Wednesday, November 16, 2016

Mambo 6 yaliyokatazwa na Pep ndani ya Manchester City.

screen-shot-2016-11-16-at-5-48-32-pm
Kutokana na story ya Samir NAsri kwamba Pep Gurdiaola amewapa ushari wachezaji wake kwamba wajihusishe na kukutana na wapenzi wao kabla ya usiku wa manane, imeibua hamu ya kujua maagizo mengine ya manager Pep ndani ya Etihad. Hivi hapa ni vitu sita ambavyo Pep ametoa maelekezo yake jinsi ya kufanyika ndani ya Etihad.
Sex
Pep huwa anasisitiza kwamba kitendo hiki kifanyike kabla ya usiku wa manane ili mchezaji apate muda mwingi wa kulala na kupumzika. Bila shaka hili hana uwezo wa ku-control zaidi ya kuwaamini wachezaji wake kwamba wanafuata anachokiagiza.
Pizza
Kuagizwa kwa Pizza kabla ya mechi ilikua ni kawaida kabla ya Pep hajaichukua timu. Lakini baada ya kuichukua Pizza haziruhusiwi kuja kabla ya mechi. Sasa hivi inameripitwa kwamba Pizzza huwa zinaletwa baada ya mechi ikiwa ni sehemu ya kurudisha nguvu baada ya mechi.
Breakfast
Ishu ya kuja na Sausage zako na mayai kwenye gari mazoezini kwa ajili ya chai mambo hayo hayapo ndani ya Etihad. Pep anatoa order kwa kila mtu kunywa chai au kula mezani pamoja kama familia zinavyofanyaga.
Juice za Matunda
Pep hataki wachezaji wake wanywe juisi za matunfa ambazo zina kiasi kikubwa cha sukari ambayo ni mbaya kwa afya yao. Pep hiwa ana sisitiza kwamba wachezaji wake wale matunda badala ya kunywa juisi iliyotengenezwa.
WiFi
Lengo kubwa anataka waongee wao kwa wao ili kuongeza kuzoeana nje ya uwanja. Kwenye eneo la kufanyia mazoezi simu zinakatazwa. Lakini Pep ameenda mbali zaidi kwa kuzuia WiFi kabisa ili kusiwe na connection yoyote.
Mitindo ya Nywere
Inasemekana kwamba Pep anakataza hadi wachezaji kujihusisha na style za nywere. Lengo lake anataka mchezaji a-focus kwenye mchezo zaidi ya kitu kingine chochote. Sasa angekua na mchezaji kama Pogba ingekuaje.

Azam U-20 kuanza na Mbao Ligi ya Vijana kesho




TIMU ya vijana ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC ‘Azam U-20’, kesho saa 8.30 mchana inatarajia kuanza kutupa karata ya kwanza kwenye Ligi ya Taifa ya Vijana kwa kukipiga dhidi ya Mbao katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera.
Azam U-20 iliyojiandaa vema kuelekea michuano hiyo, imepangwa kwenye kituo cha Bukoba chenye timu nane kinachounda Kundi A, kikiwa na timu nyingine za Kagera Sugar, Toto African, African Lyon, Mwadui, Stand United na Yanga.
Akizungumza  ram mbegeze blog  Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Idd Cheche, alisema kuwa wamejipanga vilivyo kuanza vema michuano hiyo kwa kupata ushindi kesho.
“Kikosi changu kipo kamili kwa ajili ya michuano hiyo, kimefanya maandalizi mazuri na malengo yetu makubwa ni kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kituo hiki na hatimaye kuibuka mabingwa,” alisema.
Cheche aliwatoa hofu mashabiki wa Azam FC kwa kuwaaambia kuwa wakae mkao wa kula kutokana na ubora wa timu yao na ipo vizuri kwa ajili ya kushindana na hatimaye kutwaa ubingwa.
Mabingwa hao wa kihistoria wa michuano ya awali ya vijana ya Uhai Cup, wanatarajia kung’arishwa vilivyo na baadhi ya mastaa wake wakiwemo mshambuliaji Shaaban Idd na kiungo Masoud Abdallah, ambao pia wamepandishwa kucheza kwenye timu ya wakubwa ya kikosi hicho.
Tayari mchezo wa ufunguzi wa kituo hicho umefanyika jana, ambapo ilishuhudiwa Kagera Sugar ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga huku leo Jumatano ukitarajiwa kupigwa mtanange mwingine utakaohusisha watani wa jiji la Shinyanga, Stand na Mwadui.

MPIRA NI PESA BWANA. ONA HII FC BARCELONA WAMEWEKA REKODI YA DUNIA.


screen-shot-2016-11-16-at-6-40-28-pm
Mpira pesa dunia nzima na watu wanaendelea kufanya biashara kama kawaida. Barcelona wamesaini mkataba mdhamini mpya wa jezi ambayo ni kampuni ya kuuza bidhaa online inaitwa “Rakuten”.
Uhusiano wa udhamini wa jezi kati ya Barcelona na Qatar Airways unaisha mwishoni mwa summer. Hivyo basi wame sign mkataba mpya ambao una thamani mara mbili zaidi ya uliopita.
Mkataba huo kwa mwaka utawapatia pound milioni 50 ndani ya miaka mitano ijayo. Mkata huu wa mdhamini wa jezi umeweka rekodi ya dunia. Qatar airways watabaki kuwa official airline partner.
screen-shot-2016-11-16-at-6-38-28-pm
Kampuni hiyo ya Japan ina lengo la kutanua market yao barani Asia ambapo kuna ushabiki mkubwa wa
club ya Barcelona. Ndani ya miaka 5 ya uhusiano wa kibiashara kati yao utasaidia kukuza biashara yao.
screen-shot-2016-11-16-at-6-38-35-pm

TIMU YA KITAYOSCE YA MOSHI YASHINDWA KUTAMBA

Timu ya Kitayosce ya mjini Moshi inayoshiriki ligi daraja la pili imeshindwa kutamba katika uwaja wa nyumbani baada ya kutoka suluhu ya kutofungana na timu ya PEPS ya Arusha ktk mchezo wa ligi daraja la pili uliochezwa ktk uwanja wa chuo cha ushirika mjini moshi mchezo huo umemalizika kwa suluhu ya o kwa o


baada ya mmchezo kumalizika kocha wa timu ya peps Davidi Nyambele amesema ,, anafurahia matokeo hayo kwakuwa alikuwa ancheza ugenini huku akiseama anauhakika atashinda mechi ya nyumbani,,.Tazama baadhi ya matukio ya mchezo huo

naye msemsji wa timu ya kitayosa ELISAFI WILSON MSHIGATI amesema wanajipanga kwa mchezo ujao na watarekebisha makosa waliyoyafanya leo

 mashabiki wa timu ya kitayosce wakishuhudia timu yao ikishindwa kuifunga peps fc nyumbai



-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif