Arsene Wenger ni kocha wa kipekee kabisa kwenye ramani ya soka. Ni kocha ambae Arsenal imempa uhuru mkubwa wa kufanya kazi na kufanya maamuzi makuu kuhusu timu kuliko kocha yoyote kwenye ligi kubwa duniani.
Pale Uingereza ni kocha wa pili anaelipwa pesa nyingi kuliko kocha yoyote. Analipwa paundi milion 8.5 ukijumlisha na bonus za hapa na pale. Ni Mourinho pekee amemzidi mshahara.
Mashabiki wa Arsenal ndio mashabiki wanaolipa pesa nyingi za viingilio uwanjani Emirates, na ukilipa pesa nyingi unategemea makubwa kokote pale bila sababu za kujitetea kwa yule unaemlipa.
Nitaongelea miaka 10 iliyopita ya Wenger na kama anastahili kupewa mkataba mpya au la…
  1. MAKOMBE NA MAFANIKIO
-Kipimo kikubwa cha kocha mwenye mafanikio ni vikombe alivyochukua. Na kocha mwenye mshahara mkubwa kama Wenger analipwa mshahara mkubwa achukue makombe makubwa, sio FA Cup na EFL trophy. Sio Emirates Cup wala nafasi ya nne. Ni kuchukua Premier league title au Uefa Champions league.
Kama FA Cup ingekua ni kipimo cha kocha bora basi makocha kama Alan Pardew, Roberto Martinez, Steve Bruce, Tim Sherwood na Harry Redknapp wangekua wanalipwa mshahara kama wa Mourinho na Wenger na wangetakiwa wawe kazini hawajafukuzwa kwenye timu zao. Hata Louis Van Gaal alitwaa kombe la FA Cup na Manchester United Jumapili na Jumatatu asubuhi aliletewa barua ya kufukuzwa kazi. Hii inaonesha ni kiasi gani unapofundisha timu kubwa unatakiwa uchukue makombe gani.
Arsene Wenger ameshindwa kabisa kuchukua taji la Premier league kwa miaka 10 iliyopita. Na sababu kubwa aliyojitetea nayo kwa miaka hiyo 10 ni kwamba Arsenal haikua na nguvu za kupambana kiuchumi na timu nyingine kubwa zilizochukua taji la PL. Okay, Claudio Ranieri kafanya nini na Leceister City msimu uliopita? Gharama za malipo ya mshahara za Leceister City msimu uliopita kwa timu nzima ilikua ni paundi 48m. Hii hela haitoshi hata kumnunua Mesut ozil mmoja.
Msimu wa 2015/2016, msimu ambao arsenal kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11 ilimaliza juu ya Manchester United, Chelsea, Manchester City, Liverpool na hata Tottenham, bado Arsene Wenger “alifanikiwa” kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Leceister City kwa tofauti ya pointi 10. Sio point 1, 2, 3, 4 au 5. Point 10.
Kwa miaka 12 sasa Arsenal haijawahi kushiriki mbio za Ubingwa wa England kwa ufasaha. Ninaposema kwa ufasaha naamanisha kua inapofika mwezi April, kimahesabu bado una nafasi ya kuchukua ubingwa lakini kimahesabu. Mara nyingi mbio za ubingwa Arsenal zinaishiaga mwezi February na kuna miaka zinaisha kabisa mwezi November na mbio za kutafuta nafasi ya 4 zinaanza rasmi. Hivi hata Yule Brendan Rodgers wa Liverpool ya mwaka 2014 alimshinda Wenger. Alikua kwenye ubingwa hadi mwezi May wiki ya kwanza. Hili ni swala lisilokubalika kabisa kwa timu kubwa Uingereza kama Arsenal.
Kama utashangaa rekodi mbovu ya ubingwa wa PL, utashangaa zaidi rekodi mbovu Arsenal iliyonayo kwenye michuano ya Ulaya (UEFA).  Arsene Wenger anajitahidi sana kutetea rekodi yake ya kushiriki UEFA kwa miaka 20, lakini huwa haongelei kabisa amelichukua ilo kombe la UEFA mara ngapi. Nitakusaidia kukumbuka, ARSENE WENGER HAJAWAHI KUCHUKUA UBINGWA WA UEFA TANGU MUNGU AMEWAUMBA ADAM NA HAWA.
Kibaya zaidi ni rekodi yake kutovuka hatua ya 16 bora kwa miaka 6 mfululizo. Timu yenye nia ya kuchukua ubingwa wa UEFA itavumilia rekodi hii kwa kocha mmoja tu?Arsenal inakutana na Bayern Munich msimu huu kwenye raundi ya 16. Kuna dalili itakua mwaka  wa 7 kutovuka hatua hii ya 16 bora.
Kocha alieshindwa kuchukua ubingwa wa UEFA msimu ambao Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Manchester United, Juventus, AC Milan walifanya vibaya mwaka 2004, (nafikiri wote walitoka hatua ya 16, makundi na robo fainali) na kikosi chake kilikua na wachezaji kama Henry, Bergkamp, Viera, Cole, Campbell na Pires kikafungwa na kikosi cha Chelsea robo fainali na kuachia timu kama Monaco na Porto kufika fainali kwa miaka ile, huyu ni kocha ambae kidogo kutakua na shida ya “tactical flexibility na mental strength” kwenye set up zake.
Kwa kocha anaelipwa Paundi milion 8 kwa mwaka, hiki ni kitu kisichokubalika, labda kama haujui paundi milion 8 ni pesa nyingi kiasi gani.
  1. USAJILI WA WACHEZAJI NA STYLE YA KUONGOZA TIMU KWENYE MAJARIBU
Arsene Wenger kwa historia ni kocha asiyependa kutumia pesa nyingi kwenye usajili. Miaka kama mitatu nyuma amejirekebisha lakini bado kuna matukio yametokea hapo nyuma unajiuliza kwa nini huyu mzee anafanya haya mambo.
Skendo ya Arsenal kuongeza “shilingi moja” ili kutindua kipengele cha kumnunua Suarez kutoka Liverpool ni moja ya vitu vya kihistoria kwenye soka. Hebu fikiria Arsenal wangetoa paundi milion 50 kwa liverpool kwa mwaka ule, kwani wangekataa? Never! wasingethubutu. Lakini walitoa paundi milion 50 kumchukua Ozil kutoka Madrid aliekua hatakiwi tena na naamini Arsenal hawakumtaka Ozil, ila walivyogundua anapatikana basi wakaamua kumnunua kwa sababu tu ni jina kubwa na walitaka kufariji mashabiki.
Simkatai Ozil, ni mchezaji mzuri sana lakini Ule mwaka kilio cha Arsenal ilikua ni kununua Mshambuliaji wa kiwango cha juu. Hatukuhitaji kiungo mshambuliaji, Arsenal ilikua na Carzola, Arteta na wote hawa wangecheza CAM role vizuri.
Madrid walimuweka Gonzalo Higuan sokoni kwa paundi milion 30 tu. Wenger aliona ni pesa nyingi yeye akabaki kwenye paundi milion 25. Napoli wakalipa, na kwa sababu ya upachikaji wake hodari wa magoli Napoli wamemuuza Higuain kwa  Juventus kwa shilingi paundi milion 100 kasoro.
Hebu waza Arsenal ingekua na Gonzalo Higuain au Luis Suarez leo. Namlaumu Wenger kwa hili kwa sababu angekua na nia ya kuchukua hawa watu angewachukua, instead alivyoona amekosa vyote akaamua kuwatuliza mashabiki kwa kumnunua Ozil kwa milion 50. Good player but we needed a world class Striker muda ule.
Kitendo cha Klabu kuruhusu wachezaji wake nyota kuondoka kwa sababu tu ya kutoelewana kwenye mishahara na wachezaji kuuliza lengo la klabu kuchukua makombe kulitia doa kubwa sana jinsi dunia inavyoichukulia Arsenal.
Kuwaachia kirahisi kabisa world class talent kama za Cesc Fabregas, Samir Nasri na Robin Van Persie kulionesha ni kwa kiasi gani hii timu haihitaji mambo makubwa. Mimi siamini Arsenal walishindwa kuwalipa hawa, nafikiri walitaka tu kufanya biashara lakini kwani waliwauza sh ngap na kiwango chao kilikuaje? Mbona kama waliuzwa bei rahis sana? Kuna aliyeuzwa hata Paund milion 30? wote waliuzwa chini ya milion 25 labda ukijulimsha na ad ons.
Hawa wachezaji wote waliondoka na kwenda kuchukua mataji makubwa ya ligi na kwa hilo tu walithibitisha uondokaji wao Arsenal ulikua ni sahihi, haijalishi sasa hivi wako wapi, lakini wameshinda mataji ambayo Arsenal hawajayachukua (premier league title). Halafu Fabregas unajua alitaka kurudi? Wenger akasema hamuhitaji eti kwa sababu ana Ramsey, Wilshere na Mikel Arteta na Ozil pia. Mwangalie Fabregas sasa hivi, Ana assist 34 tangu mwaka 2014 za PL na 101 kwa pamoja na atachukua ubingwa  wa PL na Chelsea msimu huu.
  1. MATOKEO MABOVU DHIDI YA VIGOGO WENZIE
Katika miaka 10 iliyopita Arsene Wenger amepokea vipigo vya kuaibisha na kudhalilisha. Kuna matokeo mengine ameyapata dhidi ya timu ndogo na timu inayotaka kusonga mbele haiwezi kuvumilia kukubakisha.
Sare 4-4 dhidi ya Newcastle, baada ya kuongoza 4-0 mpaka dakika ya 72, kufungwa 8-2 dhidi ya Man United Old Trafford kufungwa 2-0 na Manchester United na kikosi kibovu kabisa, au wakati m’baya  niliowahi kushuhudia kwa Man united, chini ya  uongozi wa David Moyes, timu nyingi zilifuta uteja msimu ule ila sisi tulishindwa kumfunga hata mechi moja.
Ndani ya msimu mmoja wa 2014/2015, Arsenal ilifungwa 6-3 na Manchester City, 6-0 dhidi ya Chelsea, na 5-1 dhidi ya Liverpool kwenye mechi za PL. Kwenye UEFA iliifunga Andeletch 3-0 mpaka dk ya 60, na mpira uliisha kwa Sare ya 3-3. Nyumbani Emirates.
Msimu wa 2015/2016 Kufungwa na Dynamo Zagreb 2-1, timu ambayo haikuwahi kushinda hata mechi moja ya UEFA kwa kipindi cha miaka 10, lakini walifanikiwa kutufunga tu sisi, na wakamaliza wa mwisho kwenye kundi. Pia Bayern Munich walitufunga 5-1 msimu huo. Pia Sheffeild Wednesday inayoshiriki daraja la kwanza walitufunga 4-0 kwenye Capital One Cup na Southmpton wakatufunga 4-0. Yote hayo ndani ya msimu mmoja
I love Wenger. I respect him, lakini nafikiri kwa rekodi kama hizi hastahili kupewa mkataba mpya. Apewe cheo kikubwa kingine lakini mkataba mpya hapana. Kocha anayelipwa paundi milion 8 kwa mwaka hana tabia hizi.
  1. UCHUMI
Hapa sasa ndio kuna mchanganyo. Na wengi wanaamini kuwa Wenger ameijenga Arsenal na kuipa uchumi imara. Ni kweli, kwa miaka flani amefanikiwa kwenye hili. Lakini kwa miaka ya hivi karibuni, HAPANA. Kwa sababu hela zinazotumika kwa sasa Arsenal haziendani na mafanikio ya Arsenal uwanjani kulinganisha na timu nyingine za kawaida tu Ulaya na hata Uingereza.
Arsene Wenger analipwa pesa nyingi kuliko mtu yoyote Arsenal. Ni kocha wa pili kwa mshahara mkubwa kwenye ligi ya Uingereza na kocha wa nne kwa mshahara mkubwa Ulaya nzima. Amefanya nini kustahili yote haya kwa miaka 12 iliyopita? Mimi sijui labda wewe unajua. Au FA Cup na UEFA qualifications? Hazitoshi bana.
Kwa mwaka 2014, mshahara mzima kwa wachezaji wote na staff wa Arsenal ulifikia paundi milioni 200, na kuthubutu hata kuipita Chelsea kwa mara ya kwanza tangu lini sijui.
Mwaka 2008 mshahara wa staff nzima wa Arsenal ulifikia paundi milion 100. Ranieri alichukua ubingwa na Leceister City kwa bajeti ya mshahara wa staff wote wa shilingi paundi milion 48 tu.
Kwa muda mrefu tu, Arsene Wenger ameruhusu kabisa Arsenal kulipa mishahara mikubwa tu kwa wachezaji kama Yaya Sanogo, Niklas Bendtner, Park Cho Young, Mathew Flamini (mara mbili), Almunia, Diaby(good player lakini majeruhi), Denilson, Squilachi, Eboue, Andre Santos, Chamakh, Amauri Bischorf, Carl Jenkison e.t.c
Hivi hawa watu angewatoa na kuamua kuwalipa mishara mizuri tu Van Persie, Nasri, Fabregas au angenunua wachezaji wazuri kabisa na kuwalipa pesa nzuri, si ingewezekana? Mbona ni simple logic tu. Matumizi gani haya ya pesa lakini? Sahivi anabishana kuwalipa mshahara mzuri Sanches na Ozil na kuna watu kama Sanogo na Carl Jenkison wako tu wanakula pesa nzuri tu.
Hebu angalia Tottenham inavyojiendesha. Walimuuza gareth bale milion 100 lakini angalia timu waliyoitengeneza na kocha waliemchukua. Angalia Liverpool inavyoenda na ‘ka budget ka kawaida’ tu. Yote hii inasababishwa na Uongozi mzuri unaojua kupanga mambo. Sawa wamefanya vibaya miaka ya hivi karibuni lakini angalia jinsi wanavyofanya maamuzi magumu kwa timu kusonga mbele.
  1. MAKOCHA WA TIMU PINZANI NA MENGINEYO
Nafikiri Wenger atapata shida sana kupambana na makocha wenye damu changa kama Klopp, Pep Guardiola, Conte, Mourinho, na Pochetino. Arsenal anaweza maliza juu ya hawa watu lakini bado hachukui ubingwa ataishia nafasi ya pili au ya 3. Nasema hivi kwa kulinganisha muda aliokaa Uingereza na makocha wageni kama hawa, wangekua na uzoefu kama yeye angemaliza juu yao kweli?
*-Conte:-* Ebu angalia alipoichukua Chelsea. Timu ilikua imesambaratika kabisa na wachezaji wakubwa walikua wanazama shimoni (Fabregas, Costa, Hazard). Jiulize ana muda gani Uingereza na hata usajili wake ulikua ni wa kusua sua lakini angalia Chelsea inavyocheza na jiulize akitulia itakuaje.
*Klopp:-* Anazingua sana, lakini naamini ni kocha ambae angetakiwa aje Arsenal. Angalau style ya mchezo anayocheza inaeleweka na naamini with few good signings Klopp atasumbua sana Uingereza. Rekodi yake dhidi  ya vigogo pale UK inajieleza na ana mwaka mmoja tu na nusu. Sisi je?
*-Pochetino* Hebu angalia wachezaji anaofanya nao kazi na nafasi aliyoko kwenye Premier League. Angalia budget yake, angalia muda aliokaa UK na angalia umri wake. Sawa anazingua sometimes lakini angalia Tottenham imetoka wapi na  sasa hivi inaenda wapi. Angalia rekodi yake dhidi ya timu kubwa halafu angalia ya kwetu. Tunaweza maliza juu yao lakini itakua ni kwa kupigana na kwa bahati kama msimu uliopita tulivyosherekea kumaliza juu yao bila aibu tena kwa bahati tu.
HITIMISHO
Namheshimu sana Mzee Wenger. Ameifanyia makubwa Arsenal na mashabiki wote wa Arsenal wanatakiwa kutambua mchango wake. Lakini hii haizuii kuonesha kua muda wa Arsene Wenger kuifundisha Arsenal umekwisha. Hastahili mkataba mpya tena. Uongozi wa Arsenal ukae chini utulie, utafute mrithi sahihi ambae ataitoa Arsenal hapo ilipo na kuipeleka hatua nyingine ya juu zaidi.
Kama atasaini mkataba mpya basi itaonesha Arsene Wenger ni mkubwa kuliko Arsenal.