Sunday, April 23, 2017

BREAKING NEWS: TFF YATANGAZA KUIPOKA SIMBA POINTI TATU, YAZIRUDISHA KWA KAGERA SUGAR



Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza kuipoka Simba pointi tatu na mabao matatu ambazo ilipewa kutokana na mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.

Wiki mbili zilizopita Simba ilipoteza mchezo dhidi ya Kagera kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kagera mkoani Kagera katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara lakini baadaye ilikata rufaa ikipinga Kagera kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi ikidai alikuwa na kadi tatu za njano, ndipo ikapewa ushindi huo kupitia Kamati ya Saa 71.

Mara baada ya kamati hiyo kuipa Simba pointi Kagera ikaomba kupitiwa upya kwa suala hilo na nsipo TFF ikatangaza kuwa suala hilo sasa litakuwa chini ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo ndiyo imetoa maamuzi hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi huo, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kuwa kuna sababu kadhaa zimechangia kuchukuliwa kwa maamuzi hayo ambapo alisitaja kuwa ni:

“Malalamiko ya Simba hayakuwasilishwa kwa wakati muafaka tangu mchezo ulipochezwa, malalamiko yao hayakuwa katika njia ya maandishi, rufaa ya Simba haikulipiwa ada, kikao cha Kamati ya Saa 72 kilikosa uhalali kutokana na kuwashirikisha watu ambao hawana uhalali wa kuwa kwenye kikao.

“Kutokana na sababu hizo kamati imeamua kufuta maamuzi yaliyochukuliwa na Kamati ya Saa 72 na kurejesha matokeo kama yalivyokuwa, pia kamati imemuagiza katibu mkuu wa TFF kuwapeweleka baadhi ya wajumbe wa bodi ya ligi katika Kamati ya Maadili ya TFF kwa kosa la kwenda kinyume na kazi zao,” alisema Mwesigwa.

HAFLA YA KUCHANGIA SERENGETI BOYS KUFANYIKA IJUMAA




Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeandaa hafla maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya timu ya Serengeti Boys inayojiandaa kucheza fainali za kuwania Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Gabon. Fainali hizi zitafanyika kufanyika kuanzia Mei 14 hadi 28, 2017.
TFF inatambua kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakichangia timu hiyo kupitia mitandao ya simu kama vile namba 0687 333 222 kadhalika Selcom kwa namba 22 33 44 pia kuweka fedha kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki ya Diamond Trust (DTB).
Sasa siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017 TFF imeandaa hafla maalumu ya kupokea michango hiyo, lakini pia kuchangisha fedha zaidi maana lengo ni kukusanya shilingi bilioni moja (Sh. 1 Bil.) Hafla hiyo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.
TFF imeamua kutumia fursa kuwakaribisha wawakilishi wa makundi mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni rasmi.
Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook hivyo TFF inaomba wawakilishi wa makundi yote ya mitandao ya jamii (admins) ambao wamekusanya michango hii wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi michango ya makundi yao kwa mgeni rasmi katika hafla hii.
Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma email kwenda fdf@tff.or.tz, kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787 176767 ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp.
Aidha wawakilishi wa makundi mengine kama idara za Serikali, mashirika ya umma na binafsi kadhalika watu binafsi ambao nao wamechangia nao pia tunaomba wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi michango yao siku hiyo ya Ijumaa.

MKENYA MARY AWEKA REKODI MPYA LONDON MARATHONI, AZOA MAMILIONI





Hii ni mara ya tatu Mary kushinda London Marathon na kikubwa leo ameweka rekodi ya kukimbia kwa muda wa 2:17:01 ambayo ni rekodi mpya ya dunia.

Kutokana na ushindi huo, Mary anaondoka na kitita cha cola 125,000 (Sh milioni 273), kinachojumuisha uvunjani wake wa rekodi hiyo.


Zawadi ya kawaida ya mshindi hula ni dola 55,000, lakini day huongezeka katakana ana kuvunja rekodi.

Tirunesh Dibaba wa Ethiopia alifukuzana vikali na Mary katika dakika za mwisho hata hivyo Mkenya huyo alionyesha ni bora zaidi alipofanikiwa kuibuka na ushindi huo.

MKENYA MARY AWEKA REKODI MPYA LONDON MARATHONI, AZOA MAMILIONI





Hii ni mara ya tatu Mary kushinda London Marathon na kikubwa leo ameweka rekodi ya kukimbia kwa muda wa 2:17:01 ambayo ni rekodi mpya ya dunia.

Kutokana na ushindi huo, Mary anaondoka na kitita cha cola 125,000 (Sh milioni 273), kinachojumuisha uvunjani wake wa rekodi hiyo.


Zawadi ya kawaida ya mshindi hula ni dola 55,000, lakini day huongezeka katakana ana kuvunja rekodi.

Tirunesh Dibaba wa Ethiopia alifukuzana vikali na Mary katika dakika za mwisho hata hivyo Mkenya huyo alionyesha ni bora zaidi alipofanikiwa kuibuka na ushindi huo.

SIMBU AJITAHIDI, ASHIKA NAFASI YA TANO LONDON MARATHON, ABEBA MAMILIONI YAKE



Wakati Mkenya Daniel Wanjiru ameshinda mbio za London Marathon, Mtanzania Alphonce Simbu ameshika nafasi ya tano.

Wanjiru aria wa Kenya ameshinda kwa muda wa saa 2, dakika 5 na sekunde 48 na Simbu ametumia saa 2, dakika 9 na sekunde 9 na kushika nafasi hiyo ya tano.
Inaonyesha anayeshika nafasi ya tano katika mashindano hayo anaibuka na kitita cha dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 22).
Hata hivyo, Simbu ambaye alianza vibaya alilazimika kubadili gia mwishoni na kuwashinda zaidi ya Wakenya sita na Waethiopia wawili, Mganda mmoja ili kushika nafasi hiyo ya tano.
Nafasi ya pili imekwenda kwa Kenenisa Bekele wa Ethiopia ambaye mwishoni alichuana vikali na Wanjiru aliyeonekana kuwa katika kiwango bora.

BREAKING NEWS: TFF YAMFUNGIA HAJI MANARA MIEZI 12, APIGWA FAINI YA SH MILIONI 9





Kamati ya Nidhamu ya TFF, imetangaza kumfungia miezi 12 Msemaji wa Simba, Haji Manara.


Pamoja na kufungiwa mwaka mmoja, Manara amepigwa faini ya Sh milioni 9.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Wakili Jerome Msemwa amesema Manara amefungiwa miezi 12 kutokana na utovu wa nidhamu.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi punde, Msemwa amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini Manara amefanya utovu mkubwa wa nidhamu.

BREAKING NEWS: KOMBE LA SHIRIKISHO, SIMBA VS AZAM, MBAO FC VS YANGA





Droo ya Kombe la Shirikisho imekamilika na sasa Simba na Azam FC zitakutana katika nusu fainali ya kwanza.

Mbao FC watakuwa wenyeji wa Yanga katika nusu fainali ya pili.


Nusu fainali ya kwanza itakayowakutanisha Simba na Azam FC itachezwa Aprili 29 na ile ya pili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza itachezwa Aprili 30.

Simba imesitisha maandamano ya amani


Klabu ya Simba inapenda kuwajulisha wanachama na wapenzi wake kuwa imesitisha maandamano iliyopanga kuyafanya Jumanne wiki ijayo 25.04.2017, baada ya nia na dhamira njema ya serikali kutaka kushughulikia sintofahamu inayoendelea baina ya klabu na Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Ikumbukwe jana klabu yetu, ililiandikia barua Jeshi la Polisi nchini ikiomba kibali cha kufanya maandamano ya amani, yaliyopangwa kuhudhuriwa na viongozi, wanachama na washabiki wa klabu yetu kwenda Wizara inayosimamia Michezo nchini, yakiwa na lengo la kupeleka kilio chetu juu ya namna TFF inavyoshughulikia malalamiko ya muda mrefu na ya sasa ya klabu hii kubwa nchini.
Katika barua iliyoandikwa na katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja kwa niaba ya Serikali, imetutaka Shirikisho na Klabu kutafuta namna sahihi na iliyo na weledi katika kushughulikia changamoto hizi zinazoweza kuvuruga amani ya nchi.
Serikali kupitia barua hiyo, imeahidi pia kutukutanisha pande zote haraka iwezekanavyo, ili kwa pamoja tumalize sintofahamu hii kwa maslahi ya mchezo wa mpira wa miguu Tanzania.
Klabu ya Simba inachukua nafasi hii ya kipekee kuishukuru serekali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa hatua mahsusi na za haraka katika kutafuta suluhisho la kudumu la jambo hili.
Tunawaomba wanachama na washabiki wetu watulie na sote tuache majibizano yoyote ili kutoa fursa kwa Serikali kusimamia kikamilifu jambo hili.
Klabu ya Simba inafanya mawasiliano na Jeshi la Polisi nchini kuwajulisha kusudio letu la kusitisha maandamano hayo.
IMETOLEWA NA…
Haji S Manara
Mkuu wa Habari wa Simba SC
Simba nguvu moja

‘Hata tukikutana na Simba poa tu’ Cannavaro


Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kikosi chao kipo tayari kupambana na timu yoyote katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA au Azam Sports Federation Cup huku akiamini watafanya vizuri na kusonga mbele kucheza fainali ya michuano hiyo.
Tayari timu nne zinazotarajiwa kucheza nusu fainali zimeshajulikana (Simba, Mbao FC, Azam FC na Yanga) ambazo zitambana kutafuta washindi wawili watakaocheza fainali.
“Yoyote atakaepangwa na sisi kwenye hatua ya nusu fainali tutapambana nae ili kupata ushindi na kufika hatua ya fainali. Hata tukipangwa na Simba ndio tayari ratiba itakuwa inaonesha hivyo, tupo tayari kuwakabili kwa sababu huwezi kuwa bingwa bila kukutana na mpinzani wako, lazima umshinde ndipo uchukue kombe.”
Yanga walipata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa jana April 22, 2017 na kufanikiwa kusonga mbele kwenye hatua hiyo ya nusu fainali.
Droo ya kuzipata timu zitakazo pambana kwenye nusu fainali itachezeshwa leo kwenye ofisi za Azam TV ambao ndiyo wadhamini wakuu wa michuano hiyo ambayo msimu huu ilishirikisha jumla ya timu 86 (ligi kuu timu 16, ligi daraja la kwanza timu 24 na ligi daraja la pili timu 24)

Maagizo ya BMT kwa TFF na Simba kuhusu mgogoro unaoendelea


Wakati kukiwa na mvutano kati ya klabu ya Simba na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeingilia kati mvutano huo na kutoa maagizo mato kwa TFF na Simba.
Katibu Mkuu wa BMT ametoa taarifa (barua) kwa vyombo vya habari akizitaka taasisi hizo mbili kumalizana kwa njia ya amani huku akisisitiza kila upande kutimiza majukumu yake kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazokubalika.
Barua ya maelekezo kutoka BMT kwa TFF na Simba;

‘Hatuihofii Simba’ – Juma Mwambusi





KOCHA msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema hawahofii timu yoyote watakayo kutanana nayo katika nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup.
Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Kombe la FA, uliochezwa jana katika Uwanja Wa Taifa.
“Sisi ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hili na tumejipanga kuhakikisha tunalitetea taji letu kwa nguvu zote, lakini tunajua timu zilizofika hatua hii ni bora lakini hatuihofii yoyote kama vile Simba, Azam, Mbao,” amesema Mwambusi.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo kumalizika, kocha Mwambusi amesema, wachezaji wa timu zote mbili walicheza vizuri lakini mvua ilionekana kama kikwazo kwa wachezaji kutocheza kabumbu safi.
Timu yoyote itakayotwaa taji hilo itaiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ni kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).


HABARI MBAYA MAN UNITED, ZLATAN NJE HADI MWAKANI 2018



Manchester United itamkosa mshambulizi wake nyota, Zlatan Ibrahimovic hadi mwaka 2018.

Zlatan aliumia katika mechi ya Europa baada ya kuruka juu, wakati anatua mguu wake ulipinda kwenda nyuma.

Imeelezwa ameumia misuli mikubwa ambayo imechanika katika goto la mguu wake wa kulia.

Hizi ni habari mbaya kwa mashabiki wote wa Man United kumkosa mkongwe huyo kwa kuwa katika msimu wa kwanza tu alishafunga mabao 28.

Siku yake ya kutimiza miaka 36, mwezi Oktoba, mwaka huu itamkuta Zlatan akiwa na nje.


Mechi - 46
Mabao - 28
Assisti - 9

Nafasi alizotengeneza - 88 

DE GEA SAFARI YA KUREJEA MADRID "IMEKWIVA", ALIWEKA SOKONI JUMBA LAKE LA KIFAHARI



Dalili zote sasa kwamba kipa, David De Gea wa man United atarejea Hispania na kujiunga na vigogo, Real Madrid.

Hii inatokana na uamuzi wa kips huyo aliyejiunga na Man United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid kuliweka sokoni jumba lake la kifahari analoishi.

De Gea ametangaza kuliuza jumba hilo lenye thamani ya pauni million 3.85.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, Madrid imekuwa ikipambana kumpata De Gea ambaye anaonekana ndiye kipa tegemeo wa timu ya taifa ya Hispania.







MASHABIKI WA CHELSEA WAJITOKEZA KUMPOKEA DROGBA AKIJIUNGA NA TIMU YA MAREKANI



Mshambuliaji mkongwe, Didier Drogba amepokelewa kwa shangwe wakati akitua nchini Marekani kujiunga na timu ya Phoenix Rising ya mjini Arizona.

Lakini ajabu, mashabiki wengi wa Phoenix walionekana zaidi ni mashabiki wa Chelsea, timu ambayo Drogba alipata umaarufu mkubwa.

Mashabiki hao walitaka Drogba kusaini jezi za Chelsea ya England badana Phoenix ambayo ni timu yao.



Kilichovutia zaidi mashabiki hao walikuwa na jezi mpya zinazotumiwa sasa na Chelsea, zikiwemo zile za nyumbani na ugenini.

Drogba alipata mafanikio makubwa akiwa Chelsea ambako aliiongoza kubeba makombe lukuki kama Kombe la Ligi, Kombe la FA, Ubingwa wa England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.


SERIKALI IMEITUMIA SALAMU ZA PONGEZI SERENGETI BOYS, NI BAADA YA KUTOA KIPIGO KWA GABON




Serikali imeipongeza Serengeti Boys kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Gabon.

Serengeti Boys wameifunga Gabon katika mechi iliyopigwa nchini Morocco ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika litakalofanyika nchini Gabon.

Msemaji wa Serikali Dk, Hassan Abbas amesema serikali inaipongeza timu hiyo ya vijana chini ya miaka 17 kwa ushindi huo.


Serikali inawasisitiza vijana hao kuendelea kupambana wakiwa wamelenga kufanya vizuri na Watanzania na serikali iko nyuma yao.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif