Saturday, December 5, 2015

Baada Ya Kuondolewa Copa Del Rey Jana – Nini Hatma Ya Benitez/Madrid Dhidi Ya Getafe Leo Hii

Wakati bado wakiwa na kumbukumbu ya kudhalilishwa nyumbani na mahasimu wao Barcelona, kisha jana wakaondolewa kwenye michuano ya Copa Del Rey, leo hii kocha aliye kwenye presha Rafael Benitez ataiongoza klabu yake ya Real Madrid kuikaribisha Getafe Santiago Bernabeu.
  Getafe ndio wageni wanaokaribishwa Bernabeu usiku wa leo na kwa namna hali ilivyo hakuna mjadala wa kuwazungumzia – kwa sababu Madrid wamekuwa wakiandamwa na sakata la  kuondolewa kwenye Copa Del Rey baada ya hukumu iliyotolewa jana – na leo mashabiki wa timu hiyo wanatarajia kuonyesha hasira zao kwa kocha Rafael Benitez kwa kile kinachoitwa uzembe wa kumpanga mchezaji ambaye alikuwa kafungiwa.
Madrid/Benitez wanaingia kwenye mchezo wa leo huku baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu ambao kimsingi ndio wamiliki wa timu wameonyesha nia ya kuchukua hatua za kisheria kwa klabu.
 
Katika mechi ya leo, James Rodriguez ambaye alikuwa kwenye ubora wake katika mechi vs Cadiz, anatarajia kuanza.
   Jana ilitangazwa kwamba Benitez hakumuweka Marcelo katika kikosi cha mechi ya leo kutokana na majeruhi lakini cha kushangaza mchezaji huyo aliandika kwenye mitandao ya kijamii – “Nimepona kabisa na nipo tayari kucheza.” – jambo hili limezidi kuongeza sintofahamu baina ya Benitez na wachezaji wake.
  Leo pia tunaweza kuona ‘BBC’ wakicheza kwa pamoja tena. Benzema alifunga magoli 6 katika mechi 6 za kwanza za ligi lakini akaumia na akaanza kuandamwa na kesi ya ulaghai dhidi ya Mathieu Valbuena – na sikza hivi karibuni amekuwa ‘off form’. Cristiano, kwa upande mwingine anaonekana kurudi kwenye mstari baada ya kufunga magoli matatu katika mechi 2 zilizopita. Usiku wa leo Ronaldo anakutana na timu ambayo ameshaifunga magoli 18 katika mechi 10 zilizopita – zikiwemo hat trick 3 na magoli mawili mawili mara 4.

Vikosi vinavyotegemewa kuanza leo na mifumo

 Getafe hawana rekodi nzuri ugenini maimu huu – wameambuliwa kupata sare moja na magoli mawili tu katika mechi 6 zilizopita – rekodi mbaya zaidi ya ugenini kwenye La Liga. Leo usiku wa leo watakuwa bila Juan Rodríguez na hivyo wanategemewa kucheza kwa mfumo wa  4-1-4-1

HUYU NDIYE MKALI WA SERIE A


Higuani
Na Simon Chimbo
Magoli mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Gonzalo Higuain dhidi ya Inter Milan katika ligi kuu soka nchini Italia juma hili yalitosha kuipa usukani wa ligi Napoli kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka 25, na hayo yote yamewezekana kwa mchango mkubwa wa mshambuliaji Gonzalo Higuain, raia wa Argentina.
Katika mechi iliyokua ya kujua nani ataibuka farasi mshindi katika mbio hizo Napoli kupitia Gonzalo Higuain ilijipatia goli lake la kuongoza katika sekunde ya 65 tu kabla ya kuongeza lingine la pili na la ushindi na kuwaacha vijana wa Roberto Mancini wakitweta katika vita hiyo.
Gonzalo Higuain ameshaweka kambani mara 12 katika michezo 14 ya serie A hadi sasa na kuifanya Napoli kuwa juu ya ligi huku pia wakiwa hawajapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi walipocheza na Sasuollo.
Muargentina huyo anawakilisha vyema falsafa mpya aliyokuja mayo kocha Sarri huku wakicheza mpira wa kasi na kuvutia hususan katika eneo la mwisho la kiwanja, ambapo Higuain amekua akiongoza vyema safu ya ushambuliaji.
Achilia mbali magoli 12 katika michezo 14 lakini pia katoa assists 22 kwa wachezaji wenzake na kuwa na wastani wa asilimia 53 shot accuracy huku Messi akiwa na 59% na Ronaldo 50% ni rekodi adhimu.
Lakini yote haya yamekuja kutokana na ukweli kuwa ujio wa kocha Sarri katika klabu hii umeleta ari na mbinu mpya za ushindi wa Napoli sanjari na fomu ya mshambuliaji Gonzalo Higuain tofauti na kipindi cha kocha Rafael Benitez.
Kocha Rafael Benitez alikua akitumia mfumo wa 4-2-3-1 na kumfanya Higuain awe peke yake muda mwingi mbele na hivyo kushindwa kupata sapoti kubwa ya wenzake, wakati hivi sasa kocha Sarri amekuja na mfumo wa 4-3-3 unaowafanya washambuliaji wa pembeni ya Higuain kushirikiana naye vizuri kutengeneza nafasi za kufunga.
Ujio wa kocha Sarri ni neema kwa Napoli na sasa wanaongoza ligi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25, itakua ni ndoto kwa mashabiki wa Napoli siku wanatwaa ubingwa wa ligi hiyo ‘Scudeto’
Mashabiki wanafurahia soka zuri la kuvutia tofauti na misimu iliyopita, Higuain anafunga magoli, timu inapata ushindi, ni msimu mzuri sana kwa Napoli kama tu wataendelea na kasi hii.

Kauli ya Ivo Mapunda akiwa mazoezini kuhusu kujiunga na Azam FC


ma
Ivo Mapunda hivi sasa ni mchezaji wa Azam FC akiwa anaongeza safu ya kikosi hicho kwenye sehemu ya ulinzi wa lango lao. Kupitia Azam FC Ivo Mapunda alisema haya kuhusu yeye kujiunga na Azam FC’
“Naamini Azam ni timu bora, sawa timu bora Afrika Mashariki na Kati, hata kama ningeenda kucheza Kenya nadhani huenda nisingepata timu nzuri kama Azam, naamini kabisa ni professional klabu tofauti na klabu nyingine ambazo nimewahi kucheza kwa hapa Afrika Mashariki na Kati na ndio maana nikaona bora nibaki hapa niweze kucheza.”


Sababu za Messi kupewa Tuzo ya Mshambuliaji Bora La Liga na Kwanini Naamini Neymar na CR7 hawastahili kuwemo Top 3 Ballon D’Or

Sababu za Messi kupewa Tuzo ya Mshambuliaji Bora La Liga na Kwanini Naamini Neymar na CR7 hawastahili kuwemo Top 3 Ballon D’Or

kama tunavyojua wiki hii kulitolewa tuzo mbalimbali za Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ kwa msimu uliopita. Mojawapo ni ile ya mshambuliaji bora wa msimu ambayo ilichukuliwa na staa wa Barcelona, Lionel Messi. 
Kati ya tuzo zilizotolewa, kipa bora, beki bora na kocha bora na nyinginezo, lakini kidogo hii ya Messi imezua mjadala wa aina yake.
Wapo wanaoamini ilimfaa mpinzani wake wa karibu, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, wakiegemea katika hoja ya kutwaa tuzo ya ufungaji ambapo alimzidi Messi. Ni kweli, Ronaldo alifanya kweli katika ishu ya kucheka na nyavu, kwani alimaliza msimu akiwa na hat trick nane, dhidi ya tano za Messi.
  Ni dhahiri unapozungumzia sekta ya ufungaji bora, Ronaldo ama CR7 kama anavyofahamika, alistahili kuchukua tuzo hiyo, lakini kuna kitu kinachowachanganya wengi. Unapozungumzia mfungaji bora na mshambualiji bora ni vitu viwili, ingawa wote wanaweza kuwa na jukumu la kufunga.
Mshambuliaji bora ni aina ya mchezaji anayetegemea mfumo wa timu na mfumo wa kocha na ili afunge lazima awe kwenye muunganiko wa timu na kushiriki katika mipango yote ya kupatikana kwa bao. Hii ni sifa kuu inayowatofautisha watu hawa. Mfungaji bora yeye anaweza kujitegemea katika kulitafuta bao na asishiriki katika upatikanaji wa mpira hadi kufika langoni mwa mpinzani.
Ni kutokana na aina hizo, tunapata aina mbalimbali za washambualiji. Kuna wale ambao huitwa washambuliaji waliokamilika ‘complete strikers’, hawa hufanya kazi zote kulingana na mfumo na hushiriki kikamilifu katika kuisaidia timu kuanzia kuitafuta mipira mpaka kupatikana kwa bao. Hapa utakutana na watu kama Luis Suarez, Messi, Sergio Aguero.

Takwimu za Ufungaji za Messi na Ronaldo msimu uliopita
Wapo wale waitwao waviziaji (poachers), hapa unakutana na kina Javier Hernandez ‘Chicharito’ Filippo Inzaghi, Ruud van Nistelrooy. Pia kuna kundi la washambuliaji wao kazi yao ni kumalizia mipira langoni (target man) hapa wamo kina Oliver Giroud, Peter Crouch, Fernando Torres, Gonzalo Higuain na wengineo. Matumizi yao uwanjani ni tofauti na kariba ya ushambuliaji wa kina Messi.
 Kuna vitu vya kumuangalia mshambuliaji bora kama straika nini majukumu yake uwanjani kama kufunga. Kulingana soka la kisasa (modern football), straika kwa sasa ni zaidi ya kufunga. Kuna wakati eneo ambalo upo unaangalia jinsi ya kuisaidia timu yako na siyo suala la kufunga mabao wewe mwenyewe, ila mchango wako kikosini kwa jumla, achilia mbali kufunga kwako.
Ndiyo maana Jose Mourinho amekuwa akilumbana na Diego Costa, siyo kusema anashindwa kufunga tu, ila anaangalia mchango wake uwanjani katika kuisaidia Chelsea hasa kipindi hiki kigumu kwao.
Majukumu ya Messi si kuwa kama straika tu ndani ya Barcelona, ila uwezo wa kutoa asisti na uwepo wake kwenye safu ya ushambuliaji husaidia sana wenzake kufunga kiurahisi.
Mathalan angalia bao linalowania tuzo ya Puskas, anatoka katikati ya uwanja, anachambua mchezaji hadi mchezaji na kutupia mpira kambani. Hayo ndiyo mahitaji ya mshambuliaji katika soka la kisasa.

Matokeo ya kura zilizompa Messi tuzo ya Ushambuliaji Bora
Hivyo, Messi amekamilika, kulinganisha na CR7 ambaye kweli anajua kufunga lakini hajakamilika kwa mantiki ya mahitaji ya soka la kisasa. Hata takwimu zinaonyesha Messi alimaliza msimu akiwa na asisti 18 dhidi ya 16 za CR7
Pia  nigusie kuhusu tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Messi, CR7 na Neymar. Kwa mtazamo wangu, sioni kama CR7 alitakiwa kuingia safari hii, ukilinganisha na wengine walivyofanya vizuri. Ninaamini ilikuwa ni fursa kwa mmoja wa Juventus alitakiwa kuwemo katika majina haya.
Hakuna aliyekubali kuwa msimu uliopita Juve ilikuwa katika ubora wake na kweli walistahili kutoa mchezaji mmojawapo katika kinyanganyiro hiki. kati ya Paul Pogba ama Arturo Vidal mmojawapo alitakiwa kuingia.
 Mimi ni shabiki mkubwa wa Ronaldo, sidhani kama alistahili kuingia kulinganisha na wenzake walivyofanya mengi mazuri.
Niliwaangalia Neymar na Luis Suarez, siamini kama Neymar alitakiwa kuwemo mbele ya Suarez, labda pengine kwa kuwa Suarez alikuwa na adhabu kwa timu ya taifa. Suarez ana mchango mkubwa tena sana kuliko Neymar ambaye naweza kusema wanajaribu kupewa promo na makampuni makubwa kwa ajili ya kujitangaza kwa tija ya biashara nchini Brazil, lakini vinginevyo hakustahili mbele ya Mruguay huyo.
Ila kama ilikuwa sababu ya adhabu ya kinidhamu kwa Suarez, Neymar anastahili kuwemo lakini kwa mtazamo wangu, Ronaldo angetoka na kuingiza jina mojawapo kati ya Vidal ama Pogba kutokana na mafanikio makubwa waliyokuwa nayo msimu uliopita.

KIONGERA AANZA MAZOEZI SIMBA SC


Kiongera 2
Nyota wa Simba SC Raphael Kiongera ameanza mazoezi mara moja mara baada ya jana kutua visiwani Zanzibar ambako Simba imekita kambi kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Azam FC utakaopigwa December 12, 2015 kwenye uwanja wa Taifa.
Kiongera amejiunga na Simba akitokea Kenya ambako alikuwa kwenye klabu ya KCB kwa mkopo mara baada ya kupona majeraha ya mguu yaliyomsumbua kwa muda mrefu.
Kiongera 3
Simba imeamua kumrejesha mshambuliaji huyo baada ya kufanya vizuri kwenye klabu ya KCB ambapo mwezi August mwaka huu alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi huo.
Kurejea kwake ni habari njema kwani Simba imekuwa ikimtegemea zaidi Hamisi Kiiza huku washambuliaji wengine wakioneka kutomshawishi kocha Dylan Kerr.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif