu huu Borussia Dortmund wanaweza kuwa wapinzani wakubwa wa Bayern tofauti na ule uliopita ambapo klabu ya Rb Leizpg ndio walionekana kuitishia Bayern na kumaliza katika nafasi ya pili.
Lakini Dortmund wanaweza kuwa vizuri kama watafanikiwa kuwabakisha Osmane Dembele na Pierre Aubemayang ambao wako kwenye tishio la kuihama klabu hiyo katika dirisha hili la usajili na kocha wao mpya Peter Bosz anategemewa kuwa mhimili mpya BvB.
Rb Leizpg wamefanikiwa sana katika dirisha hili la usajili kubakisha nyota wao wakubwa Emil Forsberg na Naby Keita aliyekuwa akiwinda sana na Liverpool na hii inatoa tumaini kwa mashabiki wao.
Lakini Rb Leizpg watakuwa na Champions League hii inaweza kuwafanya wachoke na kiwatokee kilichowatokea klabu ya Leicester City msimu uliopita ambapo wingi wa michuano uliwafanya wapwaye sana.
Maingizo mapya ndani ya Rb Leizpg akiwemo mshambuliaji toka PSG Kevin Augustin na Bruma aliyesajiliwa toka Galatasaray inaweza kwa kiasi fulani kuipa nguvu Leizpg katika msimu huu wa ligi.
Bayern Leverkusen wamepoteza wachezaji wawili muhimu Javier Hernandez Chicharito aliyekwenda West Ham na Calhanoglu aliyetimkia Ac Milan ni pigo kwao lakini kocha moya Heiko Herlich anatarajiwa kutoa mbinu mpya kuibeba Leverkusen.
Hoffeinman bado hawana uhakika wa kufudhu Champions League na wasipofudhu watabaki Europa League msimu ujao wakiungana na Hertha Berlin pamoja na Cologne na hii itazifanya timu hizo kuwa na michuano ya ziada inayoweza kuwapa mzigo wa ziada katika ligi.
Stuttgart na Hannover wamepanda ligi msimu huu  lakini Stuttgart sio wageni sana kwenye ligi kwani mwaka 2015/2016 ndio walishuka daraja na mwaka huu wamerudi, kimbembe kipo kwa Hannover ambao tayari wameanza kutabiriwa kushuka daraja.


MADRID YATAWALA TUZO ZA FIFA, YAINGIZA FAINALI WACHEZAJI SABA

Na Ram Mbegeze



Real Madrid imeendelea kutawala katika duniani baada ya kuingiza wachezaji saba kati ya 24 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Kutoka Real Madrid, wachezaji waliongia kwenye tuzo bora ya mchezaji bora Fifa ni 
Cristiano Ronaldo, Dani Carvajal, Toni Kroos, Luka Modric, Keylor Navas na Sergio Ramos.


Hiyo inaifanya Madrid kuwa timu iliyoingiza watu wengi zaidi katika listi hiyo.


EVERTON YASHINDA 2-0 NA KUJIWEKA VIZURI KUWANIA KUFIKIA MAKUNDI EUROPA LEAGUE



Everton imeitwanga Hajduk Spilit kwa mabao 2-0 na kujiweka katika hatua nzuri ya kufuzu katika hatua ya makundi ya Europa League.

Mabao ya Everton yamefungwa na Michael Keane na Idrissa Gueye katika mechi hiyo ambayo kipindi cha kwanza ilikabiliwa na tafrani kutoka kwa mashabiki wa Hadjuk hadi kusababisha mpira kusimama.


Kipindi cha pili kilikwenda vizuri na hakikuwa na bao hata moja kwa kuwa Everton hawakuweza kuongeza na wageni nao hawakupata bao. Mechi ya marudiano ni Alhamisi ijayo, Everton inayodhaminiwa na SportPesa, itakuwa ugenini.


VIKOSI:
EVERTON (4-2-3-1): Pickford 6.5; Martina 6.5, Keane 7, Williams 6, Baines 6.5; Schneiderlin 6.5 (Davies 46, 6), Gueye 6.5; Mirallas 6.5 (Besic 76), Klaassen 6 (Calvert-Lewin 62, 6), Lookman 7; Rooney 7 
SUBS NOT USED: Stekelenburg, Jagielka, Lennon, Holgate
GOALS: Keane (30), Gueye (45) 
BOOKED: Schneiderlin


HAJDUK SPLIT (4-2-3-1): Stipica 6; Juranovic 6, Nizic 6, Carbonieri 6, Memolla 5.5; Gentsoglou 6 (Toma Basic 85), Radosevic 6, Barry 6; Vlasic 6.5, Ohandza 6 (Said 66, 6), Kozulj 6 (Erceg 66, 6) 

SUBS NOT USED: Letica, Bosancic, Sehic, Tudor
BOOKED: Memolla 
REFEREE: Ivan Kruzliak (Slovakia)
























-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif