Mtandao wa www.sokkaa.com umetoa orodha ya wanasoka 10 wenye mvuto aidi duniani ‘Most Handsome Footballers in the World’.
Hii hapa ni orodha kamili;
10. Mats Hummels-Borussi Drtmund
Mats Hummels ni mchezaji wa kijerumani anaekipiga kwenye klabu ya Dortimnd ambaye kwa sasa ni nahodha wa kikosi hicho. Ana mwonekano ambao wanawake wanaoshabikia mchezo wa mpira wa miguu wamekuwa wamekuwa na maswali mengi juu ya mwanandinga huyo.
9. Gerrard Piqué–FC Barcelona
Macho yake ya blue na style ya nywele zake, Gerrard Pique anakamata nafasi ya tisa kwenye orodha ya wachezaji wa mpira wenye mvuto zaidi.
8. Cesc Fabregas-Chelsea
Ni miongoni mwa viungo wachezeshaji kwenye ligi ya England (EPL) Mbali na uwezo wake wa kupiga pasi, Fabregas pia ni mwanaume mwenye mvuto na anashika namba nane kwenye orodha hii.
7. Mario Gotze-Bayern Munich
Ni kiungo wa klabu ya Bayern Munich ambaye alipata heshima kubwa nchini Ujerumani kwenye historia ya soka baada ya kufunga goli la ushindi kwa Ujerumani mwaka 2014 dhidi ya Argentina.
6. Fernando Torres-Atletico Madrid
Fernando Tores a.k.a ‘El Nino’ amewatesa watoto wengi wa kike wanashabikia mpira kutokana na mvuto wa sura yake, stayle ya nywele na umbo la mwili wake ambalo limebalansiwa vizuri.
5. Van Persie-Fenerbahce S.K.
Robin van Persie siku za hivi karibuni amepachikwa jina la utani ‘The Flying Dutchman’ kutokana na goli alilofunga kwa kichwa wakati Uholanzi inacheza dhidi ya Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2014.
4. Iker Casillas–Real Madrid
Iker Casillas bado ni miongoni mwa magolikipa bora ulimwenguni na ni miongoni mwa wacheza mpira wenye mvuto zaidi duniani.
3. David Villa–New York City FC
Mbali na kufunga magoli mazuri, Villa amengia kwenye orodha ya wachezaji wenye mvuto pamoja na style nzuri ya nwele zake.
2. Kaka–Orlando City FC
Ricardo Kaka anashika nafasi ya pili kwenye orodha hii. Muonekano wake wa kuvutia pamoja na style ya nywele, vilifungua milango ya yeye kuingia kwenye tasnia ya fashion. kampuni nyingi za fashion zimekuwa zikimsaka mkali huyo kwa ajili ya kufanya nae matangazo.
No comments:
Post a Comment