KWA NYIMBO MPYA NA MATUKIO YOTE YA KIMICHEZO ,SIASA N.K, NENDA YOUTUBE NA UTAFUTE MBEGEZE TV KISHA BONYEZA NENO SUBSCRIBE USPIITWE NA KILA KITU
Chelsea bado wanachechemea kusaini striker namba 9 nafasi ambayo ni lazima wasajili kama Diego Costa ataondoka kama inavyoonekana, japokuwa tayari wamefanya sajili kadhaa ila hii ni lazima kwao.
Alvaro Morata anawindwa na Chelsea, pamoja na kutoanza michezo mingi msimu uliopita lakini alifunga magoli 15 na kuassist 8 na ni kati ya washambuliaji ambao wakipewa nafasi anaweza kucheka na nyavu mara nyingi zaidi lakini dau lake sio la kitoto inabidi uwe na pesa kuanzia £70m.
Andrea Belotti, kwa watu wanaoangalia sana Serie A wataelewa unyama ulioko ndani ya Muitalia huyu,michezo 34 kapasia kamba mara 26 na kuassist mara 7 hii inaonesha kila mchezo amefanya jambo, na kwa uwezo wa Belotti hakika Conte anafaa kumsimamisha namba 9.
Pierre Aubemayang, kati ya wachezaji ambao ukimuelezea ubora wake hutumii nguvu nyingi ni Mgabon huyu, namba hazidanganyi na mabao 31 aliyofunga toka ajiunge na BVB yanAeleza ubora wake na msimu uliopita alikuwa ndio kinara wa mabao katika Bundesliga.
Sergio Kun Aguero, inasemekana City wako tayari kumuuza Aguero ili kuongeza pesa za kumpata Sanchez, msimu uliopita Kun alimaliza akiwa na mabao 20 na assist 3 huku wastani wa kufunga kila baada ya dakika 120 dakika ambazo ni Harry Kane tu mwenye chache zaidi inaonesha jinsi Kun anavyoweza kuziba pengo la Costa.
All in All Chelsea inabidi wajipange haswa maana mastriker hao wote kuwapata ni mbinde kubwa sana kwani kila unayemgusa klabu yake inataka kuanzia £60m na huku Conte analalamika kuhusu bajeti ya usajili iliyopo, kama Chelsea wakishindwa kununua striker ni bora wakae chini na Costa wayamalize.