Wakati kikosi chake kikijiandaa kuikabili Mali kwenye hatua ya nusu fainali mwaka 2013 michuano iliyofanyika Afrika Kusini, Keshi alivishambulia vyama vya soka vya bara la Afrika kwa kuendelea kuajiri makocha wa kigeni bila mafanikio.
Usilete tu kocha ilimradi anatoka Ulaya na kuniambia yeye ni bora kuliko mimi. Sitakubali hilo hata kidogo,” alisema Keshi ambaye ni mshindi wa taji la Afrika (1994) akiwa nahodha na (2013) akiwa kocha wa Nigeria.
“Makocha wakigeni wanakuja kwa ajili ya pesa. Hawafanyi lolote ambacho kinatusaidia. Mimi sio mbaguzi lakini hivyo ndivyo ilivyo.”
Keshi alifariki mwaka uliopita lakini Afrika bado haijabadilika. Kati ya timu 16 zitakazoshiriki michuano ya Afrika nchini Gabon, ni makocha wanne tu wa Afrika watakaosimama kuviongoza vikosi vyao wakiongozwa na Aliou Cisse na Florent Ibenge ambao wanafahamika zaidi.
Cisse ambaye ni kocha wa zamani wa Senegal ‘Simba wa Terranga’ anarudi tena kwenye soka la Afrika akiwa alifika fainali mwaka 2002 wakati Ibege akiwa mshindi wa CHAN na kikosi cha DR Congo mwaka uliopita.
Wengine wawili ambao majina yao si maarufu ni Baciro Cande kocha wa Guinea Bissau na Callisto Pasuwa kocha wa Zimbabwe.
13 kati ya 16 wanatoka Ulaya huku Ufaransa ikiwa ndio nchi inayoongoza kutoa makocha wengi ikiwakilishwa na makocha wanne wawili zaidi ya Ubelgiji huku Israel, Spain, Poland, Ureno na Serbia zikitoa kocha mmojammoja.
Amerika Kusini ambako ni kitovu cha vipaji vya soka inawakilishwa na kocha mu-argebina Hector Cuper anakinoa kikosi cha Misri ambao ni mabingwa mara saba.
Taji la Afrika limebebwa mara 13 na makocha wa Afrika huku makocha wa kigeni wakiwa wamelibeba mara 16 ikiwa ni pamoja na msimu uliopita ambapo Herve Renard alilibeba akiwa na Ivory Coast.
Makocha wa AFCON 2017
Group A: Gabon – Antonia Camacho (Spain), Burkina Faso – Paul Duarte (Portugal), Cameroon – Hugo Broos (Belgium) na Guinea Bissau – Baciro Cande (Guinea Bissau).
Group B: Algeria – George Leekens (Belgium), Tunisia – Henryk Kasperczak (Poland), Senegal – Aliou Cisse (Senegal) and Zimbabwe – Callisto Pasuwa (Zimbabwe).
Group C: Ivory Coast – Michel Dussayer (France), DR Congo – Florent Ibenge (DR Congo), Morocco (Herve Renard) na Togo – Claude Re Loy (France).
Group D: Ghana – Avram Grant (Israel), Mali – Alain Giresse (France), Egypt – Hector Cuper (Argentina) na Uganda – Mulitin Sredojevic (Serbia).