BENFICA DE LUANDA |
Tayari Yanga ina ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya
FC Platinum ya Zimbabwe. Lakini kuna mechi ya pili itakayopigwa kati ya Aprili
3 hadi 5 ndiyo itatoa majibu.
Iwapo Yanga itafuzu, basi itakuwa na kibarua
kigumu zaidi katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho kwa kuwa inatarajia
kukutana na timu kutoka Tunisia au Angola.
ESS.. |
Etoile du Sahel (ESS) ya Tunisia au Benfica ya Angola,
moja itakayoshinda. Basi ndiyo itakutana na Yanga.
Tayari Etoile wameshinda mechi yao ya kwanza
nyumbani kwa bao 1-0 lakini lazima wasubiri pia mechi ya ugenini jijini Luanda.
Iwapo Yanga itavuka, basi inatarajiwa kukutana
na moja ya timu hizo katika mechi ya kwanza itakayopigwa kati ya Aprili 17 hadi
19 na marudiano Mei Mosi na Mei 3.
No comments:
Post a Comment