Sunday, March 8, 2015

20 BORA YA WACHEZAJI WENYE UWEZO WA KUPIGA CHENGA NA KUFUNGA BAO C.RONALDO HAYUPO

Naposema “kufanikiwa au kukamilisha chenga” namaanisha kuwa unampiga mtu au watu chenga halafu unafanikiwa kuumiliki mpira bila kupokonywa na kisha kumpasia mwingine au kufunga au kufanya vyovyote vile, Yaani unapiga chenga bila kupokonywa mpira, Sasa hapo nadhani umenipata kwa ufafanuzi huo ili usije kubakia ushangaa hapa.



 Najua haujui ila nitakujuza hapa aisee…
 Lionel Messi ndie mchezaji aliepiga chenga nyingi kwa mafanikio barani Ulaya kwa zaidi ya misimu miwili iliopita kuliko mchezaji yeyote. Messi amepiga chenga 258 bila kupokonywa mpira, Kwa hiyo, Messi ndio top dribbler in Europe zaidi ya misimu miwili iliopita. Eden Hazard wa Chelsea anafuatia kwa ukaribu zaidi akiwa amezidiwa chenga nne tu na Messi.

 Hazard ana chenga 254. Hazard ni mmoja kati ya wachezaji wawili kutoka kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kuingia kwenye 10 bora hiyo.Eden Hazard Mwingine ni Raheem Sterling wa Liverpool mwenye chenga 172 akishika nafasi ya nane.

 Lakini katika hali ya kushangaza, mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo hayupo kwenye 10 bora hiyo na wala kwenye 20 bora ya waliopiga chenga na wakakamilisha chenga zao. Cristiano Ronaldo yeye hajafikisha hata nusu ya chenga za Messi na Hazard kwa hiyo zaidi ya misimu miwili. Cristiano amepiga chenga 99 kwa kipindi hicho zaidi ya misimu miwili, ambapo imemfanya kuwa nje ya 20 bora kwenye orodha iliotolewa. Takwimu hizo zinaonyesha jinsi wachezaji wafupi kina Messi, Hazard na Sterling walivyo wachezaji hatari kwenye timu zao kama wachezeshaji wakubwa.

 Na hapa ndipo wachezaji kutoka Ligi Kuu ya Ujerumani wanapotamba. Bundesliga imetoa wachezaji sita katika kumi bora ya wapiga vyenga bora barani Ulaya. Hapa utawakuta kina Arjen Robben (172) na Frank Ribery (175) wote wa Bayern Munich. Kuna winga Roberto Firmino (244) wa Hoffenheim, Raffael (222) wa Borussia Monchengladbach, Karim Bellarabi (206) wa Bayer Leverkusen, na Eric Choupo-Moting (200) wa Schalke 04. Lucas Moura wa Paris Saint Germain (PSG) anafunga kumi bora akiwa amepiga chenga 167. Hakuna mchezaji yeyote kutoka Ligi Kuu ya Italia alieingia kwenye kumi bora ya orodha hiyo.

MWAMUZI AMKAZANIA IVI KUTOA SHUKA LANGONI


Mwamuzi Martin Saanya amemlazimisha kipa Ivo Mapunda kuondoa taulo lake langoni.


Safari hii limeandikishwa maandishi ya "Jesus Helm Me", yaani Yesu Nisaidie."

Ivo alilazimisha lakini Saanya ambaye ni askari magereza alimueleza angempa kadi. Hivyo akaitandika taulo hiyo nje ya lango.

KTK PICHA HIVI NDIVYO SIMBA VS YANGA ZILIVYO ONESHANA UBABE MSIMBAZI WAKIIBUKA KIDEDEA

SIMBA IMEIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 DHIDI YA YANGA KATIKA MECHI YA LIGI KUU BARA KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR, LEO. HIZI NI SEHEMU YA PICHA ZA PAMBANO HILO KAMA HII, 'MUUAJI' , EMMANUEL OKWI ALIVYOKUWA AKIPAMBANA NA KELVIN YONDANI...


TAMBWE AKIPAMBANA NA JONAS MKUDE WA SIMBA...

KESSY WA SIMBA AKIMILIKI MPIRA MBELE YA JAVU WA YANGA, KUSHOTO NI NDEMLA WA SIMBA.

IVO MAPUNDA WA SIMBA AKIFANYA YAKE...

BEKI MGANDA WA SIMBA, JUUKO MURISHID AKILONGA NA MWAMUZI WA MECHI HIYO, MARTIN SAANYA...

TAMBWE AKIJARIBU KUWATOKA MESSI NA KESSY...

YONDANI WA YANGA AKIRUKA JUU KUMKWEPA KIPA WAKE ALLY MUSTAPHA HUKU MESSI WA SIMBA AKIANGALIA....


CANNAVARO WA YANGA AKIMWANGUKIA MESSI WA SIMBA,....


OKWI AKIJARIBU KUMTOKA CANNAVARO WA YANGA... 

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif