Sunday, November 6, 2016

Takwimu muhimu kuelekea London derby, Arsenal vs Spurs leo

2Arsenal leo wanakabiliwa na kibarua kigumu watakapokuwa maskani yao Emirates kuwakaribisha mahasimu wao Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Premier Legue utakaofanyika saa tisa alasiri kwa majira ya Afrika Mashariki.
Timu zote zinaingia katika mchezo wa leo zikiwa na rekodi tofauti tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi mwezi August mwaka huu.
 
Dondoo muhimu kuelekea mchezo wa mahasimu hawa
  • Tottenham wameshinda mara moja kwenye dimba la Arsenal ndani ya mechi 26 walizokutana kwenye michuano yote tangu Mei 1993 (sare 10, kufungwa mra 15).
  • Ushindi huo ulikuwa ni ule wa 3-2 waliopata Novemba 2010, wakati walipotoka nyuma kwa mabao 2-0 kipindi cha kwanza na kufanya maajabu kipindi cha pili.
  • Arsenal hawajapata ushindi mbele ya Spurs kwenye michezo minne ya Premier League iliyopita (sare 3, kufungwa mara moja), na hawajawahi kucheza michezo zaidi ya mitano bila kupata ushindi dhidi ya mahasimu wao hao chini ya utawala wa Arsene Wenger. Hata hivyo waliwafungwa Spurs katika mchezo wa Kombe la Ligi msimu uliopita.
  • Mauricio Pochettino hajafungwa kwenye michezo minne dhidi ya Arsenal tangu alipowasili White Hart Lane. Hakuna kocha mwingine yeyote wa Spurs ambaye amewahi kufanya hivyo dhidi ya Arsenal.
  • Katika pambano la mahasimu hawa, timu inayotangulia kufunga imeshindwa kushinda mchezo kwenye matukio 23, idadi kubwa zaidi kwenye historia ya Premier League (sare 15, vipigo mara nane).
  • Mchezo pekee wa mahasimu hawa wa Premier Leage ulochezwa mchana ulikuwa ni ule wa Novemba 2004, Arsenal walishinda mabao 5-4 katika Uwanja wa White Hart Lane.
Arsenal
  • Arsenal wameshinda mechi 10 kati ya 11 zilizopita kwenye michezo ya ligi na Kombe la Ligi, wakifunga jumla ya mabao 32.
  • Wamepoteza mchezo mmoja tu wa Premier League lati ya 20 iliyopita (wameshinda 12, sare mara 7).
  • Mesut Ozil amehusika moja kwa moja kwenye mabao 8 katika michezo mitano iliyopita kwa upande wa Arsenal kwenye michuano yote (amefunga mabao matano, na kutoa assist tatu).
Tottenham Hotspur
  • Tottenham hawajafungwa kwenye mechi 10 za mwanzo za ligi kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1990-91.
  • Wasipofungwa leo maana yake watakuwa wamecheza mechi 11 za awali bila ya kupoteza kwenye Ligi ya Premier kwa mara ya tatu baada ya 1960-60 (michezo 16) na 1959-60 (michezo 12). Katika misimu yote hiyo walimaliza katika nafasi za kwanza na tatu mtawalia (licha kwamba wakati huo ushindi ulihesabiwa kwa poiti mbili).
  • Spurs wana rekodi nzuri ya safu ya ulinzi kwa sasa kwenye Premier League, wakirhusu mabao matano tu mpaka sasa.
  • Endapo watatoka sare leo, itakuwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tangu Aprili 2008.

CHELSEA YAONYESHA HAITAKI MCHEZO, YAITWANGA EVERTON KWA MABAO TANO KWA BAKULI



CHELSEA (3-4-3): Courtois 6.5; Azpilicueta 8, Luiz 7.5, Cahill 7.5 (Terry 84, 6); Moses 8, Kante 8, Matic 7.5, Alonso 8.5; Pedro 8.5 (Oscar 71, 6.5), Costa 8.5, Hazard 9 (Batshuayi 80, 6)
Subs not used: Begovic, Ivanovic, Chalobah, Aina
Goals: Hazard 19' 56', Alonso 20', Costa 42', Pedro 56'
Manager: Antonio Conte 8.5 

EVERTON (3-5-2): Stekelenburg 4; Williams 5, Jagielka 4.5, Funes Mori 4.5; Coleman 5, Barry 4.5 (Davies 66), Barkley 5, Cleverley 5, Oviedo 4 (Mirallas 36, 4.5); Bolasie 5 (Lennon 60, 5), Lukaku 5
Subs not used: Robles, Deulofeu, Valencia, Holgate
Booked: Jagielka, Barry, Bolasie
Manager: Ronald Koeman 4 
Referee: Robert Madley 6.5
Attendance: 41,429
Man of the Match: Eden Hazard 

Ratings by SAMI MOKBEL 





MANENO YA OMOG KWA WACHEZAJI SIMBA YAONYESHA NI FUNDI WA SAIKOLOJIA



Kocha Joseph Omog ameonyesha alivyo bora katika suala la saikolojia baada ya kuwaambia wachezaji wake, kazi haijaisha.

Omog raia wa Cameroon, amesema waliweka nguvu kubwa kwa Stand United kwa kuwa walijua ni timu ambayo haijapoteza mchezo kwenye Uwanja wa Kambarage na tayari iliisha vifunga vigogo, Yanga na Azam FC.

“Kasema baada ya hapo, African Lyon ni timu nyingine ngumu. Wachezaji hatupaswi kufikiria kazi imeisha.

“Ule mwendo ambao tumekuwa tukienda nao au tulioutumia dhidi ya Stand, dhidi ya Lyon inabidi iwe zaidi,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba.

Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara na hawajapoteza mchezo hata mmoja kati ya 13 ambayo wamecheza.


Leo wako Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kucheza mechi yao ya 14.

Katika saikolojia inaonyesha, kila binadamu baada ya kazi nzito hupenda kupumzika. Omog amejua wachezaji wake wangefurahi kupumzika au kuona kazi imeisha baada ya mechi ya Stand, jambo ambalo ni hatari kwa

PACQUIAO AMTWANGA MPINZANI WAKE MBELE YA FLOYD MAYWEATHER


Bondia Manny Pacquiao amemtwanga mpinzani wake Jessie Vargas kwa pointi na kubeba ubingwa wa Welterweight wa WBO.

Pambano hilo lililofanyika mjini Las Vegas, Marekani lilishuhudiwa na mpinzani mkubwa wa Pacquiao, Floyd Mayweather ambaye alitangaza kustaafu akiwa amecheza mapambano 49 na kushinda yote.













AUBAMEYANG AREJEA KIKOSINI, APIGA NNE DORTMUND IKISHINDA 5-2 BUNDESLIGA



Mshambuliaji nyota wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang ambaye alisimamishwa katakana na utovu wa nidhamu amerejea kikosini na kuonyesha ni mtu hatari baada ya kupiga mabao manne katika ushindi wa 5-2.

Dortmund imeigaragaza Hamburg SV katika mechi kali ya Bundesliga na kuifanya timu kushinda mfululizo katika  mechi tano.






-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif