Tuesday, November 15, 2016

‘Nimepona ila siwezi kusaini timu yoyote hivi sasa – Mazanda’


steven-mazanda-1

KIUNGO  Steven Mazanda ametupilia mbali mpango wa kusaini timu yoyote katika dirisha hili la usajili Tanzania Bara na badala yake amejipa muda zaidi wa kupumzika hadi msimu ujao.
Mazanda, mchezaji wa zamani wa Moro United, Kagera Sugar, Tanzania Prisons na Mbeya City FC amekuwa nje ya uwanja tangu alipopata majeraha ya nyama za paja msimu wa 2015/16.
“Nimeshapona kabisa matatizo yalikuwa yakinisumbua, lakini kuhusu kusaini timu yoyote katika dirisha hili, hapana.” anasema Mazanda nilipofanya nae mahojiano mafupi akiwa mkoani Mbeya.
“Unajua timu zetu zina matatizo mengi makubwa, mchezaji ukiumia na kupata majeraha makubwa wanakuacha ukijibu wewe mwenyewe. Nimeona nipumzike msimu huu na Mungu akijalia nitarejea kucheza msimu ujao. Sasa napumzika kwanza.” alisisitiza kwa ufupi kiungo huyo wa kati mwenye pasi zenye macho na mwelekeo wa kusaka ushindi kwa timu yake.

NASRI AELEZA NAMNA GUARDIOLA ALIVYOWAZUIA KUFANYA NGONO BAADA YA SAA SITA USIKU




Kiungo wa Manchester City, Samir Nasri ambaye anakipiga Valencia kwa mkopo, amesema kocha Pep Guardiola aliwakataza kufanya ngono baada ya saa sita usiku.

Nasri ameliambia gazeti namba moja la michezo la L’equipe la Ufaransa kwamba, Guardiola aliwaambia baada ya saa sita usiku hakuna ngono kwa kuwa ni hatari kwao.

“Alisema ameweza kuwasaidia wachezaji kufanya vizuri kwa mfumo huo, alisema Messi au Lewandowski walifanya vizuri kutokana na kupunguza kufanya ngono baada ya saa sita.

“Alisema ukifanya hivyo unapata muda wa kutosha wa kupumzika na inasaidia sana,” alisema.
Nasri raia wa Ufaransa aliondoka Man City katika hatua za mwisho za kufunga dirisha baada ya kuona asingewezana na Mhispania huyo.

GARRY NEVILLE ATAJA FIRST ELEVEN YAKE YA MAN UNITED, AWATUPA NJE VIGOGO ROONEY, ZLATAN



Beki na nahodha wa zamani wa Manchester United, Garry Neville ametaja kikosi chake cha kwanza cha timu yake hiyo kwa wakati huu.

Neville aliyewahi kuwa kocha wa Valencia ya Hispania amewashangaza wengi baada ya kutaja kikosi ambacho hakina Wayne Rooney wala Zlatan Ibrahimovich.

KIKOSI ALICHOTAJA...
1. David De Gea 
2. Antonio Valencia
3. Daley Blind 
4. Chris Smalling
5. Eric Bailly
6. Michael Carrick
7. Paul Pogba
8. Ander Herrera
9. Anthony Martial
10. Henrikh Mkhitaryan 

11. Marcus Rashford

SCHUMACHER APATA NAFUU KUBWA, AANZA KUCHATI NA MASHABIKI MTANDAONI


Hatimaye dereva nyota wa zamani wa magari ya langalanga maarufu kama Folmura One, Michael Schumacher ameamka na kuonyesha matumaini ya kupona.

Schumacher raia wa Ujerumani ambaye alipata ajali wakati akiteleza kwenye barafu na kujikuta akikaa kwa zaidi ya miezi mitatu bila ya kuzungumza, sasa ameanza angalau kuwasiliana na mashabiki wake.

Schumacher  amekuwa akichati katika mitandao ya kijamii hasa Instagram na Facebook, hali ambayo imeibua matumaini.

Baada ya ajali hiyo mwaka 2013, hajawahi kuonekana hadharani tena na badala yake amekuwa akilala ndani tu.
Lakini maneno yake ya kuonyesha ujasiri kwenye mitandao ya kijamii, yanaonekana kuwavutia mashabiki wengi zaidi.


Hivi karibuni, alitupia maneno yakisema: “Usikate tamaa, endelea kusonga mbele”.

Safari ya Sturridge kuachana na Liverpool imeiva


jurgen-klopp-daniel-sturridge
Akiwa bado hajafunga bao hata moja hadi sasa kwenye ligi ya England (EPL), striker wa Liverpool Daniel Sturridge huenda akaachana na kikosi cha Jurgen Klopp.
Alitupia kambani wakati England ikiibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Scotland siku ya Ijumaa huku gazeti la The Mirror likiamini kwamba Sturridge yuko tayari kuachana na majogoo wa jiji ili kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.
Kwa sasa Daniel Sturridge anapamabana kupata nafasi nyuma ya mbrazil Roberto Firmino pamoja mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi.
sturridge
Inaripotiwa kuwa, Liverpool itahitaji kiasi cha pound milioni 28 kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji huyo aliyekulia kwenye academy ya Man City.

‘Ni lazima tujipange kushinda mechi zetu ili tujinasue-Shaaban Kado’


shabani-kado
Na Baraka Mbolembole
GOLIKIPA namba moja wa Mwadui FC, Shaaban Kado amesema timu yao itanyanyuka na kuondoka chini ya msimamo katika ligi kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na mtandao huu mapema siku ya leo Jumanne, Kado amesema ni juhudi zitakazoambatana na matokeo mazuri ndizo zinahitajika katika kikosi chao ili kuondoka katika nafasi ya 14 waliyopo baada ya michezo 15 ya mzunguko wa kwanza kumalizika.
Timu hiyo ya Shinyanga imefanikiwa kukusanya pointi 13 tu, baada ya kushinda michezo mitatu, sare nne na kupoteza jumla ya michezo nane.
Wastani wao wa magoli ya kufunga na kufungwa ni wa kiwango cha chini mno kwani wamefunga magoli 12 tu na kuruhusu nyavu zao mara 21 (wastani wa magoli -9).
“Kila msimu ligi inakuwa ngumu kuliko ilivyokuwa misimu ya nyuma.” anasema, Kado mshindi mara mbili wa tuzo binafsi ya golikipa bora wa VPL (2008/09 na 2014/15.)
“Hatukuwa na matokeo mazuri sana katika raundi ya kwanza, na hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na wachezaji wengi tegemeo kuondoka mara baada ya msimu uliopita kumalizika.”anaongeza Kado golilipa ambaye alidaka kwa kiwango cha juu katika game ya Taifa Stars vs Algeria miaka mitano iliyopita huko Algeria.
“Ili kujinasua katika nafasi za chini katika msimamo itatubidi kushinda tu mechi zetu. Tunajipanga kuhakikisha hilo linatimia.”

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif