Friday, March 13, 2015

PSG KAMA IMELIPA KISASI KWA CHELSEA

Hakuna mchezaji yoyote wa Chelsea aliyemzidi David Luiz magoli msimu huu katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Rickie Lambert ana magoli mengi kuliko Diego Costa kwenye michuano ya klabu Bingwa Ulaya msimu huu.
Mwaka jana Chelsea iliitoa PSG kwa sheria ya bao la ugenini baada ya kufungana 3-3 mechi mbili. Mwaka huu PSG imeitoa Chelsea kwa staili hiyo hiyo huku matokeo yakiwa yale yale 3-3 kwa mechi mbili.
David Luiz aliiwezesha Chelsea kuitoa PSG mwaka 2014. Mwaka huu ameiwezesha PSG kuitoa Chelsea.
Chelsea ndio timu iliyopewa penati nyingi zaidi msimu huu katika michuano ya UEFA Champion League 
silva 2Na 

MSIMAMO WA LIGI YA BARA KABLA YA MECHI ZA KESHO

RnTimuPWDLFAGdPts
1YANGA169432191231
2Azam FC1686223121130
3SIMBA SC176832112926
4KAGERA SUGAR186751515025
5MTIBWA SUGAR175841817123
6Coastal Union185851312123
7RUVU SHOOTING185761214-222
8NDANDA FC186481722-522
9STAND UNITED175661618-221
10JKT RUVU175571416-220
11POLISI MORO184861316-320
12MGAMBO SHOOTING166281117-620
13MBEYA CITY174761216-419
14T. PRISONS1711061020-1013

MECHI ZA BONGO

Mechi za leo 2015-03-13
16:00TANZANIA - : -EGYPT
MICHEZO INAYOKUJA
2015-03-14
16:00SIMBA SCVs    MTIBWA SUGAR
16:00MBEYA CITYVs    MGAMBO JKT
16:00RUVU SHOOTINGVs    COASTAL UNION
16:00POLISI MOROVs    JKT RUVU

2015-03-15
16:00AZAM FCVs    NDANDA FC
16:00T.PRISONSVs    STAND UNITED
16:00YANGAVs    FC PLATINUM

ONA WCHEZAJI WA MAN UTD WANVYOTUA NA KUONDOKA MATIZI


Kawaida hapa nyumbani, wachezaji wa timu mbalimbali kubwa hupelekwa mazoezini na basi.

Huo ndiyo utaratibu, lakini inapofikia katika timu kubwa, kila mchezaji hutinga mazoezini na usafiri wake.
Picha hizi zinaonyesha namna wachezaji wa Man United ambavyo hutinga na kuondoka mazoezini wakiwa na usafiri wao.





MAKAPU:PLUIJIN AMEFANYA CHAGUO SAHIHI YANGA


MAKAPU (KUSHOTO) AKIPAMBANA NA AJIBU WA SIMBA....

MAKOCHA wanaweza kuwa ndiyo binadamu wanaoongoza kwa kulaumiwa kuliko wengi wote katika mchezo wa soka, ikiwezekana hata michezo mingine.

Mara nyingi, kocha anapoisaidia timu kupata mafanikio, kawaida huonekana ni mafanikio ya wengi, ikifeli, lawama zinaangukia kwake, hakuwa makini au hafai.
Tumeona hayo yakimuangukia Arsene Wenger wa Arsenal na makocha wengine wengi na hasa jambo la kujali vijana ambavyo limekuwa ni kama msumari kwa makocha wengi.
Jumapili iliyopita kulikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara uliosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini, kwa kuwa unawakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga.
Simba waiibuka na ushindi wa bao safi la Emmanuel Okwi, bao ambalo unaweza kuliweka katika historia ya moja ya mabao bora yaliyowahi kufungwa katika ligi hiyo.
Baada ya mechi hiyo, kama ilivyo ada kunakuwa na lawama nyingi na kawaida, mashabiki na hata viongozi wa timu hizo mbili kongwe, mara nyingi hawakubali kufungwa kimpira, badala yake kila mmoja huangusha lawama kivyake.
Moja ya lawama zilizoangushwa ni Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm kumtumia kiungo kinda Said Juma ‘Makapu’ ambaye alicheza katika kiungo cha ukabaji. Wengi walilalama kwamba Mholanzi huyo vipi aliamua kumchezesha kiungo huyo kinda katika mechi kubwa kama hiyo ya watani.
Wengi wanaona Makapu kwa kuwa ni kinda, basi alikuwa tatizo katika kikosi cha Yanga siku hiyo na wako waliopendekeza huenda Salum Telela angecheza siku hiyo.
Wako wanaoamini bora Yanga ingemchezesha Telela namba mbili na mkongwe Mbuyu Twite angerudi katikati kuendesha nafasi hiyo ya ukabaji kama ambavyo amekuwa akifanya mara kadhaa.
Hakuna aliyeiona kazi ya Makapu siku hiyo, wala hakuna anayeona jambo kubwa la msingi alilolifanya Pluijm kwa mchezaji huyo, kwa Yanga na Tanzania kwa jumla.
Makapu anayevaa namba 22 alikuwa kati ya wachezaji bora kabisa katika mechi hiyo, nitaeleza sababu kadhaa.
Moja:
Yanga haikuwa na tatizo katika kiungo cha ukabaji kwa kuwa alikuwa na nguvu na ukabaji wake ni ule wa kukera.
Ndiyo maana utaona kosakosa nyingi zilikuwa upande wa lango la Simba na Yanga wakashindwa kuzitumia lakini ulinzi wa Yanga ukiongozwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akisaidiana na Makapu na Yondani ulikuwa bora hadi walipofanya kosa lililozaa bao.
Hata ungemuweka mchezaji mkongwe, kosa walilofanya Yanga, bado lingeweza kuwa tatizo, ndiyo maana mpira wa mwisho wakati Okwi anafunga, aliupiga mbele ya Twite, lazima uamini yeyote anaweza kukosea.
Mbili:
Hakukuwa na mipira mingi ya juu iliyokuwa na madhara katika ukiachana na ule mpira aliopiga Elius Maguri mbele ya Cannavaro ambaye tayari alishaumia. Hii ilitokana na ubora wa mipira ya juu kuongezeka upande wa Yanga kwa kuwa Makapu ni kati ya wachezaji warefu na wanaopiga vichwa.
Tatu:
Makapu ana nguvu, ana uwezo wa kupiga miguu yote. Alikuwa na tatizo kidogo la nafasi, wakati upi mwafaka wa kuwa wapi na afanye nini. lakini hilo lilitokana na uzoefu alionao. Ili abadilike, ni lazima acheze, hiyo haina ujanja.
Kumlaumu Pluijm, pia ni sawa na zile lawama za msimu mmoja na nusu tu uliopita pale mashabiki walipomlaumu Kocha Ernie Brandts pale alipoanza kumuamini Telela aliyeonekana hafai na sasa wengi wanalia achezeshwe.
Kwa Pluijm, ana kila sababu ya kuendelea kumuamini Makapu, kinda mwenye kila sababu ya kucheza namba sita kwa kuwa ana sifa nyingi kwa asilimia 75 sasa. Anachotakiwa ni kuaminiwa na kupewa nafasi zaidi. Watu hujifunza zaidi hujifunza kwa vitendo, hivyo Makapu hawezi kujifunza akiwa benchi.
Kama Makapu ataendelea kupewa nafasi zaidi, basi ndiye shujaa na tegemeo wa Yanga hapo baadaye kama ambavyo Simba waliwaamini akina Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Said Ndemla na leo, ndiyo tegemeo la kikosi chao.
Acha wengine waone Plujm anakosea, lakini Makapu kucheza namba sita na sifa alizonazo ni chaguo sahihi kabisa, tena katika wakati mwafaka.

IVO AMTETEA BHARTEZ



Kipa mkongwe wa Simba, Ivo Mapunda amemtetea Barthez kwa kusema hastahili lawama kwa bao alilofungwa.

Ivo aliyewahi kudakia Yanga kwa zaidi ya misimu miwili amesema Barthez hastahili kulaumiwa kwa kuwa amefungwa bao bora.

“Bado naamini Barthez ni kipa bora na mwenye uwezo wa juu, hatakiwi kulaumiwa bali Okwi ndiye anatakiwa kupongezwa kwa kufunga bao kiufundi,” alisema Ivo.


Barthez alifungwa bao pekee lililoipa Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, Jumapili iliyopita.

Okwi alifunga bao akiwa katika kasi kubwa na kupiga mpira wa juu uliompita kipa huyo akiwa ametoka kidogo nje ya lango.

DALILI ZINAZOONESHA BHARTEZ ATAPOTEA YANGA ILA INATEGEMEA ATAKACHOKIFANYA DIDA



Nyanda wa Yanga, Ali Mustapha ‘Barthez’, amejipalia makaa na sasa kuna uwezekano mkubwa akasugua benchi katika michezo iliyobaki ya Ligi Kuu Bara na nafasi yake ikarudishwa kwa Deogratius Munishi ‘Dida’.

Barthez amekuwa katika wakati mgumu mara baada ya kufungwa bao na Mganda, Emmanuel Okwi katika mechi dhidi ya Simba, Jumapili iliyopita katika mechi ya Ligi Kuu Bara jambo ambalo limechangia kumvuruga.
Imeelezwa kuwa hatua hiyo ya kuwa na uwezekano wa kuwekwa benchi imetokana na mambo mawili; moja ni kuhofia kumuweka tena langoni kwenye mechi inayofuata akiwa na msongo wa mawazo kutokana na lawama anazopokea, lakini kingine ni kumuacha benchi ajifunze kwanza na kujiweka fiti upya.
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Yanga kimelipenyezea Championi Ijumaa kuwa, hata katika mechi inayofuata ya Yanga dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe itakayopigwa keshokutwa Jumapili, kipa atakayelinda lango la timu hiyo ni Dida.
Hata hivyo, imefafanuliwa zaidi kuwa, kurudi kwake dimbani Barthez, kutategemea na kiwango cha Dida atakachoonyesha.
“Kiukweli Barthez amekalia kuti kavu na nafasi yake imechukuliwa na Dida, yaani yule anaweza kucheza kama Dida ataharibu atakaporejea langoni. Vinginevyo itakuwa ndiyo basi tena.
“Bao alilofungwa na Okwi imeonekana naye alichangia kwa kiasi fulani kutokana na kutokuwa makini,” kilisema chanzo.
Kabla ya mechi hiyo, Barthez alisimama langoni katika michezo tisa mfululizo na kufungwa mabao mawili, lakini bao la Okwi ndilo limeonekana nuksi kwake.

MULO AELEZA SABABU ZILIZO MTOA MRWANDA KAMBINI


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro, amekanusha uvumi wa viongozi wa timu hiyo kumtimua kambini mshambuliaji wao, Danny Mrwanda na kudai kulikuwa na sababu kadhaa za mchezaji huo kuondoka kambini lakini siyo kwamba alifukuzwa.

Muro amesema sababu ya kwanza ya Mrwanda kuondoka kambini kwenye Hoteli ya Tansoma iliyopo Kariakoo jijini Dar ni kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
“Mrwanda hakufukuzwa, ni mgonjwa lakini pia ameondoka kambini kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mechi dhidi ya BDF,” alisema Muro na kuongeza:
“Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anatarajiwa kuingia kambini leo (jana) kwa ajili ya kupewa matitabu ya kiwango cha juu baada ya kuumia katika mechi ya Simba, Andrey Coutinho anaendelea vizuri baada ya kuanza mazoezi mepesi na wenzake.”

ANGALIA NEYMAR ANACHOKIFANYA AKIWASUBIRI MAN CITY


chelsea iko tayar kumtwaa varane


Chelsea imeamua kuboresha safu yake ya ulinzi na sasa iko tayari kumtwaa beki Raphael Varane wa Real Madrid.

Chelsea iko tayari kumwaga kitita cha pauni 40 kwa ajili ya kumnasa beki huyo inayeelezwa hana furaha.

Varane mwenye miaka 21 amekuwa hana furaha huenda kutokana na kutopata nafasi ya kucheza kwa kiasi kikubwa.


Madrid inawategemea wakongwe Pepe na Sergio Ramos.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif