Saturday, November 19, 2016

REKODI HIZI NANI KUWA MBABE? MECHI YA MAN UTD VS ARSENAL VS

Wikiendi hii ligi mbali mbali barani Ulaya zitaendelea, baada ya kusimama wiki iliyopita kupisha mechi za kimataifa kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi. Kwenye ligi kuu nchini England Manchester United itakuwa mwenyeji wa Arsenal kwenye uwanja wa Old Trafford.
Man United iliyopo nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 18 itaingia kwenye mechi hiyo ya mzunguko wa kumi na mbili bila mshambuliaji wake Zlatan Ibrahimovic anayetumikia adhabu. Pia itawakosa mabeki wake mahiri Eric Bailly na Chris Smalling.
Arsenal ambayo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 24 itaingia bila ya beki wake wa upande wa kulia, Hector Bellerin aliye majeruhi na kiungo Santi Cazorla.
Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya mchezo huu, je wajua kwamba?
  1. Manchester United wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya mechi kumi za hivi karibuni walizocheza dhidi ya Arsenal. Hiyo ilikuwa mwezi October 2015 ambapo United walipoteza 3-0 kwenye uwanja wa Emirate.
  1. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho hajawai kupoteza mchezo dhidi ya Arsenal kwenye mechi za ligi kuu nchini England. Ameshinda mechi tano na kutoka sare mara sita.
  1. Mechi ya Manchester United dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Old Trafford imetoa penati kumi. Kati ya penati hizo sita zimeshindwa kuingia nyavuni.
  1. Mshambuliaji wa Man United, Wyne Rooney ameifunga Arsenal mara kumi na nne kwenye mechi zote za mashindano.

Kauli za Mourinho na Wenger kuelekea mchezo wa Man United vs Arsenal jioni ya leo

azam-v-kageraLigi kuu ya England leo imerejea tena baada ya kupisha wiki ya michezo ya timu za taifa mbalimbali kwa mujibu wa kalenda ta Fifa duniani.
Urejeo wake umekuja na utamu wa aina yake pale jioni ya leo saa 9.45 utakaposhuhudiwa mchezo mkali kati ya Manchester United na Arsenal, mchezo utakaofanyika Old Trafford.
Mchezo unavuta hisia kali kutokana na uhasama uliopo kwa makocha wa timu hizi mbili, Jose Mourinho kwa upande wa Manchester United na Arsene Wenger kwa upande wa Arsenal.
Kuelekea mchezo huo, makocha wa timu zote mbili wamekuwa na maneno ya kusema huku kila mmoja akizungumza kwa maono yake juu ya mchezo huo.
kwa kuanza na meneja wa Manchester United Jose Mourinho, yeye anasema: “Rekodi yangu dhidi ya mameneja wa timu nyingine sio muhimu sana kwa leo. Kinachopatikana uwanjani inakuwa kwaajili ya timu.
“Mchezo wa leo ni kati ya mameneja wawili wenye rekodi bora kabisa kwenye Premier League. Sir Alex Ferguson hayupo hapa tena… nina mataji matatu hapa, vivyo hivyo kwa Arsene Wenger.
“Hiyo ina maana kwamba ni muhimu tuheshimiwe, hata pale matokeo yetu yanapokuwa si mazuri?
“Nadhani Wenger ana heshimu kwa ninyi nyote. Sidhani kama mimi ninayo, hasa kwa kuwa taji langu la mwisho la Premier League nimechukua miezi 18 iliyopita na sio miaka 18 iliyopita.”
Kwa upande wake, Arsene Wenger juu ya rekodi yake mbovu juu ya Mourinho: “Unajua, hatukuwa tukipoteza michezo yetu mara zote, tumewafunga lakini vilevile kumekuwa na michezo mingi tuliyomaliza kwa kutoshana nguvu.
“Nadhani nimepata ushindi dhidi ya meneja yeyote duniani katika kipindi cha miaka 20 niliyodumu hapa na sipo ktika mchezo huu kufanya ushindani kati ya mameneja wawili.
“Ni kati ya vilabu viwili na timu hizi mbili na nadhani naweza kuelewa kwamba watu wanataka kuleta utata, lakini hiyo si namna ya kuvuta hadhira. Kitakachovuta hadhira ni mvuto na ubora wa mchezo wenyewe.

Didier Drogba ni hatareee hebu angalia Top 10 ya ma-star wa soka wanaomiliki mijengo ghali zaidi duniani

HOME OF DAVID AND VICTORIA BECKHAM IN SAWFORDSBRIDGE, HERTS. PREPARATIONS AND MARQUEES FOR PARTY TO BE HELD TOMORROW BEFORE ENGLAND FOOTBALL TEAM LEAVE FOR THE WORLD CUP. 11-5-02 PIC BY IAN MCILGORM
Kwa hakika mchezo wa soka unawalipa sana wanachezaji na hiyo imewafanya wengine kumiliki mijengo ya maana pengine sawa na matajiri wengine wakubwa duniani.
Hapa tunaangalia mijengo 10 ya wachezaji ya gharama zaidi na hapo utagundua baadhi yao tayari wameshastaafu lakini wamejumuishwa kukupa wewe taswira halisi namna ambavyo mchezo huu ulivyowawezesha wachezaji hao kupata makazi bora ya kuishi.
10. Kaka- $3 Million

kaka-house

9. Andres Iniesta: $4.6 million

iniesta-house

8. Lionel Messi- $5 million

messi-houses

7. Mario Balotelli: $5 million.

baloteli-house

6. Cristiano Ronaldo: $6 million.

ronaldo-house

5. Frank Lampard: $7 million.

lampard-house

4. John Terry: $7.5 million.

terry-house

3. Wayne Rooney: $17.83 million.

rooney-house

2. David Beckham: $20 million.

beckham-house

1. Didier Drogba- $21million
drogba-house

MCHEZAJI LANGA LESSE BERCY WA JAMHURI YA CONGO

tanzania football federation
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, mwaka huu  lilimkatia rufaa mchezaji Langa-Lesse Bercy katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo, Langa Lesse Bercy, CAF liliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko Cairo, Misri  kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).
TFF iliagizwa na CAF igharimie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake  pamoja na kulipia gharama za vipimo. TFF ilikubaliana na matakwa hayo ya CAF na kulipia.
Kipimo ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili  kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.
Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko "vitani",eneo hilo halikutajwa.
TFF inaendelea kufuatia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .

Kadhalika Aidha TFF inaomba wadau wa mpira wa miguu wawe na subira katika kipindi hiki.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif