Mourinho majanga
Majanga yanazidi kumuandama kocha mreno wa Chelsea, Jose Mourinho baada ya kukumbwa na adhabu ya kutakiwa kutokaa katika benchi la ufundi katika mechi moja na kisha kutakiwa kulipa faini ya £40,000 za kimarekani kwa kauli mbovu alizozitoa dhidi ya mwamuzi aliyechezesha mechi kati ya Chelsea na Westham weekend iliyopita.
Aidha kocha msaidizi wa Chelsea ambaye naye alitolewa nje kwa kadi nyekundu hakupewa adhabu bali ameandikiwa barua ya onyo inayomkumbusha majukumu yake kama msaidizi.
Adhabu hiyo ya Mourinho ni tofauti na ile ambayo alipewa alipotoa maneno yasiyo ya busara baada ya kufungwa magoli 3-1 dhidi ya Southampton majuma kadhaa yaliyopita na kwamba ataitumikia muda wowote.
Mourinho Jukwaani
Chelsea itasafiri hadi Britannia Stadium kucheza na Stoke City weekend ijayo na kwamba Mourinho atatakiwa kutekeleza adhabu hiyo mara moja, vinginevyo akate rufaa.
Sanjari na vitendo hivyo vya kinidhamu dhidi ya FA, Mourinho pia amekua akilaumiwa kwa jinsi alivyomtendea isivyostahili aliyekua daktari wa timu hiyo mwanadada Eva Carneiro na kusababisha aondoke klabuni hapo, huku sasa akiwa amefungua kesi mahakamani kutaka fidia zake.