Friday, April 21, 2017
Ndoto za Samatta kukutana na Manchester United kwenye Europa zazimwa na Celta Vigo By shaffihdauda - April 20, 2017 9516 0 SHARE Facebook Twitter Ndoto za Mbwana Samata kusonga mbele zaidi katika michuano ya Europa imekatishwa na klabu ya Celta Vigo baada ya timu yake ya Genk kulazimishwa suluhu ya bao moja kwa moja na wababe hao wa Hispania. Pione Sisto alikuwa wa kwanza kuchungulia nyavu za Genk dakika ya 63 kabla ya Leandro Trossard kuwasawazishia Genk na mchezo kumalizika kwa sare. Kabla ya mchezo huo Celta Vigo hawajawahi kufungwa na timu yoyote kutoka Ubelgiji na matokeo hayo yaliifanya Genk kutolewa kwa jumla ya mabao 3 kwa 4, kwani mchezo wa kwanza walikubali kipigo cha bao 3 kwa 2. Katika michezo mingine iliyopigwa jana ililazimika kuongezwa muda wa ziada ili kumtafuta mshindi wa michezo hiyo, Manchester United na Anderchelt walimaliza dakika 90 kwa sare ya moja kwa moja. Baada ya dakika hizo 90 kuisha muamuzi aliongeza dakika 30, dakika ya 107 ya mchezo huo goli la Rashford liliivusha Manchester United katika hatua ya nusu fainali ya Europa Champions msimu huu. Ajax nao bao la dakika ya 120 la Amin Younes lilishuhudia klabu hiyo ikifudhu hatua ya nusu fainali baada ya kumaliza mchezo huo kwa bao 3 kwa 2 dhidi ya Shalke 04 na mchezo huo kuisha kwa aggregate ya bao 3 kwa 4na kufudhu tena nusu fainali tangia mwaka 1997. Besitikas na Lyon hadi dakika 120 zinaisha mshindi alishindwa kupatikana japo Bestikas walikuwa wakuongoza 2 kwa 1 lakini aggregate ilikuwa 3 kwa 3 hivyo mchezo huo ilibidi uamuliwe kwa tuta. Katika hatua ya matuta Lyon ambao walikuwa wageni katika mchezo huo waliibuka kidedea kwa kushinda jumla ya matuta 7 kwa 6 na hivyo nao kuungana na Celta Vigo,Manchester United na Ajax katika michuano hiyo ya Europa.
Pione Sisto alikuwa wa kwanza kuchungulia nyavu za Genk dakika ya 63 kabla ya Leandro Trossard kuwasawazishia Genk na mchezo kumalizika kwa sare.
Kabla ya mchezo huo Celta Vigo hawajawahi kufungwa na timu yoyote kutoka Ubelgiji na matokeo hayo yaliifanya Genk kutolewa kwa jumla ya mabao 3 kwa 4, kwani mchezo wa kwanza walikubali kipigo cha bao 3 kwa 2.
Katika michezo mingine iliyopigwa jana ililazimika kuongezwa muda wa ziada ili kumtafuta mshindi wa michezo hiyo, Manchester United na Anderchelt walimaliza dakika 90 kwa sare ya moja kwa moja.
Baada ya dakika hizo 90 kuisha muamuzi aliongeza dakika 30, dakika ya 107 ya mchezo huo goli la Rashford liliivusha Manchester United katika hatua ya nusu fainali ya Europa Champions msimu huu.
Ajax nao bao la dakika ya 120 la Amin Younes lilishuhudia klabu hiyo ikifudhu hatua ya nusu fainali baada ya kumaliza mchezo huo kwa bao 3 kwa 2 dhidi ya Shalke 04 na mchezo huo kuisha kwa aggregate ya bao 3 kwa 4na kufudhu tena nusu fainali tangia mwaka 1997.
Besitikas na Lyon hadi dakika 120 zinaisha mshindi alishindwa kupatikana japo Bestikas walikuwa wakuongoza 2 kwa 1 lakini aggregate ilikuwa 3 kwa 3 hivyo mchezo huo ilibidi uamuliwe kwa tuta.
Katika hatua ya matuta Lyon ambao walikuwa wageni katika mchezo huo waliibuka kidedea kwa kushinda jumla ya matuta 7 kwa 6 na hivyo nao kuungana na Celta Vigo,Manchester United na Ajax katika michuano hiyo ya Europa.
TFF imemfungulia mashtaka Haji Manara leo April 21, 2017
Manara wakati akizungumza na waandishi wa habari, alizungumzia Simba kudhulumiwa na TFF kwenye baadhi ya mambo waliyofikisha kwenye vyombo vya sheria vya shirikisho hilo, aliituhumu TFF kuipendelea Yanga lakini pia akaituhumu TFF kuendeshwa kwa ukabila pamoja na mambo mengine.
Leo April 21, 2017 zikiwa zimepita siku mbili tangu Manara azungumze na vyombo vya habari, TFF imetangaza kufungua mashtaka ya kinidhamu dhidi ya Manara.
Kupitia ukurasa wa Instagram (tanfootball) ukurasa rasmi wa shirikisho la soka Tanzania, kuna habari inayosomeka kama ifuatavyo…
>>>Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kila mwanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania analazimika kuheshimu na kufuata kanuni za maadili za shirikisho kama zilivyoainishwa kwenye kanuni zake mbali mbali.
Wanafamilia wa mpira wa miguu ni pamoja na wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi wa mpira wa ngazi zote na waajiriwa wa taasisi ambazo ni wanachama wa TFF wa ngazi mbalimbali.
Ili kutunza heshima ya mpira wa miguu Tanzania, wanafamilia wa mchezo huo katika kutimiza masharti ya kanuni za maadili za TFF, hawana budi kuheshimu na kufuata taratibu zote hizo ndani na nje ya uwanja.
Taswira njema ya shirikisho inajenga imani ya wadau wakiwamo serikali, mashirika mbalimbali ya umma na binafsi, vyombo vya habari, vyama vya mpira vya kimataifa, NGO’s na watu binafsi kwa taasisi (TFF). Kinyume chake ni kulibomoa shirikisho.
Dhima ya uongozi wa TFF ni pamoja na kulinda na kutunza heshima hii. Hivyo vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uvunjaji wa maadili havitavumiliwa, na vikitokea hatua zitachukuliwa.
Na kwa muktadha huu Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, limemfungulia mashtaka ya kinidhamu Msemaji wa Simba Bw. Hajji Manara kwenye Kamati ya Nidhamu. Leo hii Aprili 21, 2017 atapewa mashtaka yake na kujulishwa lini na wapi yatasikilizwa.
TFF inaendelea kutoa rai kwa wadau wa mpira kuwa pamoja ni kwamba ni haki yao kushauri, kupendekeza, kukosoa lakini yote haya yafanyike kwa staha ili kutunza heshima ya mpira wetu.
Kimenya amemzungumzia mchezaji wa Kagera Sugar
BEKI wa kulia wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya, amemtabiria mambo makubwa Mshambuliaji wa Kagera Sugar Mbaraka Yusuph ambae kwa sasa yupo kwenye kiwango kizuri.
Mbaraka amefikisha mabao 11 tangu asajiliwe na Kagera Sugar akitokea Simba mara baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka moja aliosaini akiwa na timu ya vijana ya Simba.
Shaffihdauda.co.tz. ilizungumza na Kimenya ambaye alisema, kama Mbaraka akiendelea kujituma na kupambana kama ilivyo sasa atafika mbali ila kikubwa asilewe sifa na kusahau majukumu yake ya uwanjani.
“Mimi natamani na ninamuombea katika
kinyanganyiro cha mfungaji bora apate Mbaraka kwani kijana anajua kucheka na nyavu na pia atakuwa amewakumbusha watu kuwa sio timu kubwa tu zinaweza kutoa mchezaji bora hata huku chini zipo,” alisema Kimenya.
Kimenya amenijuza kuwa kuna takriba timu tatu za ligi zinataka saini yake lakini kwa sasa ni mapema sana kuziweka wazi ikiwa bado masuala mengi hayajakamilika .
Beki huyo ambae alikuwa kwenye mipango ya kusajiliwa na Simba msimu huu, lakini viongozi wa Simba walishindwana bei aliyokuwa anataka Kimenya ambayo ilikuwa ni shilingi milioni 40za Tanzania.
Hazard azungumzia ugomvi wake na Mourinho.
Kati ya wachezaji ambao inatajwa kama walikuwa na ugomvi na Mourinho ni Eden Hazard ambaye tetesi zinasema msimu wa mwisho wa Mourinho Chelsea waligombana sana na Hazard akawa hamsikilizi.
Baada ya uvumi huo kuenea kwa muda sasa, Hazard ameibuka na kuzungumzia ugomvi wake na Mou ambapo alikanusha na kusisitiza uhusiano wao ulikuwa mzuri sana na anamuheshimu sana kocha huyo.
“Tulikuwa na uhusiano mzuri tuu, kuna msimu nilikuwa mchezaji bora na ikamfanya atarajie makubwa kutoka kwangu msimu unaofuata ila mambo yakawa kombo, lakini nakumbuka uhusiano wangu na yeye ulikuwa mzuri sana” alisema Hazard.
Hazard anasema mahusiano yake na Mourinho yalikuwa mazuri kama ilivyo tu kati yake na kocha wa sasa wa timu hiyo Antonio Conte na kusema hakuwahi kuwa na tofauti yoyote na kocha huyo.
Hazard ambae tetesi zinadai yuko msimu wake wa mwisho Chelsea kabla ya kutimkia Real Madrid amesema Mourinho ni kocha aliyeshinda makombe kabla na baada ya Chelsea na ni lazima aheshimiwe kwa hilo.
Mambo aliyofanikiwa Mbappe hadi sasa kuliko Ronaldo na Messi.
1.Magoli mengi kabla ya miaka 19. Wakati Cristiano Ronaldo anajiunga na Manchester United, kabla hajafikisha miaka 19 alifunga bao moja tuu lakini Lioneil Messi naye kabla kufikisha umri huo alifunga mbao 7, lakini hadi sasa Kylian Mbappe kabla siku ya kutimiza miaka 19 haijafika ameshaweka kambani mabao 13 ikiwa ni zaidi ya Ronaldo na Messi ukiyaweka kwa pamoja wakati wakiwa na umri huo.
- Aweka historia UEFA. Bao alilofunga dhidi ya Dortmund lilimfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mfululizo katika michezo yake minne ya mwanzo katika hatua ya mtoano ya UEFA, sio Messi wala sio Ronaldo aliyewahi kufanya jambo kama hilo.
- Historia nyingine Uefa. Ni wachezaji 6 tu ndio ambao wamewahi kufunga katika mechi zao nne za mwanzo walizoanzishwa katika UEFA, katika orodha hiyo Messi na Ronaldo hawapo ila jina la Kyllian Mbappe lipoo.
5.Kushoto na kulia yeye sawa tu. Wakati Messi na Ronaldo wana miguu yao ya mauaji, Kylian Mbappe katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga kwa miguu yoteyote katika champions league.
Beki wa Chelsea aongoza kupiga pasi timilifu
Lakini takwimu zinaonesha anayeongoza kwa kupiga pasi zilizowafikia walengwa wala sio kiungo bali ni mlinzi, beki wa kulia wa Chelsea Cesar Azpilicueta ndio mchezaji anayeongoza kupiga pasi zilizowafikia walengwa.
Azpilicueta hajapiga pasi nyingi kama Pogba au Henderson lakini pasi zake chache alizopiga ziliwafikia walengwa na kumfanya kukamilisha pasi kwa 87.62%.
Azpilicueta amepiga pasi 2028 lakini kati ya hizo, pasi 1777 ziliwafikia walengwa na hiyo kumfanya kuwa na wastani huo wa 87.62%, huku kiungo wa Liverpool Jordan Henderson akiwa nafasi ya pili.
Henderson hadi sasa amepiga pasi 2057, ikiwa ni pasi nyingi kuliko Azpilicueta lakini katika pasi za Henderson ni pasi 1767 sawa na 85.90% ambazo zimewafikia walengwa.
Paul Pogba naye hadi sasa amepiga pasi nyingi zaidi kuliko Henderson na Azpilicueta ikiwa ni pasi 2070 lakini kati ya pasi hizo za Pogba ni jumla ya pasi 1763 tu zilizowafikia walengwa.
Ngolo Kante yuko nafasi ya nne chini ya Pogba akiwa amepiga pasi chache kuliko Pogba, Kante amepiga pasi 1899 lakini kati ya hizo ni pasi 1686 alizofanikiwa kufikisha kwa walengwa.
Ander Herrera wa Manchester Unite yuko nafasi ya tano ambapo hadi sasa amepiga pasi 1853, kati ya pasi hizo ni pasi 1629 ambazo Herrera alikamilisha.
Ugo Ehiogo afariki dunia, ni nani huyu?
Ehiogo ana jina la Kinigeria lakini ni mzaliwa wa nchini Uingereza mwaka 1972, alifanikiwa kucheza kwa mafanikio makubwa kama mlinzi wa kati katika vilabu vya Leeds, Aston Villa, Rangers na Sheffield United na timu ya taifa ya Uingereza.
Baada ya kumaliza kucheza soka Ehiogo aliamua kuwa mwalimu wa mpira wa miguu na timu yake ya kwanza kufundisha ilikuwa ni Tottenham Hotspur chini ya miaka 23 na hata shambulio lake la moyo lilimpata asubuhi ya Alhamisi akiwa mazoezini na timu yake.
Siku ya Alhamisi Ehiogo alianguka ghafla mazoezini hapo na kukimbizwa hospitali ambapo taarifa zinasema asubuhi ya Ijumaa alifariki na ameacha mjane aitwaye Gemma na pia mtoto mmoja wa kiume.
Ehiogo ameshawahi kushinda kombe la ligi mwaka 1994 na 1996 akiwa na Aston Villa lakini pia akashinda kombe hilo mwaka 2004 akiwa na Middlesbrough, beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand amesema hadi sasa haamini kama Ehiogo ameondoka.
Nusu fainali UEFA ni kisasi cha Madrid, Monaco kinywani mwa Juventus.
Unakumbuka jinsi Simeone alivyofungwa na Real Madrid mara
mbili katika fainali za Champions League? Pengine ni kati ya suala
ambalo Simeone hataki kulikumbuka kabisa.
Lakini sasa amepewa nafasi ya kulipa kisasi kwani katika droo ya Champions League iliyofanyika mchana huu majirani hao wawili kutoka mji wa Madrid wanakutana katika nusu fainali ya Champions League
Atletico ambao walifika katika hatua hii baada ya kuwaondoa mabingwa wa soka wa nchini Uingereza klabu ya Leicester City wanakutana na Real Madrid ambao nao waliiondosha kwenye michuano hii miamba ya Ujerumani klabu ya Bayern Munich.
Tayari watu wameshaanza kuusubiri mchezo huu kwa hamu kubwa haswa wakikumbuka fainali ya mwaka 2014 na ile ya 2016 ambazo ziliwakutanisha Madrid na Atletico huku zote Madrid wakiibuka kidedea
Nusu fainali nyingine itakuwa kati ya Monaco ambao msimu huu hawashikiki watakaokutana na timu ngumu zaidi kufungika katika mashindano haya ya msimu huu,klabu ya Juventus kutoka nchini Italia.
Monaco wanaingia katika nusu fainali hii wakijiamini kutokana na kuwa na safu ya ushambuliaji kiwembe ambapo Mbappe na Falcao wamekuwa wauaji wa nyavu lakini wakikutana na ukuta mgumu wa Juventus ambao waliwatoa Barcelona katika hatua ya robo fainali.
Nusu fainali ya kwanza itapigwa tarehe 2 na 3 mwezi wa 5, kabla ya michezo ya marudiano itakayopigwa tarehe 9 na 10 ya mwezi huo huo wa tano.
Lakini sasa amepewa nafasi ya kulipa kisasi kwani katika droo ya Champions League iliyofanyika mchana huu majirani hao wawili kutoka mji wa Madrid wanakutana katika nusu fainali ya Champions League
Atletico ambao walifika katika hatua hii baada ya kuwaondoa mabingwa wa soka wa nchini Uingereza klabu ya Leicester City wanakutana na Real Madrid ambao nao waliiondosha kwenye michuano hii miamba ya Ujerumani klabu ya Bayern Munich.
Tayari watu wameshaanza kuusubiri mchezo huu kwa hamu kubwa haswa wakikumbuka fainali ya mwaka 2014 na ile ya 2016 ambazo ziliwakutanisha Madrid na Atletico huku zote Madrid wakiibuka kidedea
Nusu fainali nyingine itakuwa kati ya Monaco ambao msimu huu hawashikiki watakaokutana na timu ngumu zaidi kufungika katika mashindano haya ya msimu huu,klabu ya Juventus kutoka nchini Italia.
Monaco wanaingia katika nusu fainali hii wakijiamini kutokana na kuwa na safu ya ushambuliaji kiwembe ambapo Mbappe na Falcao wamekuwa wauaji wa nyavu lakini wakikutana na ukuta mgumu wa Juventus ambao waliwatoa Barcelona katika hatua ya robo fainali.
Nusu fainali ya kwanza itapigwa tarehe 2 na 3 mwezi wa 5, kabla ya michezo ya marudiano itakayopigwa tarehe 9 na 10 ya mwezi huo huo wa tano.
Subscribe to:
Posts (Atom)