Kesho macho ya wapenzi wa ligi ya Uingereza hawatakosa kuangalia mechi hii ambayo inachukuliwa kama mechi kubwa ya EPL. Mechi itafanyika kwenye uwanja wa Emirates siku ya jumapili na hiki kikosi bora kutokana na performance ya mwanzo wa ligi.
1)David de Gea
Tangu amalize mambo ya uhamisho ameonekana kutulia na kutoa mchango mkubwa kwenye ulinzi wa goli la Manchester united. Bila shaka makipa wa Arsenal hawaja perform vizuri kama De Gea.
2)Matteo Darmian
Tangu ajiunge na Man united kutoka Torino kwa gharama ya £14.4million amekua ni mchango mkubwa kwenye safu ya ulinzi wa Man united. Hivi sasa anaonekana kuwa ni kati ya wachezaji wachanga wanao-fit vizuri kwenye upande wa right back.
3)Chris Smalling
Muda kidogo ilikua kama kitu cha mzaha kwa mashabiki wa Manchester united kumuona Smalling kwenye safu ya ulinzi wa Manchester united. Lakini hivi sasa amekua mmoja kati ya watu wanaotegemewa kwenye kikosi cha united hadi hivi karibuni amecheka na nyavu.
4)Laurent Koscielny
Hii ni hasara kubwa kwa Arsenal kwenye mcchi ya kesho kwasababu Wenger anamtaja huyu jamaa kwama perfomance yake ni very outstanding. Kutokana na matatizo atakaa nje wiki tatu lakini angekua mchango mkubwa Arsenal.
5)Nacho Monreal
Huyu ni moja kati ya mabeki ambao wanachukuliwa poa kwenye EPL lakini wana impact kubwa kwenye timu. Huyu jamaa ana consistence na pia sio rahisi kuruhusu kupitwa kizembe.
6)Bastian Schweinsteiger
Huyu jamaa ni mzoefu sana na kwenye mechi moja aliwai kupiga pasi nyingi kuliko idadi ya pasi zote za timu pinzani. Anatoa msaada mkubwa kwenye timu sio tu mchezoni hadi kwenye uongozi wa timu kutokana na uzoefu aliokua nao.
7)Francis Coquelin
Huwezi kubisha juu ya umuhimu wa huyu jamaa kwenye midfield ya Arsnal. Hivyo basi lazima awepo kwenye kikosi bora cha combine
8)Juan Mata
Huyu jamaa ni attacking midfielder wa ukweli kwasababu mara nyingi sio rahisi kutabirika akiwa mchezoni. Amekua mchango mkubwa kwenye mechi za Manchester united.
9)Wayne Rooney
Labda ungeweza kumuweka Ozil hapa lakini Rooney ana attitude ya ushindi na licha kupata uhaba wa kutupia nyavuni kwenye mechi za United bado ana nafasi kuwa ya kuingia kwenye kikosi bora cha combine ya United na Arsenal.
10)Alex Sanches
Mr Hat-trick lazima awepo kwenye hiki kikosi na Depay inabidi akae pembeni. Depay amesuasua kwenye EPL labda kwasababu ya upya wake. Sanchez anachukua nafasi bila ubishi.
11)Anthony Martial
Ni zaidi ya watu walivyotegemea, huyu kijana ambae wengi wanamtaja kama mrithi wa Henry kwenye EPL amekua akifunga magoli muhimu kwa ajili ya Manchester united.