Tuesday, March 17, 2015

CHEKA HURU URAIANI


Bondia nyota zaidi nchini, Francis Cheka ameachiwa huru.
Cheka ameachiwa huru baada ya kushinda rufaa yake aliyokata kupinga kifungo cha miaka mitatu gerezani.


Tayari Cheka alianza kutumikia kifungo hicho mjini Morogoro.
Lakini taarifa za uhakika zinasema ameachiwa leo baada ya kushinda rufaa hiyo.

“Tayari ameachiwa, lakini tunashughulikia masuala kadhaa kumalizia ishu hiyo. Ila tayari yuko nje,” alisema Kaike Siraju, promota wa ngumi za kulipwa aliyekuwa akipambana kuhakikisha Cheka anatoka.


Cheka alihukumiwa kwenda jela baada ya kumtwanga na kumuumiza meneja wa baa yake mjini Morogoro akimtuhumu kumsababishia hasara.

KAMA YANGA ITAITOA FC PLATNAM ITAKUTANA NA HUYU AU HAWA


BENFICA DE LUANDA
Tayari Yanga ina ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe. Lakini kuna mechi ya pili itakayopigwa kati ya Aprili 3 hadi 5 ndiyo itatoa majibu.

Iwapo Yanga itafuzu, basi itakuwa na kibarua kigumu zaidi katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho kwa kuwa inatarajia kukutana na timu kutoka Tunisia au Angola.
ESS..
Etoile du Sahel (ESS) ya Tunisia au Benfica ya Angola, moja itakayoshinda. Basi ndiyo itakutana na Yanga.

Tayari Etoile wameshinda mechi yao ya kwanza nyumbani kwa bao 1-0 lakini lazima wasubiri pia mechi ya ugenini jijini Luanda.


Iwapo Yanga itavuka, basi inatarajiwa kukutana na moja ya timu hizo katika mechi ya kwanza itakayopigwa kati ya Aprili 17 hadi 19 na marudiano Mei Mosi na Mei 3.

NDUGU WA MARSH WAZUIA MWILI WAKE USIPELEKWE HOSPITAL


HAPA NI BAADA YA MWILI WA MARSH KUAGWA JIJINI DAR....
Mwili wa marehemu Kocha Sylvester Marsh ulizua vurugu kubwa baada ya kuwasili mjini Mwanza.



Baadhi ya ndugu wa marehemu akiwemo dada yake, walilazimisha mwili huo kulala nyumbani hapo wakipinga kutopelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Sekeo Toure.

Ndugu hao walidai mwili ulipaswa kulala hapo, leo uagwe na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya Igoma jijini Mwanza.

Lakini kwa busara ya waombolezaji akiwemo mkuu wa wilaya ya Nyamagama, waliwasihi kwamba ungeweza kuharibika kwa kuwa uliwasili Mwanza baada ya safari ya usiku kucha.

Baadaye wana ndugu hao walilegeza uzi na kukubaliana na waombolezaji na mwili ukapelekwa kuhifadhiwa hospitali.

Leo unaangwa na mazishi yatafanyika katika makaburi ya Igoma jijini Mwanza.

Marsh aliyewahi kuzinoa Taifa Stars, Kili Stars na timu za vijana alifariki dunia Jumamosi iliyopita baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif