Saturday, February 20, 2016

WACHEZAJI WA UTD WAMTAK JOSE KINGUMU


Mou
Baada ya Van Gaal kupoteza mchezo wake wa Europa League Alhamisi usiku dhidi ya Midtjylland kocha huyo amejiweka kwenye mazingira magumu ya kuendelea kuwa kocha wa Manchester United.
Kocha huyo tayari amepona kwenye majanga tofauti msimu huu lakini kwa sasa amejiweka kwenye wakati mgumu baada ya vipigo viwili mfululizo.
Lakini wakati huu inaonekana hata wachezaji hawapo nyuma yake tena kutokana na mwenendo wa matokeo mabovu.
Mou 1
Hadi sasa kuna baadhi ya wachezaji hawamuungi mkono Van Gaal, lakini kurasa za magazeti ya England zimetoka na story ambayo inafanana: Kundi muhimu la wachezaji wa United limepoteza imani na kocha huyo raia wa Uholanzi na linamtaka Jose Mourinho kuletwa kwenye timu kumrithi Van Gaal mapema iwezekanavyo.
Kumekuwa na taarifa kwamba, huenda Mourinho akatajwa kuwa kocha wa United baada ya kumalizika kwa msimu huu lakini wachezaji wa kikosi hicho wanamtaka mapema kabla hata ya kumalizika kwa msimu.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif