Monday, March 9, 2015

KAKA AIOKOA TIMU YAKE ISIAIBIKE HUKO MAREKANI

BAO LA OKWI LATOA MAJIBU MENGI

SIMBA imeshinda bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo safi wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.








Mchezo huo ulikuwa mtamu na wa kuvutia, kila timu ilionyesha kiwango kizuri ingawa baadhi ya wachezaji walishindwa kuonekana kama ilivyokuwa imetakiwa. Kuna mengi yanaweza yanajitokeza katika mechi ya watani kama hiyo.


Achana na vituko, lakini utaona tofauti ya wachezaji hata wale uliokuwa unawategemea watang’ara wameshindwa kabisa kuonyesha viwango vyao kama ilivyozoeleka.


Lakini kuna wale ambao uliona hawawezi kuwa tishio ndiyo wamefanya kile ambacho wengi hawakukitegemea na ndiyo maana ya mechi ya watani, ni mechi ya mambo mengi.

Unalizungumzia bao lililomaliza mechi hiyo lililofungwa na Emmanuel Okwi baada ya kupiga mpira ambao uliokuwa si lahisi kudhaniwa ungeweza kuingia kwenye lango la Yanga.


Bao hilo limekuwa jibu sahihi la maswali mengi ya siku kadhaa kuhusiana na mechi hiyo ya watani ambayo kabla haijachezwa kunakuwa na maswali milioni watu wakijiuliza na kujijibu.



Wako ambao wamekuwa wakitabiri, wako ambao wamekuwa wakifanya ushirikina, wako ambao wamekuwa wakishikana uchawi na mwisho kuzozana, lakini shuti moja la ufundi kabisa la Okwi limetoa jibu la maswali zaidi ya mia watu waliokuwa wakijiuliza.
Ushirikina hutawala katika mechi ya watani, kusingiziana, watu kuhisi na kuziamini hisia zao ni sehemu ya mambo ambayo yamekuwa yakitawala katika mechi hiyo.



Wachezaji wanapewa huduma nzuri za kulala hoteli ambazo hawawezi kulala wanapokuwa wanakutana na Kagera Sugar au Ndanda FC. Lakini mwisho, bao la Okwi, limekuwa jibu sahihi.



Huenda huu ndiyo wakati mzuri pia kwa mashabiki wa soka nchini na wale wajanjawajanja ndani ya klabu za Yanga na Simba ambao wamekuwa wakisema wanakwenda kuroga, wapate jibu.


Bao la Okwi halina uchawi, bao la Okwi si la kishirikisha, mguu wake aliopiga si mguu wa shetani, badala yake kuna mambo matatu muhimu ambayo yakipewa nafasi yanaweza kuendeleza soka na wala si ushirikina.


Okwi ana kipaji, Okwi alikuwa mjanja kwa mawasiliano kati ya ubongo kupitia macho na baadaye kuamua kwa mguu. Lakini tatu, lazima tukubali juhudi aliyoifanya kutokana na kuwa fiti yaani mazoezi ndiyo lilikuwa jibu la uwezo wa kumaliza kazi aliyoifanya.


Wakati mzuri wa kuacha kuamini mambo ya kishirikina na kuheshimu kuwa mpira una mambo yake muhimu kwa ajili ya kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri.


Ushirikina katika soka hauna msaada, ni miradi ya wachache ndani ya klabu ambao wamekuwa wakisema wana mapenzi na klabu hizo, kumbe wanazipenda kwa kuwa zinawapa chochote kitu cha kuendesha maisha yao.


Kama upande wa Yanga walikwenda kufanya ushirikina vipi hawakufunga, hata Simba mbona hakuna bao la kishirikina na badala yake tumeona sayansi ya Okwi ilivyofanya kazi waziwazi? Vizuri kuachana na hisia duni ili kuepuka kuwa watu duni tusiokwenda na kasi ya maendeleo ya dunia.


Kingine cha nyongeza ni kusaka wachawi. Huu ndiyo utakuwa wakati wa Yanga kuanza kutangaza fulani na fulani ni tatizo au walihongwa. Bao alilofungwa Barthez, angefungwa yoyote kwa kuwa akili nyingi za Okwi zilikuwa za haraka kuliko kawaida.


Unaweza kidogo ukalifananisha na bao la Jaja raia wa Brazil aliyeifungia Yanga ikipambana na Azam FC. Lakini la Okwi, limekuwa bora zaidi kutokana na lilivyotokea. Hivyo soka ina mambo yake, Yanga wakubali wamepoteza waangalie mbele na si kuanza kupambana na kuvurugana.

FEDHA WALIZOINGIZA SIMA NA YANGA JANA KATIKA DIMBA LA TAIFA


Mechi namba 117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa, imeingiza jumla ya Sh milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C, Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia watazamaji 36,693.
Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600.
Mgao wa Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh. 11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata sh.81,727.83.
Wakati huo huo Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho siku ya jumanne katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.
Siku ya jumatano JKT Ruvu watawakaribisha Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Azam FC.
Aidha mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) barani Afrika kati ya Young Africans dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbabwe, itafanyika siku ya jumapili Machi 15, 2015 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
IMETOLEWA NA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA, BARAKA KIZUGUTO.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif