Kocha Charles Boniface Mkwasa yuko katika rada za Yanga na tayari wamefanya mazungumzo naye.
Mkwasa amezungumza na Yanga kuhusiana na suala la kurejea kuchukua nafasi ya kocha msaidizi.
Taarifa za ndani za Yanga, zinaeleza Mkwasa anaonekana kuwa mkali na anayetaka kufanya mambo yake kwa uahakika.
“Mkwasa
ni mkali, kocha msaidizi anatakiwa kuwa ni yule ambaye hataki mchezo.
Hivyo uongozi wa Yanga unaonekana kutaka kumrejesha.
“Umezungumza naye mara mbili na inawezekana kweli akarejea,” kilieleza chanzo.
Pamoja
na Mkwasa, mwingine anayeweza kutua Yanga katika benchi jipya la ufundi
ni Manyika Peter, kipa wa zamani wa timu hiyo ambaye amekuwa akifanya
kazi na Mkwasa katika kikosi cha timu ya taifa.
Pia kiungo wa zamani wa timu hiyo, Sekilojo Chambua anapewa nafasi ya kuchukua nafasi ya meneje, Hafidhi Saleh.
Uamuzi
wa Yanga unafuatia kubadilishwa kwa Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm na
kumchukua George Lwandamina wakati Yanga ikiwa ndio imeanza kuamka.