Thursday, May 7, 2015

NOIJ AITA 28 KUELEKEA COSAFA


Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakaoingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam, kujiandaa na michuano ya kombe la COSAFA na kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN mwezi Juni mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF amesema, wachezaji 28 aliowaita, amewaona kwa macho yake wakicheza, na katika wachezaji aliowaita amechanganya wanaochipukia (damu changa) na wenye uzoefu wa michuano ya kimataifa.
Nooij amesema katika orodha hiyo ya wachezaji 28 watakaoripoti kambini jumatatu mchana, watapimwa afya zao na madakatari wa timu ya Taifa, na kisha watakaokuwa fit atachagua wachezaji 20 watakaokwenda kwenye michuano ya COSAFA nchini Afrika kusini.
Aidha Nooij ameongeza wachezaji 8 watakaobakia nchini wanapaswa kuwa tayari wakati wowote wanaweza jumuishwa katika kikosi kutokana na Taifa Stars kukabiliwa na michuano mbalimbali ambayo pia inahitaji kuwa na wigo mpana wa wachezaji.
Wachezaji walioitwa na kocha Nooij ni magolikipa: Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ali (Azam), walinzi: Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Haji Mwinyi (KMKM).
Wengine ni viungo: Amri Kiemba, Salum Abubakar, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhira).
Washambuliaji ni Ibrahim Ajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John Bocco, Kelvin Friday (Azam) na Juma Luizio (Zeco United).
Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumatano, Mei 13 saa 1 jioni kwa shirika la ndege la Fastjet kuelekea nchini Afrika Kusini katika mji wa Rusterburg - North West Province ambapo ndipo michuano ya COSAFA CUP itafanyika kuanzia Mei 17 mpaka Mei 31 mwaka huu.
Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars iliyopo katika kundi B katika michuano ya COSAFA, itacheza dhidi ya Swaziland Mei 18, Mei 20 (Madagascar Vs Tanzania) na Mei 22 ( Tanzania vs Lesotho), mshindi wa kundi B atacheza robo fainali dhidi ya timu ya Taifa kutoka Ghana.
Mara baada ya kumalizika kwa michuano hiyo, Taifa Stars itarejea nchini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017, dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 13 nchini Misri, kisha kurejea nchini kucheza na Uganda Juni 21 kuwania kufuzu kwa fainali za wachezaji wa ndani CHAN.
Mart Nooj amesema ataitumia michuano ya COSAFA kama sehemu ya maandalizi ya michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN.

CHEKI ALICHOSEMA PEP GUADIOLA BAADA YA MCHEZO WA JANA


Uwezo wa Lionel Messi ndio uliamua matokeo ya mchezo wa jana kati ya Barcelona and Bayern Munich, mchezo ambao ilishuhudiwa Bayern ambao ni mabingwa wa Ujerumani wakipokea kipigo cha mabao 3-0 katika uwanja wa Camp Nou. Hayo ni maneno ya Pep Guardiola ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona.
Messi alifunga magoli mawili katika mchezo huo huku akitoa pasi ya bao la mwisho lililofungwa na Mbrazil Neymar Santos Jr.
"Bayern wamefanya vizuri kwa kipindi kirefu sana," alisema Guardiola ambaye aliifunika Barca kwa umiliki wa mpira, kitu ambacho ni adimu sana kutokea kwa Barca, wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kuwa mara ya mwisho hali hiyo kutokea kwa Barca ni mwaka 2006, alisema. 
"Lakini Messi alionesha ubora wake. Barca sio sana kivile, ila yeye si wa kawaida, Barca ni timu imara ambayo ina nyota wengine wazuri kama vile Luis Suarez na Neymar.
"Barca ni wazuri mno, wana uwezo wa kutengeneza nafasi popote watakapo. Ni vipaji vya wachezaji wao ndio vilitupoteza, kucheza hapa Camp Nou ni vigumu sana.
"Lakini hata hivyo nadhani tuliuweka mpira katika himaya yetu, mapaka pale walipopata goli lao la kwanza. Ni baada ya pale ndipo tulipoanza kupoteana, lakini sitalaumu mchezaji yeyote yule, timu imepitia vipindi vigumu sana msimu huu."

MWADUI FC YAVUNJA UKIMYA JUU YA KOCHA WAO

Uongozi wa timu ya Mwadui ya mkoani Shinyanga umefunguka juu ya taarifa za kuachana na kocha wake.
Taarifa mbalimbali zilidai kuwa kuna uwezekano wa wageni hao kwenye ligi kuu msimu ujao kuachana na Jamhuri kiwelu na kusaka kocha mwingine.
Lakini Mpenja blog ilibisha hodi kwenye mgodi huo wa almasi na kuzungumza na katibu kuu wa timu hiyo Ramadhani Kilao ili kujua ukweli na undani wa taarifa hiyo, ambapo katibu huyo alikanusha taarifa hizo.
"Hizi taarifa hata sijui zinatokea wapi,kwetu hatuna hizo taarifa lakini nashangaa kuona zinazungumzwa kila siku,Julio ni kocha wetu labda yeye atuache ".Alisema Kilao.
Alipoulizwa kuhusiana na taarifa za kuwepo mpango wa kuleta kocha wa kigeni,katibu huyo amesema hawajalifikiria hilo lakini alidai kwamba uwezo wanao wa kumchukua kocha yeyote awe wa ndani au nje ya nchi.
"Uwezo wa kuleta kocha tunao tena hata tukitaka watatu,lakini kwasasa hilo hatujalifikiri"Alisema.
Kocha mkuu wa Mwadui Jamhuri kiwelu alifanikiwa kuipandisha daraja timu hiyo na baada ya kufanya hivyo aliekea kukinoa kikosi kama kocha msaidizi wa muda lakini baada ya kuondoka kwa kocha James Nandwa kikosini hapo Julio sasa ndiye kocha mkuu wa wagasi wa kaya Coastal Union.

MAZANDA BADO HALI SI NZURI

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
NYOTA wa kikosi cha Mbeya City, Steven Mazanda na Yusuph Abdalah Sisalo watalazimika kusubiri mpaka msimu ujao ili kurejea uwanjani kukitumikia tena kikosi chao kutokana na majereha makubwa waliyokuta nayo mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Daktari mkuu wa City, Dk Joshua Kaseko, amekaririwa katika mtandao rasmi wa klabu hiyo akieleza kuwa nyota hao wawili wameshindwa kupona majeraha yao katika muda uliotarajiwa hivyo waatalazimika kusubiri msimu mpya ili kurejea uwanjani.
“Awali kulikuwa na dalili njema kuwa huenda wangepona haraka na kurejea kumalizia michezo ya mwisho, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu, lakini imeshindikana  na kama unavyofahamu si jambo nzuri kumlazimisha mchezaji kucheza wakati vipimo vinaonesha bado hayuko sawa. Kwa sasa hakuna namna nyingine zaidi ya wao kuendelea na matibabu ili wapone kabaisa tayari kwa msimu ujao”, amesema Dk Kaseko.
Mazanda aliumia goti la mguu wa kulia akiwa mazoezini siku moja kabla City haijashuka dimbani Sokoine kuivaa Stand United ya Shinyanga kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliomalika kwa City kushinda bao 2-0 huku Sisalo akiumia goti la mguu wa kulia dk ya 15 ya kipindi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Ndanda Fc ulichezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Ndanda FC.

ALLIANCE YAAGWA


Na Kassim Mtolea,Mwanza
Timu ya soka ya Alliance ya Mkoani Mwanza imeagwa rasmi na Mkurugenzi wa timu hiyo James Bwire pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoani hapa(MZFA) Jackson Songora.
Akizungumza na Mpenja blog,Mkurugenzi wa timu ya Alliance James Bwire amesema kuwa maandalizi yao yapo vyema na timu itasafiri ijumaa kuelekea Manyara
Bwire alisema pia timu yao itaondoka na wachezaji 30,makocha watatu,viongozi wawili kutoka chama cha soka mkoani Mwanza,wapishi
wawili Kwa upande wa Mwenyekiti wa MZFA,Jackson songora amesema kuwa anaiomba
timu ya Alliance ifanye vyema ili ipande kuelekea ligi Daraja la pili.
Alliance FC imefanikiwa kusajili wachezaji watano kutoka timu ya Nyange na Nyamagana FC ambao ni George Philemon,Juma Mussa,Baraka
Abeid,Salim Juma na Amir Mohamed Kwa upande wake kocha wa Alliance,Kessy Mziray amesema maandalizi yao
yako vyema kwa kuwa wameweza kucheza mech tatu za kirafiki na kushinda zote.
Mechi ya Kwanza Alliance fc itacheza siku ya jumapili dhidi ya timu ya Bariadi FC kutoka Shinyanga
Alliance fc itaondoka mwanza siku ya ijumaa asubuhi kuelekea Manyara.

IVO MAPUNDA AOMBA MKATABA MPYA SIMBA


Na Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Mkataba wa Ivo na Simba umebakisha siku 13 kumalizika.'
KIPA mkongwe wa Simba, Ivo Mapunda, amesema ana matumaini ya kuendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao licha ya kutokuwapo kwa dalili zozote za mazungumzo na viongozi wa timu hiyo.
Ivo mwenye mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba tangu atue kwenye mzunguko wa pili msimu uliopita akitokea Gor Mahia ya Kenya, ameuambia mtandao huu kuwa angependa kuendelea kuichezea timu hiyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya, lakini ameuachia uongozi na benchi la ufundi uamue.
“Ninaamini nimefanya kazi nzuri katika msimu mmoja na nusu niliofanya kazi hapa Simba, lakini kama mchezaji siwezi kulazimisha nimewaachia viongozi na benchi la ufundi kama wataona ninafaa, watanifuata tuzungumze. Ninadhani hatutoshindwa kufikia makubaliano kwa sababu tumefanya kazi kwa pamoja na tunajuana,”amesema Ivo.
Mkataba wa Ivo mwenye umri wa miaka 31, utamalizika Mei 20, mwaka huu na kiwango chake kimekuwa msaada kwa Simba, licha ya makosa machache yaliyoigharimu timu yake msimu huu na kusababisha kupoteza baadhi ya mechi ikiwamo ile ya Kagera Sugar FC iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo alimtemea Atupele Green mpira uliorushwa na Salum Kanoni na kumweka katika utata.

PACQUIAO AFANYIWA UPASUAJI WA BEGA


Pacquiao afanyiwa upasuaji wa bega
Bondia Kutoka Ufilipino Manny Pacquiao amefanyiwa upasuaji wa bega lake alilodai kuwa ndiyo iliyopelekea yeye kushindwa na Floyd Mayweather jumapili iliyopita.
Bondia huyo tayari anakabiliwa na kesi moja huko Nevada kwa kutosema ukweli kuhusiana na hali yake ya afya kabla ya pigano.
Hata hivyo daktari wake Neal ElAttrache, amesema kuwa amefurahia matokeo ya upasuaji huo licha ya ripoti kudokeza kuwa Pacquiao anahitaji muda wa mwaka mmoja kuuguza jeraha hilo.
Mayweather amesema hana pingamizi ya kuzichapa dhidi ya Pacquiao
Pacquiao mwenye umri wa miaka 36 alinyimwa dawa ya kupunguza maumivu kabla ya mechi alipokuwa akilalama kuteguka bega.
Hata hivyo imebainika kuwa kabla ya pigano hilo shirikisho la riadha na masumbwi ya kulipwa katika jimbo la Nevada lilipuzilia mbali ombi la shindano hiyo kwani haikuwa imearifiwa awali.
NAC inapendekeza kushtakiwa kwa bondia huyo mfilipino kwani hakusajili maumivu ya aina yeyote katika fomu maalum siku moja kabla ya pigano.
Manny anakabiliwa na kesi moja huko Nevada kwa kutosema ukweli kuhusiana na hali yake ya afya kabla ya pigano.
Kutokana na masaibu yake, mwanamasumbwi wa kulipwa Floyd Mayweather, 38,amejitokeza na kusema kuwa hana pingamizi ya kuchuana tena dhidi ya Pacquiao ila katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Awali mwanadondi huyo alikuwa amesema yuko tayari kuzichapa dhidi ya Muingereza Amir Khan miongoni mwa wanandondi wengine.

DADA YAKE ADEBAYOR AJIBU MAPIGO YAKE


Baada ya status ya Adebayor ambayo ilishtua watu wengi kwenye mtandao hao mchezaji Didier Drogba alimpost Adebayor na kumuombea mambo ambayo yanaenda vibaya na familia yake yaende vizuri. Sasa kwenye ile ile post dada yake Adebayor anaitwa Lucia Adebayor amemjibu akienda kinyume na status ya Ade.
Tafsiri yake kwa ufupi ni hii hapa,
“Endelea kuongopea kaka, yako wapi magari uliyompa mama. Umeyachukua yote. nyumba unayosema umemnunulia dada vyote ni uongo. Simu alizoiba Rotimi vyote ni uongo. Pesa sio kila kitu, sisi ni familia na hatukuitaji tena uwe peke yako na sisi tuwe peke yetu. Ukweli kwamba unazo sasa hivi lakini havikuhakikishi mambo ya kesho. Mungu akusamehe.”

TAARIFA MBAYA KWA MAN CITY:YAYA TOURE ANA ASILIMIA 90 KUONDOKA


Wakala wa nahodha na kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Touré Gnégnéri amethibitisha taarifa za uhakika wa mchezaji huyo kuchana na klabu ya Man City, mwishoni mwa msimu huu.
Dimitri Seluk wakala wa kiungo huyo anayeonekana kuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Man City, amekiambia kituo cha televisheni cha Sky Sports kwamba kuna asilimia 90 kwa Toure kuondoka Etihad Stdium.
Seluk hakusema ni wapi Toure, atapoelekea endapo atakamilisha mipango ya kuondoka mjini Manchester, lakini amesisitiza suala la mchezaji wake kuhitaji kubadili mazingira ya soka lake ambalo amelicheza akiwa nchini England kuanzia mwaka 2010.
Hata hivyo inadaiwa kwamba tayari klabu tatu barani Ulaya zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Toure.
Yaya Toure akiwa na wakala wake Dimitri Seluk
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, hakuwa na mafanikio makubwa msimu huu, kama ilivyokua misimu kadhaa iliyopita, na imebainika kuna baadhi ya mambo hayamfurahishi.
Vyombo vya habari nchini Italia, jana viliripoti kwamba uongozi wa klabu ya Inter Milan umeahidi kuyafanyia kazi mapendekezo ya meneja wa klabu hiyo kwa sasa Roberto Mancini ambaye ameonyesha dhamira ya dhati ya kumsajili Yaya Toure.
Mancini alimsajili Toure mwaka 2010, akitokea nchini Hispania alipokua akiitumikia klabu ya Barcelona kwa ada ya uhamisho wa paund million 24.

HIZI NDIZO TAARIFA SAHIHI ZA TIMU ALIKOENDA MSUVA KUFANYA MAJARIBIO


Jana habari mbalimbali za Msuva kusepa kwenda kufanya majaribio ya kucheza na soka huko South Africa zilisambaa sana. Kutoka kwenye vyanzo vyangu nililiripotu kama tetesi lakini leo asubuhi nimewasiliana na Msuva mwenyewe akiwa South Africa kupata uhakika zaidi.
Majibu ni kwamba hajaenda kufanya majaribio na Orlando Pirates, timu aliyoenda kufanya nayo majaribio ni Bidvest Wits ambayo pia inashiriki ligi kuu ya South Africa.
Bidvest Wits kwa sasa ipo namba 4 nyuma ya Pirates kwenye msimamo wa ligi. Msuva alipata nafasi pia ya kuangalia mechi kali kati ya Kaizer Chiefs vs Bidvest Wits. Hapo chini kuna audio ya sauti nikiongea nae pamoja na picha akiwa uwanjani kuangalia mechi.



Huyo jamaa aliyekaa na Msuva anaitwa Charles ndie aliyemuunganishia mchongo wa trial

BY MBEGEZE

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif