Wednesday, February 18, 2015

UEFA EUROPA LEAGUE: ALHAMISI USIKU WAKE, WAINGEREZA LIVERPOOL, EVERTON, SPURS, CELTIC DIMBANI!

EUROPALIGI-NICEUEFA EUROPA LIGI itarindima Alhamisi Februari 19 kwa Mechi 16 za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 na Uingereza ina Timu 4 kwenye hatua hiyo.
Timu hizo ni Everton, Liverpool, Tottenham za England na Celtic ya Scotland.
Liverpool, Tottenham na Celtic zote zitacheza Mechi zao za kwanza Nyumbani na Everton kukipiga Ugenini na Young Boys ya Uswisi.
Liverpool, ambao Msimu huu walianzia UEFA CHAMPIONZ LIGI na kutupwa EUROPA LIGI baada ya kumaliza Nafasi ya 3 kwenye Kundi lao, watakuwa kwao Anfield kuivaa Besiktas ya Uturuki bila ya Kiungo wao Chipukizi Lazar Markovic ambae amefungiwa Mechi 4 na UEFA.
Besiktas, wakiwa na Straika hatari Demba Ba chini ya Kocha mahiri Slaven Bilic wa Croatia, ni Timu ngumu inayocheza Soka la uwiano chini ya Mfumo 4-2-3-1.
Tottenham wao wapo kwao White Hart Lane kucheza na Fiorentina ya Italy wakati Cetic wao watakuwa huko Italy kucheza na Vigogo wa Nchi hiyo, Inter Milan.
+++++++++++++++++++++
MECHI ZA TIMU ZA UINGEREZA:
Young Boys v Everton
Liverpool v Besiktas
Tottenham v Fiorentina
Celtic v Inter Milan
+++++++++++++++++++++
Raundi hii itahusisha Mabingwa wa Nchi zao 7 pamoja na Timu mbili zilizowahi kutwaa Kombe hilo huko nyuma.
Aalborg BK (Denmark), AFC Ajax (Netherlands), RSC Anderlecht (Belgium), Celtic FC (Scotland), Legia Warszawa (Poland), Olympiacos FC (Greece) na FC Salzburg (Austria) ni Mabingwa Watetezi wa Nchi zao.
Sevilla FC ya Spain ndio Mabingwa Watetezi ambao pia walitwaa Kombe hili Mwaka 2006 na 2007 wakati VfL Borussia Mnchengladbach waliwahi kulibeba Mwaka 1974 na 1979.
Mabingwa Watetezi, Sevilla, wao wataanzia Nyumbani kucheza na WajerumaniBorussia Monchedgladbach.
Marudiano ya Raundi hii ni Wiki ijayo Alhamisi Februari 26.
UEFA EUROPA LIGI
RAUNDI YA MTOANO TIMU 32
Alhamisi Februari 19
**SAA 3 Usiku
Young Boys v Everton
Torino v Athletic Bilbao
Wolsfburg v Sporting Lisbon
Aalborg v Club Brugge
Dnipro v Olympiakos
Trabzonspor v Napoli
AS Roma v Feyernoord
PSV Eindhoven v Zenit St Petersburg
**SAA 5 Dakika 5 Usiku
Guingamp v Dynamo Kiev
Anderlecht v Dynamo Moscow
Ajax v Legia Warsaw
Sevilla v Borussia Monchedgladbach
Villarreal v FC Salzburg
Liverpool v Besiktas
Tottenham v Fiorentina
Celtic v Inter Milan
Alhamisi Februari 26         
20:00 Zenit St. Petersburg v PSV Eindhoven
20:00 Dinamo Moscow v RSC Anderlecht
21:00 ACF Fiorentina v Tottenham Hotspur
21:00 Red Bull Salzburg v Villarreal CF
21:00 Besiktas v Liverpool
21:00 Internazionale v Celtic
21:00 FC Dinamo Kiev v Guingamp
21:00 Legia Warsaw v Ajax Amsterdam
21:00 Borussia Mnchengladbach v Sevilla FC
23:05 Club Brugge KV v Aalborg BK
23:05 Athletic de Bilbao v Torino FC
23:05 SSC Napoli v Trabzonspor
23:05 Olympiacos CFP v FC Dnipro Dnipropetrovsk
23:05 Sporting Lisbon v VfL Wolfsburg
23:05 Feyenoord Rotterdam v AS Roma
23:05 Everton FC v BSC Young Boys
Raundi zijazo
Raundi ya Mtoano Timu 16: Mechi 12 & 19 Machi
Robo Fainali: Mechi 16 & 23 Aprili
Nusu Fainali: Mechi 7 & 14 Mei
Fainali: Jumatano Mei 27, Tenth Anniversary Stadium, Warsaw, Poland

MOURINHO APONDWA KUISIFIA CHELSEA BAADA KUNUSURIKA PARIS!

MOURINHO-MIMACHOWAKATI Bosi wa Chelsea Jose Mourinho akiisifia Timu yake kuwa ni kubwa na imara baada kuponea chupuchupu huko Paris walipotoka 1-1 na 
Paris St-Germain katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Jumanne Usiku, baadhi ya Wachambuzi huko England wamemponda Meneja huyo.
Licha ya kukiri Chelsea ilibahatika kupata Sare na PSG, Mourinho aliisifia na kuisema Timu yake ni kubwa na imara: “Kazi ngumu ni kuijenga Timu kubwa na imara na sisi ni Timu kubwa na imara. Lakini haya ni mambo yasiyotabirika ya Soka!”
Hata hivyo Wachambuzi wamempinga Mourinho kwa msimamo huo, na hasa Roy Keane, Nahodha wa zamani wa Manchester United, ambae alitamka: “Nadhani wanao uwezo wa kuwa Timu kubwa na imara. Ni wazi yeye ni Meneja mkubwa na bora lakini kuwa Timu kubwa na imara ni kutwaa Mataji. Kusema hilo sasa ni upuuzi!”
Jumanne Usiku, ndani ya Parc des Princes Jijini Paris, Chelsea walitangulia kwa Bao la Branislav Ivanovic lakini Edinson Cavani akaisawazishia PSG na kama si uhodari wa Kipa Thibaut Courtois basi PSG wangeondoka na lundo la Magoli.
Mourinho alizungumza: “Ukiona umahiri wa Kipa wetu basi utakiri tumebahatika kutofungwa!”
Lakini matokeo hayo ni bora kuliko Msimu uliopita kwenye Robo Fainali ya Mashindano haya haya walipokung’utwa 3-1 na PSG ndani ya Parc des Princes na Chelsea kushinda Mechi ya Pili huko Stamford Bridge 2-0 na Bao hilo la Pili kufungwa Dakika za mwishoni na Demba Ba na kuwapenyeza kwa Ubora wa Goli za Ugenini.
Mourinho amesema: “Hii ni nafasi kwetu. Ni wazi Mechi mbili sasa ni moja. Sasa kila kitu kitaamuliwa Stamford Bridge, si katika Mechi mbili!”
Chelsea na PSG zitarudiana hapo Jumatano Machi 11 na Mshindi kutinga Robo Fainali.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif