Monday, November 14, 2016

Cleveland Hawakamatiki ni shidaaa


cleveland-cavs_96lhgpxyii5j13cyjb0quoo5f
LeBron James hakumuhitaji Kevin Love au Kyrie Irving ili kumaliza mchezo dhidi ya Charlotte Hornets na hii hutokea kwa vilabu vichache ambavyo wachezaji wake wanaaminiana.
James,alikuwa ndiye mchezaji pekee wa kikosi cha kwanza katika robo ya nne ya mchezo huo, akafunga pointi 11 kati ya pointi zake 19 katika kipindi cha mwisho na kuisadia Cavaliers kuibuka na ushindi wa pointi 100-93 dhidi ya Charlotte Hornets.
Channing Frye akafunga pointi 20 ambazo ni nyingi zaidi kwake msimu huu huku pia akicheza dakika zote za robo ya nne akiwa pamoja na James, Iman Shumpert, Richard Jefferson na Jordan McRae.
Kyrie Irving aliongeza pointi 19 huku Kevin Love akiendelea kuwa na kiwango bora na alimaliza mchezo akiwa na pointi 17, katika mchezo ambao alikosekana J.R. Smith, kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.
Cleveland Cavalierswameweka rekodi ya kupata walau mitupo 10 ya pointi 3 katika michezo 9 ya kwanza ya msimu.
Kemba Walker alifunga pointi 21 kwa upande wa Hornets, ambao wamepoteza michezo miwili mfululizo baada ya kuanza ligi vyema kwa rekodi ya 6-1.

Cazorla ampa mbwa wake jina la mchezaji wa Manchester


screen-shot-2016-11-14-at-10-56-29-amKupitia channel ya Youtube ya Arsenal, kuna video mbalimbali zinawekwa zikionyesha maisha
ya wachezaji wa Arsenal. Kwenye moja ya kipengele cha channel hiyo inamuonyesha mchezaji
Santi Cazorla akijibu maswali ya haraka ambayo wameita “Rapid Fire” aliulizwa majina ya mbwa wake ambapo mmoja kati ya hao mbwa anamwita Zlatan.
Kwenye moja ya maswali aliulizwa kwamba anamchagua Ronaldo wa sasa au De Lima, Cazorla alijibu De Lima ni striker bora kutokea kwenye maisha ya soka aliyoshuhudia. Kwa upande wa movue Cazorla alisema kwamba Loed of Rings ndio movie bora kwake.
Kumpa jina la Zlatan mbwa wake kwake yeye ni moja ya njia za kuonyesha jinsi gani anamkubali mchezaji huyo ambaye anacheza timu yake pinza kwenye ligi ya England.
Hii hapa ni video kamili….

Sanchez aingia mazoezini na “Bandage”




screen-shot-2016-11-14-at-11-20-18-am
Moja ya story kubwa weekend hii ni mvutano kati ya Arsene Wenger na kocha wa timu ya taifa ya Chile kuhusu mchezaji Alex Sanchez. Kama ilikupita ni kwamba upande wa Wenger anataka mchezaji huyo apumzishwe ili aweze kupona vizuri lakini kocha Chile ameamua kumtumia kwenye mechi ya timu ya taifa.
Wenger alifikia point ya kusema kwenye chombo cha habari kwamba future ya mchezaji huyo ni muhimu kwa pande zote mbili. Hivyo basi aachwe apone vizuri ndio acheze. Lakini kocha wa Chile alimuacha apumzike kwenye mechi moja na anataraji kumtumia kwenye mechi ya Jumanne.
Kwmeye moja ya mazoezi kuelekea mechi ya Chile, Sachez ameonekana akifannya mazoezi na bandage kwenye upaja kitu ambacho kinaonyesha bado kuna vitu anatakiwa apone kabla hajaanza mazoezi hayo au mechi kabisa.
Kwenye moja ya maneno ya Wenger alisema,“Kuna utengano kati ya timu ya taifa na club, wanataka matokeo kwenye mechi yao kitu ambacho naelewa. Lakini kujali afya ya mchezaji ni muhimu zaidi. Sanchez siku zote huwa anataka kucheza hata kama hayupo sawa”
screen-shot-2016-11-14-at-11-19-59-am


Olivier Giroud ana njia mbili za kutoka

Frenchman Olivier Giroud ni chaguo la pili la kocha Arsene Wenger ambae mara nyingi huchagua kumtumia Sanchez kama central striker. Ripoti moya kuelekea January ni kwamba Giroud kama anataka kuwa kwenye kikosi cha kwanza ana option mbili ya kwenda Napoli au Ac Milan.
Giroud ameanza kwenye kikosi cha kwanza mara moja kwenye north london derby lakini mechi nyingine zote ameanzia benchi. Sasa amevunja ukimya na kukubali kwamba huu msimu umeanza vibaya kwake tangu ahamie England mwaka 2012.
Giroud alisema,“Nikikaa kwenye benchi naicheki Arsenal inacheza vizuri bila mimi maana yake treni inaenda vizuri bila mimi. Sasa sitaki iniache mbali sana. Hali ikiendelea hivi itanileta athari hapo baadae, siwezi kucheza mechi moja kati ya tano”.
Pia inasemekana Giroud hakupenda alivyoachwa kwenye kikosi cha mechi ya Champions League kwenye mechi dhidi ya PSG.

DALILI ZA DEPAY KUMKIMBIA JOSE MOURIHNO UNITED

Dalili ziko wazi Depay kusepa Manchester United.


screen-shot-2016-11-14-at-10-17-04-amJuzi nilikupa habari kuhusu kocha wa Everton kuonyesha uhutaji wake wa service ya Memphis Depay kwenye kikosi chake. Depay sasa hivi amekua anahusishwa sana na Everton hadi club yenyewe imeanza kumzunguzia kwenye social media pages zao.
Depay amefunga goli kwenye mechi za kutafuta nafasi ya kucheza kombe la dunia dhidi ya Luxembourg jumapili na Everton hawakuona hatari kumtaja mchezaji huyo kwenye twitter page yao.
Kwa njia yoyote ile kwa sasa hivi Depay hawahusu Everton na hawatajihusisha na kumtaja kwenye page zao. Sasa kutajwa huko kwamba amefunga goli ndiko kumechochea na kukamilisha kila dalili kwamba Depay anaweza kujiunga nao ikifika January.
screen-shot-2016-11-14-at-10-16-39-am
Mchezaji huyu mwenye miaka 22 amepata nafasi chache sana za kucheza Manchester united. Nyingi anaingia kwa sub na umri wake bado anahitaji kcuhaza sana. Habari zaidi zinasema kwamba Depay ataenda Everton kwa mkopo sio kuuzwa kamili.

WAANDISHI WA HABARI UFARANSA WAWAWEKA TRUMP NA ARSENAL DUUUU


screen-shot-2016-11-14-at-10-32-57-am

Vyombo vikubwa vya habari huko Ufaransa vimeingia kwenye aibu ya muda mfupi kwa kuparamia habari ambazo baadae iliwabidi wazitoe kwenye mitandao yao.
Sio Ufaransa peke yake hata mitandao mikubwa duniani walijikuta waki qoute habari hii. Website kama RMC Sport, Yahoo na gazeti kubwa la michezo nchini Ufaransa L’Equipe waliandika kwenye website na kufuta baadae.
Habari yenyewe ni kwamba Donald Trump ni shabiki mkubwa wa Arsenal lakini hapendezwi na mwenendo wa Arsenal kama mashabiki wengine duniani. Source ya kwanza ya story ni mtandao unaitwa Politica ambao walisema kwamba mwanzo mwa mwezi wa tatu walimfanyia interview Trump kuhusu mapenzi yake na michezo.
Politica wakaandika qoute hii ambayo shabiki yoyote wa Arsenal angeisema hivi hivi,“Mimi ni shabiki namba moja wa Arsenal, mimi ni real Gunner na nategemea sisi tuziabishe club nyingine lakini sisi ndio tunaabishwa. Arsene Wenger anaumiza roho za Gunners wengi duniani na mimi ni mmoja wapo.”
“Huyu jamaa anaendesha club kama vile ni mali yake. Sitaki kuona Manchester inatufunga lakini sasa hata Swansea. Arsenal imekua punching bag kwa kila mtu.”
Hii quote ilisambaa sana mara baada ya Trump kushinda urais, lakini hapo nyuma haikusambaa sana kwasababu hakuna aliyeifatilia.

Warriors waonyesha wanachomaanisha

h
Kuna kila ukweli kuwa klabu ya Golden State Warriors inahofiwa kutokana na wachezaji wake nyota ambao wakiwa katika fomu na viwango vyao haishikiki hasa katika ushambuliaji. Alfajiri ya leo almanusura wachezaji wake bora watatu wapate pointi 30 kila mmoja.
Klay Thompson alifunga pointi 30 huku akibadili matokeo katika nusu ya pili ya mchezo huo, Stephen Curry pia alifunga pointi 30 huku akipata mitupo 5 ya pointi 3s, na Warriors wakaichapa Phoenix Suns iliyokuwa imechangamka 133-120.
Kevin Durant aliongeza pointi 29, rebound 9 na assits 5.
Thompson alipata mitupo 11 kati ya 18 huku pia akipata mitupo 5 ya pointi 3 huku pointi 14 kati ya hizo zikiwa kazifunga katika robo ya 4, huku Draymond Green akimaliza mchhezo na pointi 14, assist 11na rebounds 7.
Eric Bledsoe pamoja na T.J. Warren walifunga pointi 20 kila mmoja kwa upade wa Suns.

THORGAN HAZARD AFUNGUKA KUHUSU CHELSEA KUCHEMSHA KWA LUKAKU, DE BRUYNE


Inaonekana kuwa sasa Chelsea wamekuwa wakijuta katakana na kutowapa nafasi ya kutosha washambuliaji wao wawili wa zamani, Romelu Lukaku na Kevin De Bruyne.
Lukaku sasa ni tegemeo la ufungaji Everton huku De Bruyne akisumbua na kikosi cha Man City chino ya Pep Guardiola.
THORGAN HAZARD
Mshambuliaji, Thorgan Hazard anayekipiga katika kikosi cha Borussia Mönchengladbach ya Ujerumani ameyasema hayo.
“Nina uhakika ni hivyo, watakuwa wanajuta kutokana na kushindwa kuwapa nafasi. Sasa wangekuwa msaada mkubwa kwao,” alisema ambaye pia ni raia wa Ubelgiji kama ilivyo kwa De Bruyne na Lukaku.
Wachezaji hao walishindwa kabisa kupata nafasi katika kikosi cha Chelsea chini ya Jose Mourinho.

HAZARD AWEKA WAZI MAPEMA, ANAAMINI HAWEZA KUVAA VIATU VYA UNAHODHA WA JOHN TERRY



Mshambuliaji nyota wa Chelsea, Eden Hazard amesema asingependa kuwa nahodha wa Chelsea kama ilivyo kwa John Terry.

Hazard amesema hatauweza unahodha kwa kuwa yeye si mtu anayezungumza sana kama ilivyo kwa Terry hasa wakati wa kuhamasisha.

“Sidhani kama nitaweza kama ilivyo kwa Terry, yeye ana uwezo wa kuzungumza. Mimi siwezi kabisa.

“Kawaida yang nimekuwa nikizungumza na miguu yangu uwanjani ifanye kipi ambacho ni sahihi,” alisema.


Hazard aria wa Ubelgiji, amerejea katika kiwango kizuri na sasa anaonekana kuwa tegemeo la uzalishaji na ufungaji mabao katika kikosi cha Chelsea.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif