Thursday, March 16, 2017

Tetesi za usajili magazeti ya Ulaya leo


Mtandao wa michezo wa Italia ujulikanao kama Tuttomercatto umeripoti kwamba, bosi wa Chelsea
anamuangalia kiungo wa Napoli Kalidou Koulibaly kama usajili wake wa kwanza katika dirisha lijalo la usajili. Conte amekuwa akimuwinda Msenegal huyo toka akiwa anaifundisha Juventus lakini sasa amemkazia buti na anataka kumchukua. Koulibaly ambae alisajiliwa na Napoli kutoka timu anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta timu ya Fc Genk, amekuwa na msimu mzuri sana toka awasili Napoli.
Tukibaki hapohapo katika klabu ya Chelsea, gazeti la Mirror linasema Chelsea wanajipanga kumchukua Romelo Lukaku kutoka Chelsea kwa dau kubwa sana. Lukaku ambaye amekataa kusaini mkataba mpya tena mnono na Everton ameanza kuwindwa na timu mbalimbali lakini Chelsea wanaonekana wako serious zaidi. Lukaku ambaye alikuwa Chelsea hapo mwanzo amekuwa na msimu mzuri sana safari hii na Chelsea wako tayari kuvunja account zao ili kumrudisha.
Sun nalo likiongelea usajili wa Lukaku kwenda Chelsea linasema, Chelsea wako tayari kumuuza Diego Costa ile endapo tu watafanikiwa kupata sahihi ya Lukaku na Alvaro Morata. Chelsea hawana uhakika wa kumbakisha Diego Costa msimu ujao, na kumekuwa na tetesi kwamba Costa anaweza kutimkia China au kurudi katika timu yake ya zamani ya Athletico Madrid.
Lakini vile vile kocha wa Liverpool Jurgen Klopp yuko katika mbio za kumchukua mshambuliaji kinda wa RB Leipzig Timo Werner. Werner mwenye miaka 21 msimu huu amekuwa wa moto sana kiasi cha kuwatishia washambuliaji wa Bundesliga. Klopp anahitaji mshambuliaji mwingine wa kati na anamuona Werner kama mtu sahihi kwa Liverpool.
Neymar na Messi watofautiana kuhusu usajili, Neymar ni rafiki wa karibu sana wa Phillipe Coutinho na sasa Neymar amewaomba Barca wamnunue Coutinho toka Liverpool. Lakini Messi ni kama hataki Coutinho aje Barcelona. Messi anaona kama Coutinho akija Barcelona baasi itaharibu pacha yake ya ushambuliaji kati yake na Luis Suarez

Leicester na Man United kuziumiza Liverpool na Arsenal.

Leicester City wamefudhu katika hatua ijayo ya Champions League ambayo ni robo fainali baada ya kuitupa nje Sevilla, hakuna aliyetarajia Leicester wanaweza kufika hapa walipo kutokana na kiwango walichonacho msimu huu. Msimu huu Leicester wako na mwendo usioeleweka kwani wanahangaika kupigania kubaki katika ligi kuu Uingereza, lakini toka kocha aliyewapa ubingwa wa Uingereza Claudio Ranieri atimuliwe, Leicester wanaonekana kurudi na makali mapyaa.

United nao katika mashindano ya Europa walipata suluhu ya moja kwa moja dhidi ya Rostov katika pambano lililopita, United watawakaribisha Rostov wiki hii wakiwa na faida ya goli la ugenini. Manchester United wanapewa nafasi kubwa kuchukua kombe la Europa katika msimu huu.
Sasa baasi katika timu nne za juu ligi ya Uingereza, Manchester United na Leicester hawapo.Chelsea anaongoza ligi, Totenham nafasi ya pili,Man City ya tatu na Liverpool ya nne na Arsenal ya tano. Katika Champions League timu tatu za juu ndizo zinafudhu moja kwa moja kushiriki Champions League lakini ligi moja inaweza kutoa timu tano.

Kama Leicester watabeba kombe la Champions League(bado mechi 4 kwa fainali) na United wakabeba Europa baasi aliyeko nafasi ya nne itabidi wampishe bingwa wa Europa, huku bingwa wa Champions League akienda kama bingwa mtetezi.

Hakuna aliyewaza kama Leicester wanaweza kuwa mabingwa wa Uingereza, vivyo hivyo watu wanawaza hawawezi kuwa mabingwa wa UEFA lakini wanaweza fanya lolote. Njia pekee ya Arsenal na Liverpool kujiweka mahali salama ili kucheza Champions League msimu ujao ni kumaliza ligi katika nafasi tatu za juu.

Ahmad kampiga-chini Hayatou urais wa CAF

Rais wa chama cha soka cha Madagascar Ahmad Ahmad ameushtua ulimwengu wa soka baada ya kumbwaga Issa Hayatou ambaye alikuwa rais wa muda mrefu wa shirikisho la soka Afrika na kushinda urais wa Caf leo March 16, 2017.
Uchaguzi uliomalizika Addis Ababa umempa ushindi Ahmad Ahmad baada ya kupata kura 30 dhidi ya 20 za Issa Hayatou.
Matokeo hayo yanahitimisha miaka 29 ya utawala wa Hayatou kama kiongozi wa juu wa soka la Afrika.
Mipango na mbinu kabla ya uchaguzi zimepelea kuwashangaza wengi baada ya kushuhudia kambi ya Hayatou ikidondoshwa.
Hayatou mwenye miaka 70 sasa, alikuwa rais wa CAF tangu mwaka 1988 wakati huo Lionel Messi akiwa na miezi tisa tu tangu azaliwe wakati mtawala huyo mzaliwa wa Cameroon alipotangazwa kusimamia soka la bara la Afrika.
Alianza kutawala tangu March 10, 1988 alikuwa anaifukuzia rekodi ya kuendelea kusalia madarakani kwa awamu ya nane mfululizo.
Uchaguzi ulifanyika leo baada ya mkutano mkuu wa 39 huko mjini Addis Ababa.
Ahmad anakuwa rais wa saba wa CAF kwenye historia ya shirikisho hilo lenye miaka 60 hadi sasa tangu kuanzishwa kwakwe.
Aliingia madarakani akiwa rais wa chama cha soka cha Madagascar mwaka 2003 na sasa amefanikiwa kuwa rais wa CAF kwa miaka minne ya kwanza, ameahidi kuboresha shirikisho hilo na kuwa la kisasa ili kuendana na wakati huku akisema atahakikisha kunakuwa na uwazi wa hali ya juu.
Hayatou aliwahi kupata upinzani mkubwa mara mbili kabla ya sasa lakini mara zote alishinda kwa kishindo, lakini safari ameishia kupata kura 20 ambazo zimemaliza matumaini yake ya kutawala kwa zaidi ya miongo mitatu.

Hizi ni taarifa njema kwa soka la Zanzibar




Hatimaye mkutano mkuu wa 39 wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) unaoendelea mjini Addis-Ababa, Ethiopia, umepitisha ombi la chama cha soka Zanzibar (ZFA) kuwa mwanachama rasmi wa CAF.
Ni jambo la kihistoria kwa Zanzibar kwani safari hii ombi lao limepitishwa bila kupingwa na inakuwa nchi ya 55 mwanachama wa kujitemea wa CAF.

Awali Zanzibar ilikuwa inaunganishwa na Tanzania bara chini ya TFF na kupelekea kukosa haki za kushiriki kama nchi kwenye mashindano yanayoandaliwa na CAF pamoja na yale ya FIFA.
Pendekezo hilo lilipelekwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndugu, Jamal Malinzi na lilipokelewa na wajumbe 54 wengine waliokuwepo.

Hii maana yake ni kuwa kwa sasa CAF ndio shirikisho mwanachama wa FIFA kwa upande wa mabara lenye wanachama wengi zaidi kuliko wote.
Vilabu vya Zanzibar vimekuwa vikishiriki mashindano mbalimbali ya CAF lakini kwa ngazi ya kitaifa hawakuwa na ruhusa na walicheza kwa kuungana na Tanzania bara na kushiriki kama Tanzania.
Kwa maana hiyo basi, chama cha soka cha Zanzibar kitapata uwezeshaji wa kifedha moja kwa moja kutoka CAF na FIFA kwa ajili ya timu ya taifa.



-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif