Wednesday, May 13, 2015



Simon Sserunkuma (kushoto) akielekezwa jambo na kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Simon Sserunkuma alisajiliwa dirisha dogo na klabu ya Simba, lakini kiwango chake kimeshindwa kuwaridhisha mabosi wa Msimbazi.'
KIUNGO mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Simon Sserunkuma, ameomba kuendelea kuitumikia Simba kwa miezi sita zaidi licha ya klabu hiyo kutangaza kumtema.
Simon Sserunkuma na Waganda wenzake, Dan Sserunkuma na Joseph Owino, walitangazwa na klabu ya Simba juzi kwamba hawataendelea kuitumikia klabu hiyo ya Msimbazi baada ya viwango vyao kutowakosha mabosi wao.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, ameuambia mtandao huu muda mfupi uliopita kuwa Simon ameomba miezi sita wamuangalie zaidi na asiporidhisha katika kipindi hicho, atakuwa tayari kuondoka.
"Ni kweli wachezaji wetu watatu kutoka Uganda tumeamua kuachana nao, lakini mmoja ambaye ni Simon Sserunkuma ameomba tumpe miezi sita zaidi ya kumwangalia," amesema Hanspope.
Kiongozi huyo amesema watavuka nje ya mipaka ya Tanzanua kusaka nyota wengine wakali watakaoziba nafasi zilizoachwa na Waganda hao.
13 May 2015


KOCHA wa timu ya Real Madrid atakosa michezo yote iliyobakia ya msimu huu baada ya kufungiwa na shirikisho la soka la Hispania {RFEF}.
Kufungiwa huko kunahusishwa na makofi ya dharau aliyompigia refa wa mchezo kati ya Real Madrid na Valencia waliyotoka sare ya goli 2-2 jumamosi iliyopita.
Ancelotti alikutwa na makosa hayo baada ya kuvunja sheria ya kifungu namba namba 117 cha nidhamu ambayo inasema “kwa wote ambao watashughulika na waamuzi awe meneja au maafisa wengine kwa hali yoyote ile awe na hasira au mitazamo ya dharau au kupuuza … adhabu yao ni kusimamishwa ” .
Mwamuzi Carlos Clos Gomez aliandika katika ripoti yake ya mchezo” Mwisho wa mchezo kocha Ancelotti kutoka umbali wa mita 30,aligeuka na kunipigia makofi ambayo ni ya dharau na yanapingana na maamuzi yangu  katika mchezo ule”
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 atakosa mechi hizo hadi msimu huu unaisha dhidi ya Espanyol na Getafe,katika harakati za kupunguza pengo la pointi 4 dhidi ya vinara wa ligi hiyo Barcelona.
Real Madrid wanakutana na Juventus leo katika usiku wa ulaya na kujaribu kubadili matokeo ya 2-1 baada ya kupoteza mechi ya kwanza,Barcelona tayari wameshafuzu kwa fainali ya juni 6 pale Berlin.


REAL Madrid walihitaji ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Juventus usiku huu ili kutinga fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, lakini ndoto zao zimezimwa Santiago Bernabeu.

Cristiano Ronaldo ameamusha uwanja wa mzima wa Bernabeu baada ya kufunga goli la kuongoza dakika ya 23' kwa mkwaju wa penalti na limedumu mpaka mapumziko,  lakini Alvaro Morata amesawazisha goli hilo dakika ya 57' akipokea pasi murua kutoka kwa Paul Pogba.

Morata ameiadhibu klabu yake ya zamani na kuunyamazisha mji wa Madrid baada ya mabingwa hao watetezi wa UEFA, Real Madrid kuvuliwa taji lao walilotwaa mjini Lisbon mwaka jana wakiifunga Atletico Madrid.
Mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Juventus mjini Turin, Juve walishinda magoli 2-1 na kutokana na sare ya leo wanatinga fainali kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-2.
Licha ya matokeo hayo, mechi ya leo imebalansi kwa muda mrefu na timu zote zimemilikia mpira asilimia 50 kwa 50, lakini dakika za mwisho Real wameongeza asilimia za kumiliki mpira mpaka kufikia 53 kwa 47.
Juventus tangu droo ya nusu fainali ilipotoka, watu wengi waliwadharau, lakini wamefanikiwa kutinga fainali itayofanyika juni 6 mwaka huu mjini Berlin, Ujerumani dhidi ya Barcelona fc.
Barca walitinga fainali jana kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-3 dhidi ya Bayern Munich.
Mechi ya kwanza Camp Nou, Barca walishinda 3-0 na jana usiku walifungwa 3-2.

TAKWIMU ZA LEO

Saturday, May 9, 2015

EBU ONA WACHEZAJI AMBAO NI MARAFIKI ZAIDI DUNIANI

Katika uhalisia wa maisha ya ulimwenguni hapa, kuna watu ambao wana marafiki wengi tu katika sehemu mbalimbali, iwe maofisini, mashuleni na kadhalika.
Lakini mbali na hivyo lazima kutakuwa na mtu mmoja tu ambaye ndio rafika yako kipenzi zaidi ya marafiki zako wengine.
Vivyo hivyo katika ulimwengu wa soka kuna wachezaji wengi tu ambao ni marafiki wa kutupwa.
Hawa ni baadhi tu ya wachezaji ambao urafiki wao ni wa kupika na kupakua, kwa maana ya kwamba, urafiki wao ni mkubwa sana katika maisha yao kila siku.
10, Olivier Giroud na Laurent Koscielny
9. Sergio Ramos na Iker Casillas

8. Cesc Fabregas na Gerard Pique

7. Lionel Messi na Jose Manual Pinto

6. Zlatan Ibrahimovic na Maxwell Scherrer

5. Cristiano Ronaldo na Marcelo

4. Mousa Dembele na Jan Veronghen

3. Mario Gotze na Marco Reus

2. Gareth Bale na Luka Modric

1. Thiago Silva na David Luiz
09 May 2015

LIGI KUU YA TANZANIA BARA YAFIKIA TAMATI LEO


Pazia la ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2014/15 limefungwa rasmi leo, ambapo imeshudiwa timu za Ruvu Shooting na Polisi Moro zikishuka daraja baada ya kupoteza michezo yao.
Kwa kuanzia katika jiji la Mbeya, timu ya Mbeya City walikuwa wakiwakaribisha Maafande wa Polisi Moro ambao hata hivyo walikuwa tayari wameshuka daraja. Katika mchezo huo Mbeya City walishinda kwa bao 1-0.
Mkoani Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, kulikuwa na pambano kali na la kusisimua, ambapo Ndanda FC walikuwa wakiwakaribisha mabingwa wapya wa ligi hiyo Yanga SC na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0. Matokeo hayo yamezua shangwe na vifijo kwa Ndanda baada ya kijihakikishia nafsi yao ya kubaki ligi kuu kwani endapo wangepoteza mchezo huo basi wangeshuka daraja moja kwa moja.
Katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ilikuwa ni patashika nguo kuchanika pale Stand United walipokuwa awanawakaribisha Ruvu Shooting, matokeo ya mchezo huo ni kwamba Stand waliibuka na ushindi wa goli 1-0 kwa bila na kunusurika kushuka daraja, huku Ruvu Shooting wao wakiteremka daraja.
Huko Manungu Complex katikati ya mshamba ya miwa, Mtibwa walikuwa wakiwakaribisha Wagosi wa Kaya Coastal Union, ilishuhudiwa Mtibwa wakifungwa mabao 2 kwa 1 na hata hivyo timu hizo kusalia katika ligi kuu msimu ujo.
Nao Tanzania Prisons ya Mbeya na Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera walitoshana nguvu kwa kutoka suluhu, mchezo huo ulipigwa katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza. Matokeo hayo yameinusuru Prisons kushuka daraja na kusalia ligi kuu kwa msimu ujao.
Nako katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, timu ya JKT walikuwa wanawakaribisha Wekundu wa Msimbazi Simba Sc na kushuhudia Simba wakiibuka na ushinda wa magoli 2-1. Mchezo huo ulikuwa hauna athari yoyote kwa timu zote mbili, hivyo kusalia ligi kuu.
Kwenya uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Azam Fc waliwakaribisha vijana wa Mgambo JKT kutoka jijini Tanga na kushuhudia timu hizo zikitoka suluhu.
Timu ambazo zimepanda ligi kuu kwa msimu ujao ni Mwadui FC, Majimaji, Toto Africans na African Sports.






RnTimuPWDLFAGdPts
1YANGA26174552183455
2Azam FC261310336181849
3SIMBA SC26138538191947
4MBEYA CITY2681082222034
5MTIBWA SUGAR2671182525032
6KAGERA SUGAR2688102226-432
7Coastal Union2671182025-532
8JKT RUVU2687112025-531
9NDANDA FC2687112129-831
10STAND UNITED2687112334-1131
11T. PRISONS2651471822-429
12MGAMBO SHOOTING2685131828-1029
13RUVU SHOOTING2678111629-1329
14POLISI MORO26510111627-1125

Friday, May 8, 2015

BENTEKE MCHEZAJI BORA WA MWEZI KTK LIGI YA UINGEREZA

BE
Mshambuliaji Christian Benteke ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu England kwa mwezi wa Aprili.


Benteke amekuwa mchezaji wa kwanza wa Aston Villa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi tokea Desemba, 2008 alipishinda Ashley Young ambaye sasa yuko Manchester United.

Thursday, May 7, 2015

NOIJ AITA 28 KUELEKEA COSAFA


Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakaoingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam, kujiandaa na michuano ya kombe la COSAFA na kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN mwezi Juni mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF amesema, wachezaji 28 aliowaita, amewaona kwa macho yake wakicheza, na katika wachezaji aliowaita amechanganya wanaochipukia (damu changa) na wenye uzoefu wa michuano ya kimataifa.
Nooij amesema katika orodha hiyo ya wachezaji 28 watakaoripoti kambini jumatatu mchana, watapimwa afya zao na madakatari wa timu ya Taifa, na kisha watakaokuwa fit atachagua wachezaji 20 watakaokwenda kwenye michuano ya COSAFA nchini Afrika kusini.
Aidha Nooij ameongeza wachezaji 8 watakaobakia nchini wanapaswa kuwa tayari wakati wowote wanaweza jumuishwa katika kikosi kutokana na Taifa Stars kukabiliwa na michuano mbalimbali ambayo pia inahitaji kuwa na wigo mpana wa wachezaji.
Wachezaji walioitwa na kocha Nooij ni magolikipa: Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ali (Azam), walinzi: Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Haji Mwinyi (KMKM).
Wengine ni viungo: Amri Kiemba, Salum Abubakar, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhira).
Washambuliaji ni Ibrahim Ajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John Bocco, Kelvin Friday (Azam) na Juma Luizio (Zeco United).
Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumatano, Mei 13 saa 1 jioni kwa shirika la ndege la Fastjet kuelekea nchini Afrika Kusini katika mji wa Rusterburg - North West Province ambapo ndipo michuano ya COSAFA CUP itafanyika kuanzia Mei 17 mpaka Mei 31 mwaka huu.
Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars iliyopo katika kundi B katika michuano ya COSAFA, itacheza dhidi ya Swaziland Mei 18, Mei 20 (Madagascar Vs Tanzania) na Mei 22 ( Tanzania vs Lesotho), mshindi wa kundi B atacheza robo fainali dhidi ya timu ya Taifa kutoka Ghana.
Mara baada ya kumalizika kwa michuano hiyo, Taifa Stars itarejea nchini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017, dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 13 nchini Misri, kisha kurejea nchini kucheza na Uganda Juni 21 kuwania kufuzu kwa fainali za wachezaji wa ndani CHAN.
Mart Nooj amesema ataitumia michuano ya COSAFA kama sehemu ya maandalizi ya michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN.

CHEKI ALICHOSEMA PEP GUADIOLA BAADA YA MCHEZO WA JANA


Uwezo wa Lionel Messi ndio uliamua matokeo ya mchezo wa jana kati ya Barcelona and Bayern Munich, mchezo ambao ilishuhudiwa Bayern ambao ni mabingwa wa Ujerumani wakipokea kipigo cha mabao 3-0 katika uwanja wa Camp Nou. Hayo ni maneno ya Pep Guardiola ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona.
Messi alifunga magoli mawili katika mchezo huo huku akitoa pasi ya bao la mwisho lililofungwa na Mbrazil Neymar Santos Jr.
"Bayern wamefanya vizuri kwa kipindi kirefu sana," alisema Guardiola ambaye aliifunika Barca kwa umiliki wa mpira, kitu ambacho ni adimu sana kutokea kwa Barca, wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kuwa mara ya mwisho hali hiyo kutokea kwa Barca ni mwaka 2006, alisema. 
"Lakini Messi alionesha ubora wake. Barca sio sana kivile, ila yeye si wa kawaida, Barca ni timu imara ambayo ina nyota wengine wazuri kama vile Luis Suarez na Neymar.
"Barca ni wazuri mno, wana uwezo wa kutengeneza nafasi popote watakapo. Ni vipaji vya wachezaji wao ndio vilitupoteza, kucheza hapa Camp Nou ni vigumu sana.
"Lakini hata hivyo nadhani tuliuweka mpira katika himaya yetu, mapaka pale walipopata goli lao la kwanza. Ni baada ya pale ndipo tulipoanza kupoteana, lakini sitalaumu mchezaji yeyote yule, timu imepitia vipindi vigumu sana msimu huu."

MWADUI FC YAVUNJA UKIMYA JUU YA KOCHA WAO

Uongozi wa timu ya Mwadui ya mkoani Shinyanga umefunguka juu ya taarifa za kuachana na kocha wake.
Taarifa mbalimbali zilidai kuwa kuna uwezekano wa wageni hao kwenye ligi kuu msimu ujao kuachana na Jamhuri kiwelu na kusaka kocha mwingine.
Lakini Mpenja blog ilibisha hodi kwenye mgodi huo wa almasi na kuzungumza na katibu kuu wa timu hiyo Ramadhani Kilao ili kujua ukweli na undani wa taarifa hiyo, ambapo katibu huyo alikanusha taarifa hizo.
"Hizi taarifa hata sijui zinatokea wapi,kwetu hatuna hizo taarifa lakini nashangaa kuona zinazungumzwa kila siku,Julio ni kocha wetu labda yeye atuache ".Alisema Kilao.
Alipoulizwa kuhusiana na taarifa za kuwepo mpango wa kuleta kocha wa kigeni,katibu huyo amesema hawajalifikiria hilo lakini alidai kwamba uwezo wanao wa kumchukua kocha yeyote awe wa ndani au nje ya nchi.
"Uwezo wa kuleta kocha tunao tena hata tukitaka watatu,lakini kwasasa hilo hatujalifikiri"Alisema.
Kocha mkuu wa Mwadui Jamhuri kiwelu alifanikiwa kuipandisha daraja timu hiyo na baada ya kufanya hivyo aliekea kukinoa kikosi kama kocha msaidizi wa muda lakini baada ya kuondoka kwa kocha James Nandwa kikosini hapo Julio sasa ndiye kocha mkuu wa wagasi wa kaya Coastal Union.

MAZANDA BADO HALI SI NZURI

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
NYOTA wa kikosi cha Mbeya City, Steven Mazanda na Yusuph Abdalah Sisalo watalazimika kusubiri mpaka msimu ujao ili kurejea uwanjani kukitumikia tena kikosi chao kutokana na majereha makubwa waliyokuta nayo mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Daktari mkuu wa City, Dk Joshua Kaseko, amekaririwa katika mtandao rasmi wa klabu hiyo akieleza kuwa nyota hao wawili wameshindwa kupona majeraha yao katika muda uliotarajiwa hivyo waatalazimika kusubiri msimu mpya ili kurejea uwanjani.
“Awali kulikuwa na dalili njema kuwa huenda wangepona haraka na kurejea kumalizia michezo ya mwisho, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu, lakini imeshindikana  na kama unavyofahamu si jambo nzuri kumlazimisha mchezaji kucheza wakati vipimo vinaonesha bado hayuko sawa. Kwa sasa hakuna namna nyingine zaidi ya wao kuendelea na matibabu ili wapone kabaisa tayari kwa msimu ujao”, amesema Dk Kaseko.
Mazanda aliumia goti la mguu wa kulia akiwa mazoezini siku moja kabla City haijashuka dimbani Sokoine kuivaa Stand United ya Shinyanga kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliomalika kwa City kushinda bao 2-0 huku Sisalo akiumia goti la mguu wa kulia dk ya 15 ya kipindi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Ndanda Fc ulichezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Ndanda FC.

ALLIANCE YAAGWA


Na Kassim Mtolea,Mwanza
Timu ya soka ya Alliance ya Mkoani Mwanza imeagwa rasmi na Mkurugenzi wa timu hiyo James Bwire pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoani hapa(MZFA) Jackson Songora.
Akizungumza na Mpenja blog,Mkurugenzi wa timu ya Alliance James Bwire amesema kuwa maandalizi yao yapo vyema na timu itasafiri ijumaa kuelekea Manyara
Bwire alisema pia timu yao itaondoka na wachezaji 30,makocha watatu,viongozi wawili kutoka chama cha soka mkoani Mwanza,wapishi
wawili Kwa upande wa Mwenyekiti wa MZFA,Jackson songora amesema kuwa anaiomba
timu ya Alliance ifanye vyema ili ipande kuelekea ligi Daraja la pili.
Alliance FC imefanikiwa kusajili wachezaji watano kutoka timu ya Nyange na Nyamagana FC ambao ni George Philemon,Juma Mussa,Baraka
Abeid,Salim Juma na Amir Mohamed Kwa upande wake kocha wa Alliance,Kessy Mziray amesema maandalizi yao
yako vyema kwa kuwa wameweza kucheza mech tatu za kirafiki na kushinda zote.
Mechi ya Kwanza Alliance fc itacheza siku ya jumapili dhidi ya timu ya Bariadi FC kutoka Shinyanga
Alliance fc itaondoka mwanza siku ya ijumaa asubuhi kuelekea Manyara.

IVO MAPUNDA AOMBA MKATABA MPYA SIMBA


Na Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Mkataba wa Ivo na Simba umebakisha siku 13 kumalizika.'
KIPA mkongwe wa Simba, Ivo Mapunda, amesema ana matumaini ya kuendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao licha ya kutokuwapo kwa dalili zozote za mazungumzo na viongozi wa timu hiyo.
Ivo mwenye mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba tangu atue kwenye mzunguko wa pili msimu uliopita akitokea Gor Mahia ya Kenya, ameuambia mtandao huu kuwa angependa kuendelea kuichezea timu hiyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya, lakini ameuachia uongozi na benchi la ufundi uamue.
“Ninaamini nimefanya kazi nzuri katika msimu mmoja na nusu niliofanya kazi hapa Simba, lakini kama mchezaji siwezi kulazimisha nimewaachia viongozi na benchi la ufundi kama wataona ninafaa, watanifuata tuzungumze. Ninadhani hatutoshindwa kufikia makubaliano kwa sababu tumefanya kazi kwa pamoja na tunajuana,”amesema Ivo.
Mkataba wa Ivo mwenye umri wa miaka 31, utamalizika Mei 20, mwaka huu na kiwango chake kimekuwa msaada kwa Simba, licha ya makosa machache yaliyoigharimu timu yake msimu huu na kusababisha kupoteza baadhi ya mechi ikiwamo ile ya Kagera Sugar FC iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo alimtemea Atupele Green mpira uliorushwa na Salum Kanoni na kumweka katika utata.

PACQUIAO AFANYIWA UPASUAJI WA BEGA


Pacquiao afanyiwa upasuaji wa bega
Bondia Kutoka Ufilipino Manny Pacquiao amefanyiwa upasuaji wa bega lake alilodai kuwa ndiyo iliyopelekea yeye kushindwa na Floyd Mayweather jumapili iliyopita.
Bondia huyo tayari anakabiliwa na kesi moja huko Nevada kwa kutosema ukweli kuhusiana na hali yake ya afya kabla ya pigano.
Hata hivyo daktari wake Neal ElAttrache, amesema kuwa amefurahia matokeo ya upasuaji huo licha ya ripoti kudokeza kuwa Pacquiao anahitaji muda wa mwaka mmoja kuuguza jeraha hilo.
Mayweather amesema hana pingamizi ya kuzichapa dhidi ya Pacquiao
Pacquiao mwenye umri wa miaka 36 alinyimwa dawa ya kupunguza maumivu kabla ya mechi alipokuwa akilalama kuteguka bega.
Hata hivyo imebainika kuwa kabla ya pigano hilo shirikisho la riadha na masumbwi ya kulipwa katika jimbo la Nevada lilipuzilia mbali ombi la shindano hiyo kwani haikuwa imearifiwa awali.
NAC inapendekeza kushtakiwa kwa bondia huyo mfilipino kwani hakusajili maumivu ya aina yeyote katika fomu maalum siku moja kabla ya pigano.
Manny anakabiliwa na kesi moja huko Nevada kwa kutosema ukweli kuhusiana na hali yake ya afya kabla ya pigano.
Kutokana na masaibu yake, mwanamasumbwi wa kulipwa Floyd Mayweather, 38,amejitokeza na kusema kuwa hana pingamizi ya kuchuana tena dhidi ya Pacquiao ila katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Awali mwanadondi huyo alikuwa amesema yuko tayari kuzichapa dhidi ya Muingereza Amir Khan miongoni mwa wanandondi wengine.

DADA YAKE ADEBAYOR AJIBU MAPIGO YAKE


Baada ya status ya Adebayor ambayo ilishtua watu wengi kwenye mtandao hao mchezaji Didier Drogba alimpost Adebayor na kumuombea mambo ambayo yanaenda vibaya na familia yake yaende vizuri. Sasa kwenye ile ile post dada yake Adebayor anaitwa Lucia Adebayor amemjibu akienda kinyume na status ya Ade.
Tafsiri yake kwa ufupi ni hii hapa,
“Endelea kuongopea kaka, yako wapi magari uliyompa mama. Umeyachukua yote. nyumba unayosema umemnunulia dada vyote ni uongo. Simu alizoiba Rotimi vyote ni uongo. Pesa sio kila kitu, sisi ni familia na hatukuitaji tena uwe peke yako na sisi tuwe peke yetu. Ukweli kwamba unazo sasa hivi lakini havikuhakikishi mambo ya kesho. Mungu akusamehe.”

TAARIFA MBAYA KWA MAN CITY:YAYA TOURE ANA ASILIMIA 90 KUONDOKA


Wakala wa nahodha na kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Touré Gnégnéri amethibitisha taarifa za uhakika wa mchezaji huyo kuchana na klabu ya Man City, mwishoni mwa msimu huu.
Dimitri Seluk wakala wa kiungo huyo anayeonekana kuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Man City, amekiambia kituo cha televisheni cha Sky Sports kwamba kuna asilimia 90 kwa Toure kuondoka Etihad Stdium.
Seluk hakusema ni wapi Toure, atapoelekea endapo atakamilisha mipango ya kuondoka mjini Manchester, lakini amesisitiza suala la mchezaji wake kuhitaji kubadili mazingira ya soka lake ambalo amelicheza akiwa nchini England kuanzia mwaka 2010.
Hata hivyo inadaiwa kwamba tayari klabu tatu barani Ulaya zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Toure.
Yaya Toure akiwa na wakala wake Dimitri Seluk
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, hakuwa na mafanikio makubwa msimu huu, kama ilivyokua misimu kadhaa iliyopita, na imebainika kuna baadhi ya mambo hayamfurahishi.
Vyombo vya habari nchini Italia, jana viliripoti kwamba uongozi wa klabu ya Inter Milan umeahidi kuyafanyia kazi mapendekezo ya meneja wa klabu hiyo kwa sasa Roberto Mancini ambaye ameonyesha dhamira ya dhati ya kumsajili Yaya Toure.
Mancini alimsajili Toure mwaka 2010, akitokea nchini Hispania alipokua akiitumikia klabu ya Barcelona kwa ada ya uhamisho wa paund million 24.

HIZI NDIZO TAARIFA SAHIHI ZA TIMU ALIKOENDA MSUVA KUFANYA MAJARIBIO


Jana habari mbalimbali za Msuva kusepa kwenda kufanya majaribio ya kucheza na soka huko South Africa zilisambaa sana. Kutoka kwenye vyanzo vyangu nililiripotu kama tetesi lakini leo asubuhi nimewasiliana na Msuva mwenyewe akiwa South Africa kupata uhakika zaidi.
Majibu ni kwamba hajaenda kufanya majaribio na Orlando Pirates, timu aliyoenda kufanya nayo majaribio ni Bidvest Wits ambayo pia inashiriki ligi kuu ya South Africa.
Bidvest Wits kwa sasa ipo namba 4 nyuma ya Pirates kwenye msimamo wa ligi. Msuva alipata nafasi pia ya kuangalia mechi kali kati ya Kaizer Chiefs vs Bidvest Wits. Hapo chini kuna audio ya sauti nikiongea nae pamoja na picha akiwa uwanjani kuangalia mechi.



Huyo jamaa aliyekaa na Msuva anaitwa Charles ndie aliyemuunganishia mchongo wa trial

BY MBEGEZE

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif