Kilichosubiriwa kimetimia na inawezekana kikawa. Kilichotegemewa
pengine sicho kilichotimia, na kilifikiriwa inawezekana sicho
kilichotokea. Wengi walisubiri kuona mchezo kati ya Oklahoma City
Thunders dhidi ya Golden State Warriors hasa uhasama kati ya Kevin
Durant dhidi ya Russell Westbrook.
Kevin Durant
alihama kutoka klabu ya OKC na kuelekea Oakland katika klabu ya
Warriors na ukawa ni uhamisho ambao ulizua maswali mengi ambayo wengi
walihisi amekuwa mchezaji asiyejiamini na ambaye kama angehama
hakutakiwa kujiunga na klabu yenye nyota wengine bali angeeenda
kutengeneza ufalme wake mahali kwingine.
Alikwua ni Durant ambaye alikuwa na usiku mzuri zaidi kwani
aliiongoza Warriors kupata ushindi mnono. Durant alipata mitupo 7 ya
pointi 3 ambayo ndio mingi zaidi kuwahi kuipata katika mchezo mmoja na
kumaliza mchezo na pointi 39. Warriors wakamaliza mchezo kwa kuichapa
OKC na
Russell Westbrook kwa pointi 122-96.
Westbrook alidhibitiwa na kufunga pointi 20 tu baada ya kuja katika
mchezo huu akiwa mfungaji bora zaidi akiwa na wastani wa pointi 37.8 kwa
mchezo.
Stephen Curry aliongeza pointi 21 points na assist 7, huku
Klay Thompson ambaye amekuwa na msimu mbaya hasa kwenye ufungaji wake wa pointi 3 akifunga pointi 18, na kupata mitupo 4 ya pointi 3.
Victor Oladipo aliiongoza Oklahoma City akimaliza na pointi 21.
TAKWIMU
Kevin Durant amefunga pointi 20 au zaidi katika michezo 69 mfululizo akiungana na
Michael Jordan ambaye alifanya hivyo kuanzia Nov. 24, 1990, mpaka April 19, 1991.
Pointi 39 za Kevin Durant zimekuwa pointi nyingi zaidi kwa mchezaji kuifunga timu yake ya zamani akilinagana na Danny Ainge na
Stephon Marbury ambao waliwahi kufanya hivyo.