Thursday, November 3, 2016

KINNAH:ASANTENI MASHABIKI


IMG_20160727_121624
Siku moja baada ya kuiduwaza Yanga kwa kipigo cha bao 2-1,kocha  mkuu wa Mbeya City fc Kinnah Phiri amejitokeza na kuwapongeza mashabiki wa timu hiyo kwa namna walivyojitokeza kwa wingi na kuishangilia timu yao muda wote  wa mchezo jambo lililoanikiza ushindi huo.

Akizungumza na Ram mbegeze blog  mapema leo Kocha Phiri alisema kuwa  nguvu kubwa ya ushangiliaji iliyokuwa inatoka upande wa jukwaa la mashabiki wa City iliwafanya wachezaji kutambua kuwa wanalo jukumu kubwa la kucheza kwa nguvu na umakini mkubwa kuhakikisha wanapata matokeo ambayo yangekuwa faraja pekee kwa mashabiki wao waliojitopkeza uwanjani kwa wingi.
“Hakika ilikuwa siku nzuri, mashabiki walijitokeza kwa wingi, nguvu  yao ya ushangiliaji ilistua mioyo ya wachezaji wangu wakatambua kuwa wanadeni kubwa la kusherehesha furaha kwa mashabiki wao kwa kufanya jambo moja tu la kucheza kwa nguvu na umakini kuhakikisha wanashinda na kupata pointi tatu kutoka moyoni ninawashukuru sana walifanya kazi kubwa” alisema.
Kuhusu hali ya kikosi na mpango wa kushinda mchezo huo kiufundi, Kocha Phiri alisema kuwa, awali aligundua nguvu kubwa ya Yanga inatoka pembeni ya uwanja huku akianikizwa na viungo wa katikati hivyo alilazimi kubadili mfumo na kikosi kuhakikisha timu hiyo ya Dar es Salaam haipati mwanya wa kupita au kutengeneza nafasi ya kufunga bao.
“Yes!nilifanya maamuzi mengi tofauti hii ni baada ya kuifuatilia Yanga kwenye michezo kadhaa,nilibadilisha kikosi nikabadilisha mfumo,Yanga ni timu nzuri  huwezi kuiweka kwenye kundi la timu ndogo lakini ubora wetu kwenye mchezo wa jana uliwanyima nafasi ya kucheza mchezo wao waliouzoea na kushindwa kuleta hatari langoni kwetu,vijana wangu walicheza kwa namna nilivyowaelekeza ndiyo sababu kila mmoja aliona tumecheza vizuri ” alisema.

MAUAJI YA SOKOINE YAZIDI KUWAPAGAWISHA ZAIDI MASHSBIKI WA CITY


Ushindi walioupata mbeya city jana katika dimba la sokoine umewapagawisha mashabiki wa timu hiyo huku mashabiki wa yanga wakiwa na mawazo tele kwaani wikend hii pia watakuwa na kibarua kigumu sana dhidi ya wajelajela
 
 img-20161102-wa0059


img-20161102-wa0058

img-20161102-wa0055

img-20161102-wa0053

img-20161102-wa0052img-20161102-wa0050img-20161102-wa0049img-20161102-wa0048img-20161102-wa0060

TAZAMA MECHI ZA EUROPA LEAGUE ZINAZOPIGWA LEO


November 3
21:00
Fenerbahce
Manchester United
21:00
Zorya
? - ?
Feyenoord
November 3
19:00
FC Astana
? - ?
Olympiacos
21:00
APOEL Nicosia
? - ?
Young Boys
November 3
21:00
Anderlecht
? - ?
Mainz 05
21:00
FK Qabala
? - ?
Saint-Etienne
November 3
21:00
Maccabi Tel Aviv
? - ?
AZ Alkmaar
21:00
Zenit St. Petersburg
? - ?
Dundalk
November 3
21:00
Astra Giurgiu
? - ?
Viktoria Plzen
21:00
Austria Wien
? - ?
Roma
November 3
21:00
Athletic Bilbao
? - ?
Genk
21:00
Sassuolo
? - ?
Rapid Wien
November 3
23:05
Ajax
? - ?
Celta Vigo
23:05
Panathinaikos
? - ?
Standard Liege
November 3
23:05
Braga
? - ?
Konyaspor
23:05
Gent
? - ?
Shakhtar Donetsk
November 3
23:05
Nice
? - ?
Salzburg
23:05
Schalke 04
? - ?
FC Krasnodar
November 3
23:05
Fiorentina
? - ?
Slovan Liberec
23:05
PAOK Thessaloniki FC
? - ?
Qarabag FK
November 3
23:05
Southampton
? - ?
Inter
23:05
Sparta Prague
? - ?
Hapoel Beer Sheva
November 3
23:05
FC Zuerich
? - ?
Steaua Bucuresti
23:05
Villarreal
? - ?
Osmanlispor FK

TRA ya Hispania yatinga mifukoni mwa Alexis Sanchez.


Walcott & Sanchez
Mshambuliaji wa klabu ya arsenal, Alexis Sanchez anashutumiwa kuhusika na ubadhikifu wa fedha zinazosimamiwa na mamlaka ya kodi ya Hispania inayokadiriwa kuwa kiasi cha Euro Milioni moja (€1 million) kutokana na kile kilichopatikana kwenye haki za sura yake akiwa na klabu ya Barcelona, hii imetajwa na gazeti la Katalunya, El Periodico.
Jarida hilo la kila siku limeripoti kuwa mamlaka ya mashitaka na kesi za jinai imefungua kesi ya madai dhidi ya Sanchez ambaye anadaiwa kukwepa kulipa kodi ya mapato katika kipindi cha miaka 2012 na 2013 kinachokadiriwa kuwa €983,443 (£889,169) ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania 2392779271, bilioni mbili na milioni 400.
El Periodico limesema kuwa Sanchez, ambaye alijiunga na Arsenal katika majira ya joto ya mwaka 2014 baada ya misimu mitatu akiwa Barca, inasemekana alitumia makampuni kutoka Chile na yale ya Malta kusimamia upatikanaji wa fedha zake za mauzo ya sura yake.
Ripoti ya jarida hilo inasema kuwa mchezaji huyo raia wa Chile anadaiwa kufanya ubadhilifu wa kiasi cha fedha za kitanzania bilioni moja na milioni mia tano, 1581455655 (€587,677) mwaka 2012 na bilioni moja na milioni 60, 1065017652 (€395,766) mwaka 2013.
Kama ikithibitishwa, Sanchez mwenye miaka  29 atakuwa mchezaji wa tano kutoka katika vitabu vya klabu ya Barcelona kuhusishwa na tatizo la fedha  na mamlaka za mapato  katika mahakama za Hispania.
Mapema mwaka huu, nyota wa Barcelona Lionel Messi alikutwa na hatia kwa makosa matatu ya ubadhilifu fedha na mahakama za nchini humo. Messi alipiwa faini pamoja na adhabu ya kifungo cha miezi 21 jela.
Alexis Sanchez aliichezea Barcelona katika kipindi cha miaka ya 2011 na 2014.
Mchezaji mwenzie na Messi katika klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Javier Mascherano alikutwa pia na hatia ya mauzo ya haki za sura yake na akahukumiwa pia kulipa faini na kifungo cha mwaka mmoja.
Nyota wa zamani wa Cameroon Samuel Eto’o, aliyeichezea Barca kuanzia mwaka 2004 na 2009 ambaye kwa sasa yupo na klabu ya Uturuki, Antalyaspor, na pia raia wa Brazil beki Adriano wote wamewahi kukutwa na kesi za ukwepaji kodi nchini Hispania.

Ndugu wa Mohamed Bin Hammam naye kwenda jela ya FIFA.


mohamed-bin-hammam-620
Na Ram Mbegeze

Kamati ya maadili na sheria ya FIFA imetuma maombi ya kutaka aliyekuwa msaidizi wa Mohamed bin Hammam afungiwe kifungo cha maisha kujihusisha na soka kutokana na uchunguzi wa rushwa kwenye soka unaomhusu.

Kamati hiyo ya maadili ya  FIFA imesema hayo jana Jumatano kuwa uchunguzi wake kwa Najeeb Chirakal “ulilenga malipo yaliyofanywa kwa watendaji kadhaa wa soka duniani.”

Pia ilipendekeza kuwa majaji wa maadili na sheria wa FIFA kuweka sheria mpya ya kifungo cha maisha kwa kesi zote zinazohusu hongo na rushwa, ahadi za zawadi, migongano ya kimaslahi na kushindwa kwa maafisa kutoa ushirikiano kwa wachunguzi.

Chirakal aliishi sana nchini Qatar na alikuwa mfanyakazi wa Bin Hammam, moja ya watendaji wenye nguvu waliowahi kuwepo ndani ya FIFA na Rais wa chama cha soka cha bara la Asia ambaye alipewa kifungo cha maisha na FIFA mwaka 2012.
Bado haijawekwa wazi ni lini kamati ya majaji ya FIFA itakutana kutoa maamuzi ya kesi hii lakini mara nyingi huchukua wiki kadhaa.

Chirakal aligundulika hapo nyuma kupitia machapisho ya jarida la Uingereza,The Sunday Times na ripoti ya Pricewaterhouse Coopers kuhusiana na taarifa za kifedha za chama cha soka cha bara la Asia ikiwa ni ya mahusiano ya watendaji wa bara la Afrika na Asia kuhitaji fedha kutoka kwa Bin Hammam.

Mwezi Oktoba 2012, Chirakal alisimamishwa kupisha uchunguzi na mahakama ya maadili ya FIFA kutokana na kushindwa kutoa ushirikiano kuhusiana na sakata la Bin Hammam.
Akiwa kama msaidizi wa Bin Hammam aliombwa kutoa taarifa rasmi na nyaraka lakini akashindwa kufanya hivyo.

Kamati ya maadili ya FIFA ilimwondoa Bin Hammam kwa mara ya pili mwezi Desemba 2012 kutokana na usimamizi mbovu wa kifedha wa chama cha soka Asia (AFC), ambayo ilitoka katika taarifa iliyovujishwa ya ukaguzi wa mahesabu iliyofanywa na shirika la uhasibu linalofahamika kama PwC.

Ripoti hiyo ilimhusisha Chirakal na washirika wengine wa Rais huyo waliokuwa kwenye mlolongo wa kujihusisha na viongozi wa vyama vya soka barani kama Amadou Diallo, waliokuwa wakiomba fedha kutoka kwa Bin Hammam, ambaye alikuwa anatumia utajiri wake binafsi kuhonga. Diallo alihusishwa na kashfa ya mwaka 2011 kutokana na kupata fedha zisizo halali katika kampeni iliyofanikiwa ya Qatar kupata uenyeji wa kombe la dunia mwaka 2022.

Bin Hammam alifungiwa mara ya kwanza na FIFA mwaka 2011 kutokana na malipo yasiyokuwa halali kwa wapiga kura kutoka Caribbean wakati anagombea urais wa FIFA dhidi ya Sepp Blatter. Kifungo hicho cha maisha kilifutwa na mahakama ya masuala ya kimichezo.

HILI NI SOMO

Kuna kila sababu ya wachezaji  wa kitanzania kujifunza kwa kichuya ambae toka akiwa mtibwa amekuwa na kiwango kilekile hakijashuka
tunakumbuka hata katika mashindano ya mapinduzi pale zanibar alifanya vema sana
tofauti na wachezaji wengine ambapo pengine wangemaliza viwango vyao

ushauri:sasahivi kichuya anatakiwa kujituma zaidi na aamini kuwa bado hajafika na atafika mabali zaidi,asijerizika mapema,starehe za marara kwa mara kama akifanya hivyo tutamshuhudia ktk anga zingine

KIPIGO CHA JANA, MBEYA CITY WAIPA YANGA MTIHANI MWINGINE MBEYA



Ushindi wa mabao 2-1 walioupata Mbeya City dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, jana unakuwa mtihani mwingine kwa Yanga.

Yanga wanaingia kwenye mtihani huo kutokana na mechi inayofuatia dhidi ya Prisons ambao wanakutana nao Jumamosi.

Prisons ambao wanashindana kwa juhudi zote na Mbeya City, hawatakubali kuona wao wanaishindwa Yanga kwa mambo mawili.

Kwanza ni kwa ajili ushindani wao mkali dhidi ya Mbeya City ambao wamewaonyesha wamewaweza Yanga, vipi wao washindwe?

Pili wanachuana na Mbeya City kwa pointi, Prisons sasa wana 16 na wasingependa kuzidiwa zaidi kwa kuwa sasa tayari Mbeya City wana 19.

Kufanikisha yote haya, lazima Prisons washinde ili kuwakimbiza wapinzani wao Mbeya City, pia kuwaonyesha hakuna wanachoshindwa pia.

.

LEGIA NI VIBONDE LAKINI WAPATA POINTI YAO YA KWANZA LIGI YA MABINGWA KWA KUIZUIA MADRID KWA SARE YA 3-3



Legia Warsaw: Malarz, Bereszynski, Rzezniczak, Pazdan, Hlousek, Kopczynski, Moulin, Guilherme, Odjidja (Jodlowiec 87), Radovic (Prijovic 77), Nikolic (Kucharczyk 69)
Subs not used: Cierzniak, Jodlowiec, Czerwinski, Hamalainen, Broz

Real Madrid: Navas, Carvajal, Nacho, Varane, Fabio Coentrao (Asensio 77), Bale, Kovacic, Kroos, Ronaldo, Morata (Diaz 85), Benzema (Vazquez 65)
Subs not used: Casilla, Isco, Danilo, Tejero
Referee: Pavel Kralovec






EUROPA CUP...MAZOEZI YA MWISHO YA MAN UNITED KABLA YA KUIVAA FENERBAHCE YA ROBON VAN PARSIE


MECHI TANO ZIJAZO ZA MAN UNITED
Oct 17: Liverpool (a, PL) DREW 0-0 
Oct 20: Fenerbahce (h, EL) WON 4-1
Oct 23: Chelsea (a, PL) LOST 4-0
Oct 26: Man City (h, EFLC) WON 1-0
Oct 29: Burnley (h, PL) DREW 0-0 










'JEZI' MPYA ARSENAL ZAWACHANGANYA MASHABIKI, WENGI WALALAMIKA SI JEZI NZURI



Sweta walizovaa wachezaji wa Arsenal wakiwa kwenye picha ya kikosi, zimezua mjadala mkubwa hasa kwa mashabiki wao barani Asia.

Wengi hawakuelewa kuhusiana na sweta hizo, hasa baada ya wachezaji wa Arsenal kuonekana wakiwa na Kocha wao, Arsene Wenger wakiwa wametupia sweta hizo.

Wengi waliamini ni jezi mpya na kuanzisha mjadala mpana mtandaoni wakipinga lakini Arsenal kitengo kinachoshughulika na masuala ya masoko barani Asia, kimefafanua.


Kwamba hizo ni sweta maalum kwa ajili ya sikukuu na lengo ni ksuaidia watoto wenye matatizo baada ya mauzo yake.

SIMBA WANOGEWA NA USHINDI, WATAKA PONTI SITA ZA LYON, PRISONS



Baada ya kuitwanga Stand United iliyokuwa haijawahi kufungwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga msimu huu, Simba imenogewa na pointi.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema wanataka kumalizia mechi mbili zilizobaki za mzunguko wa kwanza kwa ushindi pia.
“Kwanza nikuambie ligi bado ni ngumu, lakini tunapenda kushinda mechi mbili za African Lyon na Prisons. Halafu tutaanza kujipanga kwa mzunguko wa pili,” alisema.
Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 35 kileleni, tofauti ya pointi nane na Yanga wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 27.
MECHI ZA SIMBA ZA MZUNGUKO WA KWANZA:
NOV 6     Vs African Lyon
NOV 9      Vs Prisons 

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif