Kiungo
mkabaji wa CSKA Moscow ya Russia, Roman Eremenko amefungiwa miaka
miwili baada ya kubainika anatumia madawa ya kulevya aina ya Cocaine.
Eremenko
amepatikana na hatia hiyo baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
dhidi ya Bayer Leverkusen iliyopigwa Septemba 14, mwaka huu na
Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), limepitisha na kuitangaza adhabu hiyo.
Kutokana na adhabu hiyo, Eremenko raia wa Finland ataukosa msimu wote ujao pia utakaofuata nusu msimu.
Bodi
ya Uefa ya Uthibiti, Hadhi na Nidhamu imesema itaendelea kufanya
uchunguzi kama kawaida kwa wachezaji mbalimbali kama ambavyo imekuwa
ikifanya.