Tuesday, July 4, 2017

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 04.07.2017 na RAM MBEGEZE

TADHALI SUBSCRIBE MBEGEZE TV YOUTUBE KWA HABARI MBALIMBALI ZA KIMICHEZO

Mshambuliaji wa Uhispania na Chelsea Diego Costa, 28, anataka kuondoka Stamford Bridge kwa wakati anaotaka yeye, na jambo hilo linachelewesha hatua ya Chelsea kumsajili Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton (Daily Mirror).
Antonio Conte anataka Chelsea watoe hata pauni milioni 100 kumsajili Romelu Lukaku, kama Everton wanataka kiasi hicho ili kumuuza (The Telegraph).
Mshambuliaji kutoka Argentina Lionel Messi, 30, atasaini mkataba mpya Barcelona mara tu atakaporejea kutoka kwenye fungate yake baadaye mwezi huu (Goal).
Paris Saint-Germain wanajiandaa kupanda dau jipya la kumtaka mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, na wamewasiliana na wawakilishi wa mchezaji huyo (L'Equipe).
Arsenal wanapanga kutoa pauni milioni 70 kuwasajili viungo wawili kutoka Sporting Lisbon ya Ureno, William Carvahlo, 25, na Gelson Martins, 22 (A Bola).
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wayne Rooney
Arsene Wenger atakutana na Alexis Sanchez, 28, na Hector Bellerin, 22, wiki hii kujaribu kuwashawishi wasiondoke Emirates (The Sun).
Everton wana uhakika wa kumrejesha Goodison Park Wayne Rooney, 31, kutoka Manchester United msimu huu (TalkSport).
West Ham United wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez "Chicharito" , 29, kutoka Bayer Leverkusen (Telegraph).
Liverpool wanapanga kutoa euro milioni 12 kumsajili kipa wa Sevilla Sergio Rico (ABC Sevilla).
Chelsea wameonesha dalili kuwa wapo tayari kutoa pauni milioni 60 kumsajili beki wa kushoto Alex Sandro kutoka Juventus (Telegraph).
Barcelona wanaongoza katika mbio za kumsajili beki wa Juventus Leonardo Bonucci. Chelsea wanataka kumsajili beki huyo, lakini yeye angependa kwenda Barcelona (Daily Mirror).

Inter Milan wanataka kupanda dau la kumtaka mshambuliaji wa PSG Angel di Maria (Tuttosport).
Kipa wa zamani wa Arsenal Jens Lehmann anatarajia kurejea Emirates kama mmoja wa makocha wa kikosi cha kwanza (Guardian).
Gianluigi Donnarumma amekataa kuhamia Paris-Saint-Germain na amekubali kusaini mkataba mpya kusalia AC Milan (Sky Sport Italia).
Kiungo wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, 24, amefanya mazoezi na Birmingham City, akitaka kuhamia klabu hiyo kutoka Lazio (Daily Mirror).
Southampton wanataka kukamilisha usajili wa pauni milioni 8.75 wa mshambuliaji Yann Karamoh, 18, ambaye ana mzozo na klabu yake ya Caen ya Ufaransa (Sun).
Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya utakaompeleka hadi mwaka 2020 (AS).
Meneja wa Manchester United Jose Mpurinho anakasirishwa na hatua ya klabu hiyo kutosajili wachezaji zaidi ya Victor Lindelof, 22, peke yake mpaka sasa (Daily Mirror).
Jose Mourinho anataka mshambuliaji Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid na kiungo Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea wajiunge na kikosi chake kabla ya Jumapili watakapoanza safari ya Marekani ya mechi za maandalizi (Daily Star).
Real Madrid 'wamekomaa' na Alvaro Morata hadi Manchester United watakapotoa pauni milioni 79 (Marca).
Kiungo kutoka Guinea Naby Keita, 22, anataka kuhamia Liverpool, lakini klabu yake RB Leipzig inataka pauni milioni 70 (Daily Mirror).

Crystal Palace wameshindwa kulipa pauni milioni 30 wanazotaka Liverpool kwa ajili ya beki wa kati Mamadou Sakho, 27 (Guardian).
Manchester United wanajiandaa kupanda dau kumsajili beki Marc Bartra, 26, kutoka Borussia Dortmund (Manchester Evening News).
Newcastle bado hawajafanikiwa kumsajili kipa Pepe Reina, 34, kwa kuwa Napoli hawajapata mtu wa kuziba nafasi yake (Newcastle Chronicle).
Leicester City wamefanya mazungumzo ya awali na Sevilla kuhusu usajili wa kiungo Vicente Iborra (Sky Sports).

Kipa Wojciech Szczesny amerejea Arsenal kutoka Roma alipokuwa kwa mkopo kwa miaka mwili (Instagram).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kiingereza): Tetesi kuhusu uhamisho Ulaya
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.


Mnyate Abaki Simba Kibishi.




WINGA Jamal Mnyate aliyekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba amefunguka na kusema kuwa bado ataendelea kuwemo katika klabu hiyo kutokana na kuwa na mkataba na timu hiyo.
Mnyate alisajiliwa na Simba akitokea katika klabu ya Mwadui kwa mkataba wa miaka miwili lakini tangu alivyosajiliwa alifanikiwa kucheza mechi kadhaa kutokana na mara nyingi akiwa anasumbuliwa na majeruhi.
“Kwa hivi sasa ni ngumu kusema msimu ujao nitakuwa wapi, kwasababu bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Simba kikubwa mimi na wasikiliza wao waajiri wangu watakavyonambia kuhusu hatima yangu,”alisema.
Mnyate alisema hawezi kuzungumza chochote kwa sasa kutokana na kuwa bado yupo chini ya mkataba na timu hiyo, lakini angekuwa ameshamaliza nao mkataba angekuwa huru kusema msimu ujao angeenda timu gani.
Aidha,Mnyate amewapongeza  Viongozi wake kwa usajili walioufanya kwa kuwarudisha  wachezaji wao wa Zamani kama Emmanuel Okwi,Shomary Kapombe ambao walikuwa tishio  ligi kuu.

MUZAMIRU AGEUKA LULU AFRIKA KUSINI, WATAALAMU WAMSOGELEA KWA UKARIBU ZAIDI




Kiungo nyota wa Simba, Muzamiru Yasin amegeuka lulu kwa baadhi ya timu za Afrika Kusini.

Muzamiru yuko Afrika Kusini akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika michuano ya Cosafa ambayo imetinga nusu fainali kwa kuwatwanga wenyeji Afrika Kusini.

Taarifa zinaeleza, mawakala kadhaa wameanza kumfuatilia kwa karibu baada ya kuwa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri zaidi.

Moja ya magazeti ya Afrika Kusini yameeleza kuwa Muzamiru ni lulu kutokana na uwezo aliouinyesha katika mechi zote hadi taifa Stars inafikia nusu fainali ya michuano ya Cosafa.


Imeelezwa moja ya timu zilizovutiwa ni Bidvest na Mpumalanga Black Ace lakini wataalamu wanaofuatilia wachezaji au mawakala wanaweza kuwapeleka wachezaji katika timu hata za nje ya Afrika Kusini.

Katika michuano hiyo Muzamiru amekuwa injini kuu ya kuendesha kiungo cha Stars na kusababisha mvuto huo.

KAULI YA YANGA KUACHANA NA DIDA YAWASHITUA YANGA




Kauli iliyotolewa na Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali kuwa wameachana na kipa wao Deogratius Munish ‘Dida’ imeonyesha kuwashitua mashabiki wengi wa klabu hiyo.

Wengi wamekuwa wakihoji sababu ya Dida kuondoka na wengine wakimtaka kuvuta subira.

Lakini wako mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiutaka uongozi wa Yanga kukaa na kumalizana naye vizuri.

Wengine wameshauri kama amepata timu nje aende lakini si hapa Tanzania.

Pondamali alisema Dida aliwaambia hatasaini mkataba na juhudi za kumbembeleza zimekwama.


Hivyo kips African Lyon waliyemsajili, Beno Kakolanya waliyenaye na watasajili kipa mwingine chipukizi.

BAADA YA KAMATI YA UCHAGUZI KUSITISHA ZOEZI, KAMATI YA UTENDAJI INAKUTANA MCHANA HUU


KARIA: KAIMU RAIS WA TFF

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inakutana leo saa 7 mchana.

Inakutana kujadili suala la uchaguzi baada ya kamati ya uchaguzi kuahirisha mchakato wa uchaguzi.

Kamati hiyo iliahirisha mchakato wa uchaguzi baada ya mwenyekiti wake kutofautiana na wajumbe waliokuwa wakitaka Jamal Malinzi lazima afanyiwe usaili licha ya kuwa mahabusu.

Kama haitoshi, Mwenyekiti wake, Waikili Revocatus Kuuli alisema wajumbe walitaka kuwakata baadhi ya wagombea bila sababu za msingi.


Hivyo akaona hakukuwa na suala la weledi na kuamua kusimamisha mchakato wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

Hivyo, kamati ya utendaji ya TFF italisikiliza hilo na kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kuamsha mchakato huo wa uchaguzi.

EVERTON YAFANYA KWELI, YAMSAJILI KEANE KWA KITITA CHA PAUNI MILIONI 30



Everton inayodhaminiwa na SportPesa imeonyesha imepania kujiimarisha msimu ujao baada ya kumwaga pauni million 30 kumnasa beki kisiki Michael Keane kwa mkataba wa miaka mitano.

Keane alikuwa kisiki katika kikosi cha Burnley na klabu kadhaa kubwa zilionekana kumtolea “mimacho” lakini Everton imefanya kweli mapemaa.

Maana yake, Keane atakuwa kati ya wachezaji watakaotua nchini na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia Alhamisi ya Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.




-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif