Wednesday, February 10, 2016

Kiasi Cha Fedha Atakachokuwa Akilipwa Mourinho Man Utd Na Muda Wa Mkataba Wake Watajwa

Tetesi za kupewa kwa Jose Mourinho na klabu ya Manchester United zinazidi kushika hatamu kila dakika.
 
Gazeti la kila siku El Confidencial leo limeripoti taarifa za ndani za mkataba unaosubiriwa kusainiwa baina ya Jose Mourinho na waajiri wake wapya Manchester United.
Taarifa za ‘Special One’ kubeba mikoba ya Van Gaal zimechapishwa na kila chombo cha habari huko England asubuhi ya leo.
Vichwa vya habari vya magazeti vimeandika kwamba: Jose Mourinho amewaambia marafiki wa karibu kwamba atakuwa boss mpya wa United kuanzia msimu ujao.
  Kwa mujibu wa El Confidencial, wakati dili la kumleta Mourinho likiwa linamaliziwa katika hatua za mwisho, wakala wa kocha huyo Jorge Mendes na timu yake ya wanasheria kwa sasa wanaripotiwa kuwa kwenye kumalizia majadiliano ya vipengele vya mwisho na Red Devils.
Taarifa zaidi kutoka kwenye sehemu ya mkataba wa Mourinho na United ni kwamba mkataba utakuwa wa kuanzia msimu wa 2016/17 mpaka 2019/20, huku akiweka kibindoni kiasi cha 20 million euros kwa mwaka.

Ramires apokelewa kwa shangwe kuanzia airport


1
Baada ya kumaliza maisha ya soka kwenye barani Ulaya, Ramires amejiunga na club ya Jiangsu Suning inayoshiriki Chinese Super League.
Ramires amepokelewa na mashabiki na kukabidhiwa maua na mashabiki kuanzia alipowasili airport. Ramires tayari ameshaifungia goli moja club yake mpya kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Anzhi Makhachkala ya Russia.Ramires alisepa Chelsea kwa gharama ya £25million.
Ligi ya China inafanya juhudi kubwa kuwaleta mastaa wenye majina makubwa ili kuipa umaarufu ligi yao. Tayari kuna majina makubwa mengi kwenye ligi yao kama Robihno, Ramires, Asamoah na wengineo.
2

Azam FC kuzialika Tanzania TP Mazembe, Zesco United


COVER

Habari na mtandao wa AzamFC:
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kuwa mwenyeji wa michuano maalumu ya kimataifa ya timu nne itakayofanyika mwanzoni mwa mwakani.
Michuano hiyo ni ile waliyoenda kushiriki jijini Ndola Zambia hivi karibuni na kutwaa ubingwa, ambapo imeanzishwa kwa muungano wa klabu tatu, Azam FC, TP Mazembe na Zesco United.
Akizungumza hivi karibuni na mtandao wa www.azamfc.co.tz mara baada ya kikosi hicho kurejea kutoka Zambia, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alisema mwakani ni zamu yao kuandaa michuano hiyo na hivi sasa wanajipanga kuweza kuwaalika marafiki zao hao pamoja na kuangalia namna gani watakavyocheza nao hapa nyumbani.

“Tulialikwa kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo ilipofanyika Kongo katika mji wa Lubumbashi, ambapo tulikubaliana kimaandishi kwamba tutengeneze umoja huu, ambao ni umoja wa vilabu vitatu TP Mazembe, Zesco United na sisi Azam FC.

“Na mwaka huu tumepata nafasi hiyo tena kwa kualikwa, ambapo tumeweza kuwa mabingwa na mwaka jana TP Mazembe walikuwa mabingwa na akaenda kuchukua ubingwa wa Afrika (Ligi ya Mabingwa Afrika), kwa hiyo Azam FC mwaka huu tumechukua ubingwa tunategemea kupata matokeo mazuri katika mashindano ya CAF kwa sababu mechi nzuri na tumejiandaa,” alisema.
Kawemba alisema kuwa lengo kubwa la kuunda umoja huo ni kuweza kuzipa nafasi timu zinazoshiriki michuano ya CAF kuweza kufanya mazoezi kwa pamoja, huku akisisitiza kuwa michuano ya umoja huo ni mikubwa na sio kama wengi wanavyodhania.

“Ingawa watu wanaona kuwa hayana tija, lakini kwetu tunaamini ya kuwa yanatija na yametupa nafasi hiyo ya kujijenga, kila mtu aliona tulivyocheza mwaka jana dhidi ya El Merreikh baada ya kutoka Lubumbashi na mwaka huu tunaamini kabisa mechi ya Bidvest Wits itakuwa tofauti na tulikuwa tukisema hivyo pia hata hao wanaotubeza sasa hivi walikuwa wakituuliza Azam mnajiandaa kwa namna gani kwenye michuano ya Kimataifa, kwa hiyo haya ndio majibu na huwa hatuzungumzi bali tunafanya kwa vitendo,” alisema.

Aliongeza kuwa; “Na sio kama tunabeza mtu yoyote, hatuwezi kujiandaa kucheza dhidi ya Bidvest kwa kucheza na klabu ya hapa nyumbani, hakuna klabu yoyote inayoweza kutupa mazoezi hapa, kwa hiyo tumeenda kufanya mazoezi huko kwa ajili ya Bidvest na timu zinazokuja na kwa hapa nyumbani tumerudi, tumefanya mazoezi ya juu kidogo na tunaamini hakutakuwa na tatizo lolote.”
Bosi huyo aliwaondoa hofu mashabiki wa Azam FC kwa kuwaambia kuwa wamekuja kuendeleza pale walipoishia na hawana wasiwasi kwa yanayoendelea hivi sasa Tanzania katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

“Tunaangalia michezo yetu iliyoko mbele yetu na tuna uhakika tutafanya vizuri na tutakaa katika nafasi ambayo tunastahili kukaa na kila mtu anajua nafasi hiyo ni ipi,” alimalizia Kawemba.
Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB hivi sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejisanyia jumla ya pointi 42 sawa na Simba inayokamata nafasi ya pili na Yanga inayoshika usukani kwa pointi 43.

Lakini matajiri hao wa Azam Complex wana mechi mbili mkononi, zinazoweza kuwaweka juu kileleni kwa tofauti ya pointi tano kwa atakayemfuatia kama wakizishinda zote, jambo la kuvutia zaidi mpaka sasa ndio timu pekee kwenye ligi ambayo haijapoteza mchezo wowote.

WESTBROM DUUUUU


Timu ya soka ya West bromwich Albion imesonga mbele kwenye raundi ya tano baada ya ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Peterborough.
Dakika tisini zilimalizika kwa timu hizi kwenda sare ya bao 1-1 ambapo Jon Taylor alianza kuifungia timu yake bao la kuongoza kwenye dakika 55, ya mchezo.
Kiungo wa West Brom Darren Fletcher akachomoa bao hilo katika dakika ya 71 ya mchezo huo.
Katika changamoto za mikwaju ya penati wachezaji wa Peterborough Martin Samuelsen na Lee Angol walikosa penati zao.

McCarthy: Mourinho ndiye afaaye Man Utd

  Kuna uwezekano mkubwa Mourinho akamrithi Van Gaal Manchester United
Jose Mourinho ndiye afaaye zaidi kusaidia Manchester United kukabiliana vilivyo na Manchester City watakaokuwa chini ya Pep Guardiola msimu ujao, haya kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Porto Benni McCarthy.
BBC imefahamu kwamba huenda Mourinho, 53, aliyekuwa meneja wa Chelsea, huenda akateuliwa kumrithi Louis van Gaal kama meneja Old Trafford majira yajayo ya joto.
McCarthy, 38, alicheza chini ya Mourinho raia huyo wa Ureno alipokuwa mkufunzi wa Porto.
"Mourinho ni mmoja wa watu wanaojua jinsi ya kumshinda Guardiola na mbinu zake,” ameambia BBC Sport.
“Alipokuwa Real Madrid, alimshinda mara kadha. AKiwa Inter Milan, alifanikiwa pia dhidi yake (Guardiola).

Image copyright Getty
Image caption McCarthy alichezea Porto Mourinho alipokuwa meneja
"Kwa sasa sioni mtu yeyote anayeweza kumkabili Pep na mbinu zake Manchester City isipokuwa tu Mourinho akiwa United, atakwua na rasilimali, wachezaji na usaidizi wa kifedha wa kukabiliana na Guardiola."
Guardiola, alikuwa kocha wa Barcelona, kwa sasa ni mkufunzi mkuu wa Bayern Munich.
Klabu ya Manchester City ilitangaza majuzi kwamba atamrithi Manuel Pellegrini majira yajayo ya joto.



Image copyright PA
Mourinho alifutwa kwa mara ya pili Chelsea mwezi Desemba, baada ya kushindwa mechi tisa kati ya 16 za kwanza ligini.
Alifutwa kazi miezi saba tu baada ya kuongoza klabu hiyo kushinda Ligi ya Premia.
Alikuwa Chelsea kwa kipindi cha kwanza 2004-2007.

HOFU HOFU YA MOURINHO, TAARIFA ZAELEZA AKITUA TU OLD TRAFFORD, MATA, FELLAINI, WANAPIGWA BEI


Ujio wa Kocha Jose Mourinho katika klabu ya Manchester United sasa ni gumzo na hofu kuu.

Tayari taarifa zinaeleza kwamba kama Mourinho atatua Manchester United, mara moja atamuuza kiungo Mhispania Juan Mata.

Taarifa zinaeleza Mata aliyenunuliwa na Man United kwa kitita cha pauni million 37 kutoka Chelsea wakati huo Mourinho akiwa kocha, hata Marouane Fellaini aliyenunuliwa kwa pauni million 27 kutoka Everton, naye safari itamkuta.


Mata na Mourinho hawakuwa katika uhusiano mzuri wakati kiungo huyo alipoondoka Chelsea na kujiunga na Man United iliyokuwa ikifundishwa na David Moyes.

Hali hiyo inazidisha hofu, kwamba Mourinho ambaye inaelezwa tayari amekubaliana na Man United kuchukua nafasi ya Louis van Gaal.

Wachezaji hawana uhakika mani atabaki, mani ataondoka wakati kocha huyo atakapotua Old Trafford mwishoni mwa msimu.

ZLATAN APIGA BAO LA KIFUA IKIITUNGUA LYON 3-0


PSG: Sirigu, Maxwell, Silva, Aurier (Matuidi 84'), Marquinhos, Motta (Luiz 76'), Stambouli, Moura, Rabiot, Ibrahimovic (Di Maria 70'), Cavani
Subs (not used): Ongenda, Augustin, Kurzawa, Douchez
Booked: Luiz
Goals: Ibrahimovic 63' 67' Rabiot 75'
Lyon: Lopes, Jallet (Ferri 77'), Morel, Kone, Umtiti, Gonalons, Ghezzal, Darder (Grenier 74'), Tolisso, Lacazette, Cornet (Valbuena 67')
Subs (not used): Bedimo, Gorgelin, Yanga-Mbiwa, Labidi

Booked: Umtiti


LEWANDOSWKI APIGA MBILI NA KUMBEBA GUARDIOLA MWENYE JINAMIZI LA KUHAMIA MAN CITY



Bayern Munich imeshinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Bochum katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Ujeurmani.

Shukurani kwa mshambuliaji Robert Lewandowski aliyefunga mabao mawili yaani brace na kusaidia kupunguza presha kwa kocha Pep Guardiola anayehamia Man City.

Guardiola amekuwa kwenye presha kubwa kutoka kwa magwiji wa Bayern ambao wanaamini hawezi kukubaliana na timu nyingine suala la kuhamia kabla ya kumalizana na klabu hiyo kwa maana ya kumaliza kazi zake.


Wanaamini hawezi kuwekeza akili zake zote Munich. Lakini ushindi huo, unazidi kupunguza presha hiyo.





TAARIFA YA MOURINHO NA MAN UNITED


Muda mfupi baada ya taarifa kuzagaa kwamba boss wa Spurs Mauricio Pochettino huenda akachukua kibarua cha ukocha kwenye klabu ya Manchester United, tarari kuna taarifa zinazosema Jose Mourinho ameshamalizana na klabu hiyo ya Old Trafford.
The Sun linasema Man United wapo kwenye mazungumzo na wawakilishi wa manager wa Spurs lakini kiuhalisia inasemekana kocha huyo hana wakala.
Magazeti matatu ya Jumatano (leo) yametoka na vichwa vya habari vinavyofanana kila gazeti likidai Jose Mourinho ameshawaambia rafiki zake wa karibu kwamba yeye ni kocha mpya wa Manchester United.
Tangu kocha huyo atimuliwe na klabu yake ya zamani Chelsea, ripoti za Mourinho kuchukua mikoba ya Louis van Gaal mwishoni mwa msimu huu zimezagaa Ureno, Italia, Hispania na sasa England.
Jumapili iliyopita Louis van Gaal alikuja juubaada ya kuulizwa kuhusu hatma yake kunako Old Trafford baada ya Manchester United kuambulia sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Chelsea.
Hivi ni vichwa vya habari vya baadhi ya magazeti yaliyotoka leo huku habari kubwa ambayo imepewa uzito na magazeti yote ni kuhusu Mourinho kutua Man United.
Magazeti 2
Magazeti 1

RATIBA RAUNDI YA NNE AZAM SPORTS FEDERATION CUP HII HAPA

 
Ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imetolewa leo, ambapo jumla ya timu 16 zinakutana katika hatua hiyo (16 bora) itakayoanza kutimua vumbi wikiendi ya Februari 26-1 Machi 2015 katika viwanja mbalimbali nchini.
Michuano hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 64 kutoka ngazi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, inaingia katika mzunguko wa nne huku kukiwa na timu kutoka katika ngazi zote za ligi za TFF nchini.
Februari 26, 2016

Ndanda fc vs Jkt Ruvu

Coastal Union vs Mtibwa Sugar

Februari 27, 2016

Mwadui fc vs Rhino Rangers

Prisons vs Mbeya City/Wenda

Februari 28, 2016

Simba sc vs Singida United

Panone fc vs azam fc

Machi 1, 2016

Young Africans vs Jkt Mlale

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif