Kiungo nyota wa Simba, Muzamiru Yasin amegeuka lulu kwa baadhi ya timu za Afrika Kusini.
Muzamiru
yuko Afrika Kusini akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
katika michuano ya Cosafa ambayo imetinga nusu fainali kwa kuwatwanga
wenyeji Afrika Kusini.
Taarifa zinaeleza, mawakala kadhaa wameanza kumfuatilia kwa karibu baada ya kuwa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri zaidi.
Moja
ya magazeti ya Afrika Kusini yameeleza kuwa Muzamiru ni lulu kutokana
na uwezo aliouinyesha katika mechi zote hadi taifa Stars inafikia nusu
fainali ya michuano ya Cosafa.
Imeelezwa
moja ya timu zilizovutiwa ni Bidvest na Mpumalanga Black Ace lakini
wataalamu wanaofuatilia wachezaji au mawakala wanaweza kuwapeleka
wachezaji katika timu hata za nje ya Afrika Kusini.
Katika michuano hiyo Muzamiru amekuwa injini kuu ya kuendesha kiungo cha Stars na kusababisha mvuto huo.
No comments:
Post a Comment