Katika mchezo vs Atletico Madrid jumamosi hii, Real Madrid na
Zinedine Zidane kwa mara nyingine watakuwa wakitegemea silaha zao za
ushambuliaji kupata ushindi muhimu katika Derby na kujiongezea wa pointi
katika uongozi wa La Liga.
Hautokuwa mtihani mwepesi katika dimba la Estadio Vicente Calderon,
Madrid hawajapata ushindi katika Derby sita zilizopita za ligi,
wakifungwa mechi 4 na sare 2.
Kuondoa mkosi wa Bale
Tangu alipowasili kutokea Tottenham Hotspur miaka 3 iliyopita, Gareth
Bale amepata mafanikio makubwa: 2 Champions League titles, a Club World
Cup, 2 UEFA Super Cups na Copa Del Rey.
Katika kufanikisha hayo amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika ulimwengu wa soka.
Lakini pamoja na mafanikio mpaka sasa ameshindwa kufunga goli au
kupata ushindi dhidi ya Rojiblancos – pamoja na Valencia pia, katika La
Liga.
Mpaka sasa ameshacheza mechi 5, sare 2 (zote katika uwanja Calderon)
na vipigo vitatu – viwili kati ya hivyo katika uwanja wa Santiago
Bernabeu – kipigo kimoja kikiwa kile cha 4-0 msimu wa 2014/15.
Msimu huu amekuwa na kiwango kizuri, katika mechi 2 zilizopita
amefunga magoli 3, na huenda msimu huu akavunja rekodi yake binafsi ya
kufunga magoli 19 kwenye La Liga. .
Benzema
Mara ya mwisho Real Madrid wamefunga goli dhidi ya Atletico Madrid katika ligi ilikuwa – October 2015 katika uwanja Calderon.
Siku hiyo, ilikuwa Karim Benzema ambaye alifungua ukurasa wa magoli
lakini hilo lisikuchanganye – rekodi yake vs Atletico sio nzuri kabisa.
Mshambuliaji huyu wa kifaransa amefunga magoli 3 tu katika mechi 13 vs Vijana wa Simeone.
Katika timu zote 33 alizokutana nazo katika La Liga, Benzema amepiga
idadi ndogo zaidi ya mashuti vs Atletico, pamoja na Alaves ambao
amekutana nao mara tu.
Ronaldo
Cristiano Ronaldo ameshafunga magoli 8 vs Atletico katika miaka yake 7
aliyokaa Santiago Bernabeu mpaka sasa. Rekodi nzuri ukizingatia nafasi
anayocheza.
Kwa CR7, mchezo wa jumamosi sio tu wa kuongeza namba ya magoli
aliyofunga dhidi ya majirani zake, bali pia ni wakati muafaka wa
kurudisha makali yake.
Msimu huu amefunga magoli 7 katika mashindano yote msimu huu, msimu uliopita alifunga idadi kama hii kwenye mechi 3 za kwanza.
Lakini Ronaldo, 31, ameshathibitisha ni mmoja ya walio bora na
jumamosi hii atakuwa anatafuta goli lake la 8 vs mshindi wa tuzo ya
Zamora wa msimu uliopita na golikipa bora kwenye ligi Jan Oblak.
Morata – mfungaji bora wa kikosi cha Real Madrid msimu huu,
hatakuweko katika kikosi cha Zidane baada ya kugundulika kupata majeruhi
kwenye mguu.