KWA NYIMBO MPYA NA MATUKIO YOTE YA KIMICHEZO
,SIASA N.K, NENDA YOUTUBE NA UTAFUTE MBEGEZE TV KISHA BONYEZA NENO
SUBSCRIBE USPIITWE NA KILA KITU
Siku zinakwenda tu na masaa yanakatika kuelekea ufunguzi wa
ligi kuu nchini Uingereza Epl hapo mwezi wa 8 na kila timu inapambana
kuhakikisha inakuwa tayari kwa ajili ya mapambano hayo.
Chelsea bado wanachechemea kusaini striker namba 9 nafasi ambayo ni
lazima wasajili kama Diego Costa ataondoka kama inavyoonekana, japokuwa
tayari wamefanya sajili kadhaa ila hii ni lazima kwao.
Alvaro Morata anawindwa na Chelsea, pamoja na kutoanza michezo mingi
msimu uliopita lakini alifunga magoli 15 na kuassist 8 na ni kati ya
washambuliaji ambao wakipewa nafasi anaweza kucheka na nyavu mara nyingi
zaidi lakini dau lake sio la kitoto inabidi uwe na pesa kuanzia £70m.
Andrea Belotti, kwa watu wanaoangalia sana Serie A wataelewa unyama
ulioko ndani ya Muitalia huyu,michezo 34 kapasia kamba mara 26 na
kuassist mara 7 hii inaonesha kila mchezo amefanya jambo, na kwa uwezo
wa Belotti hakika Conte anafaa kumsimamisha namba 9.
Pierre Aubemayang, kati ya wachezaji ambao ukimuelezea ubora wake
hutumii nguvu nyingi ni Mgabon huyu, namba hazidanganyi na mabao 31
aliyofunga toka ajiunge na BVB yanAeleza ubora wake na msimu uliopita
alikuwa ndio kinara wa mabao katika Bundesliga.
Sergio Kun Aguero, inasemekana City wako tayari kumuuza Aguero ili
kuongeza pesa za kumpata Sanchez, msimu uliopita Kun alimaliza akiwa na
mabao 20 na assist 3 huku wastani wa kufunga kila baada ya dakika 120
dakika ambazo ni Harry Kane tu mwenye chache zaidi inaonesha jinsi Kun
anavyoweza kuziba pengo la Costa.
All in All Chelsea inabidi wajipange haswa maana mastriker hao wote
kuwapata ni mbinde kubwa sana kwani kila unayemgusa klabu yake inataka
kuanzia £60m na huku Conte analalamika kuhusu bajeti ya usajili iliyopo,
kama Chelsea wakishindwa kununua striker ni bora wakae chini na Costa
wayamalize.
KWA NYIMBO MPYA NA MATUKIO YOTE YA KIMICHEZO ,SIASA N.K, NENDA YOUTUBE NA UTAFUTE MBEGEZE TV KISHA BONYEZA NENO SUBSCRIBE USPIITWE NA KILA KITU
Emmanuel Adebayor aliitumikia Real Madrid kwa kipindi kifupi
mwaka 2011. Lakini hakuendelea kubaki Santiago Bernabeu, pamoja na
kumvutia kocha Jose Mourinho, japokuwa mchezaji mwenyewe alikuwa anataka
kubaki na Los Blancos.
Akiongea katika mazungumzo na kituo cha BBC cha Uingereza, Adebayor
amefunguka kwamba moja ya sababu zilizopelekea Real Madrid kutoendelea
nae ilikuwa ni barua iliyotumwa na ndugu yake wa kiume kwenda kwa maboss
wa Bernabeu, ikiwashauri viongozi wa Real kutomsajili nahodha huyo wa
Togo.
Adebayor anasema alifanya kila kitu ili aweze kuendelea kubaki Madrid. “Nilifanya
kila kitu ili niweze kubaki jijini Madrid, lakini kwasababu ya kaka
yangu sikuweza kubaki pale kwasababu alituma barua ….. barua rasmi
kutoka kwa familia ya Adebayor ikiwaeleza Madrid kwanini hawatakiwi
kunisajili. Hii ilichangia sana kuniharibia mipango yangu Santiago
Bernabeu,” alieleza Adebayor, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Basakhesir.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na Tottenham ana uhusiano mbaya
sana na familia yake, familia ambayo anasema hata kuzungumza nao ni mara
chache sana.
Anasema familia yake huwa haimtafuti hata kumsalimu pale anapopata
majeruhi au matatizo mengine, kipindi pekee wanachowasiliana nae ni
wakati wanahitaji msaada wa kifedha tu.
Katika kuonesha jeuri ya pesa matajiri wa kiarabu
wanaoimiliki klabu ya PSG wamepiga hodi katika klabu ya Barcelona tayari
kwa ajili ya kuvunja rekodi ya dunia kumtwaa mshambuliaji wa klabu hiyo
Neymar.
Taarifa zinasema kiasi cha zaidi ya £200m ambayo ni mara mbili na
zaidi ya pesa zilizotumika kumnunua Paul Pogba ambaye kwa sasa ndio
anashikilia rekodi ya usajili ya dunia kwa sasa.
Ripoti zinasema klabu ya PSG inataka kutumia mwanya wa Neymar kukosa
uhuru wa kucheza free mbele ya Messi hivyo wanataka kutuma ofa ya
karibia £222m ambayo ni wazi itawashawishi Barcelona kumuuza.
Katika dili hiyo Neymar atakula £30m kila mwaka na uwepo wa Dani
Alves katika kikosi cha PSG unaweza kuwa ushawishi mkubwa kwa Neymar na
PSG wanaweza kumtumia mlinzi huyo kumshawishi Neymar.
Habari zinasema Neymar hana furaha na Barcelona kwani ni ngumu
kuchukua tuzo ya Ballon D’Or ukicheza mbele ya Suarez na Messi ambapo
washambuliaji hao wanaminya uhuru wa Neymar akiwa uwanjani.
Lakini klabu ya Barcelona yenyewe wamesema hawana mashaka hata kidogo
kuhusu kuondoka kwa Neymar kwani suala hilo katika soko la usajili ni
gumu kutokea na wao wanapuuza uvumi wote kuhusu Neymar.
Josep Vives msemaji wa klabu ya Barcelona amesema “hata hatuwazi
kuhusu hilo kwani ni ngumu kutokea, ni mchezaji wetu muhimu sana na
sidhani kama tunaweza kupokea ofa yoyote juu yake.”
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesisitiza kikosi chake kitafanya
vizuri msimu ujao licha ya kutokuwa na usajili wa mbwembwe.
Bwire amesema Shooting hawafanyi mambo kutaka kujionyesha badala yake ni mipango sahihi.
Tuesday, July 4, 2017
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 04.07.2017 na RAM MBEGEZE
TADHALI SUBSCRIBE MBEGEZE TV YOUTUBE KWA HABARI MBALIMBALI ZA KIMICHEZO
Mshambuliaji wa
Uhispania na Chelsea Diego Costa, 28, anataka kuondoka Stamford Bridge
kwa wakati anaotaka yeye, na jambo hilo linachelewesha hatua ya Chelsea
kumsajili Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton (Daily Mirror).
Antonio
Conte anataka Chelsea watoe hata pauni milioni 100 kumsajili Romelu
Lukaku, kama Everton wanataka kiasi hicho ili kumuuza (The Telegraph).
Mshambuliaji
kutoka Argentina Lionel Messi, 30, atasaini mkataba mpya Barcelona mara
tu atakaporejea kutoka kwenye fungate yake baadaye mwezi huu (Goal).
Paris
Saint-Germain wanajiandaa kupanda dau jipya la kumtaka mshambuliaji wa
Monaco Kylian Mbappe, 18, na wamewasiliana na wawakilishi wa mchezaji
huyo (L'Equipe).
Arsenal wanapanga kutoa pauni milioni 70
kuwasajili viungo wawili kutoka Sporting Lisbon ya Ureno, William
Carvahlo, 25, na Gelson Martins, 22 (A Bola).
Arsene Wenger atakutana na Alexis Sanchez, 28, na
Hector Bellerin, 22, wiki hii kujaribu kuwashawishi wasiondoke Emirates
(The Sun).
Everton wana uhakika wa kumrejesha Goodison Park Wayne Rooney, 31, kutoka Manchester United msimu huu (TalkSport).
West
Ham United wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester
United Javier Hernandez "Chicharito" , 29, kutoka Bayer Leverkusen
(Telegraph).
Liverpool wanapanga kutoa euro milioni 12 kumsajili kipa wa Sevilla Sergio Rico (ABC Sevilla).
Chelsea
wameonesha dalili kuwa wapo tayari kutoa pauni milioni 60 kumsajili
beki wa kushoto Alex Sandro kutoka Juventus (Telegraph).
Barcelona
wanaongoza katika mbio za kumsajili beki wa Juventus Leonardo Bonucci.
Chelsea wanataka kumsajili beki huyo, lakini yeye angependa kwenda
Barcelona (Daily Mirror).
Inter Milan wanataka kupanda dau la kumtaka mshambuliaji wa PSG Angel di Maria (Tuttosport).
Kipa wa zamani wa Arsenal Jens Lehmann anatarajia kurejea Emirates kama mmoja wa makocha wa kikosi cha kwanza (Guardian).
Gianluigi Donnarumma amekataa kuhamia Paris-Saint-Germain na amekubali kusaini mkataba mpya kusalia AC Milan (Sky Sport Italia).
Kiungo
wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, 24, amefanya mazoezi na
Birmingham City, akitaka kuhamia klabu hiyo kutoka Lazio (Daily Mirror).
Southampton
wanataka kukamilisha usajili wa pauni milioni 8.75 wa mshambuliaji Yann
Karamoh, 18, ambaye ana mzozo na klabu yake ya Caen ya Ufaransa (Sun).
Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya utakaompeleka hadi mwaka 2020 (AS).
Meneja
wa Manchester United Jose Mpurinho anakasirishwa na hatua ya klabu hiyo
kutosajili wachezaji zaidi ya Victor Lindelof, 22, peke yake mpaka sasa
(Daily Mirror).
Jose Mourinho anataka mshambuliaji Alvaro Morata,
24, kutoka Real Madrid na kiungo Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea
wajiunge na kikosi chake kabla ya Jumapili watakapoanza safari ya
Marekani ya mechi za maandalizi (Daily Star).
Real Madrid 'wamekomaa' na Alvaro Morata hadi Manchester United watakapotoa pauni milioni 79 (Marca).
Kiungo
kutoka Guinea Naby Keita, 22, anataka kuhamia Liverpool, lakini klabu
yake RB Leipzig inataka pauni milioni 70 (Daily Mirror).
Crystal Palace wameshindwa kulipa pauni milioni 30 wanazotaka Liverpool kwa ajili ya beki wa kati Mamadou Sakho, 27 (Guardian).
Manchester United wanajiandaa kupanda dau kumsajili beki Marc Bartra, 26, kutoka Borussia Dortmund (Manchester Evening News).
Newcastle bado hawajafanikiwa kumsajili kipa Pepe
Reina, 34, kwa kuwa Napoli hawajapata mtu wa kuziba nafasi yake
(Newcastle Chronicle).
Leicester City wamefanya mazungumzo ya awali na Sevilla kuhusu usajili wa kiungo Vicente Iborra (Sky Sports).
Kipa Wojciech Szczesny amerejea Arsenal kutoka Roma alipokuwa kwa mkopo kwa miaka mwili (Instagram).
Habari
zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha
kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii
(Kiingereza): Tetesi kuhusu uhamisho Ulaya
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.
WINGA Jamal Mnyate aliyekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha
Simba amefunguka na kusema kuwa bado ataendelea kuwemo katika klabu hiyo
kutokana na kuwa na mkataba na timu hiyo.
Mnyate alisajiliwa na Simba akitokea katika klabu ya Mwadui kwa
mkataba wa miaka miwili lakini tangu alivyosajiliwa alifanikiwa kucheza
mechi kadhaa kutokana na mara nyingi akiwa anasumbuliwa na majeruhi.
“Kwa hivi sasa ni ngumu kusema msimu ujao nitakuwa wapi, kwasababu
bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Simba kikubwa mimi na wasikiliza wao
waajiri wangu watakavyonambia kuhusu hatima yangu,”alisema.
Mnyate alisema hawezi kuzungumza chochote kwa sasa kutokana na kuwa
bado yupo chini ya mkataba na timu hiyo, lakini angekuwa ameshamaliza
nao mkataba angekuwa huru kusema msimu ujao angeenda timu gani.
Aidha,Mnyate amewapongeza Viongozi wake kwa usajili walioufanya kwa
kuwarudisha wachezaji wao wa Zamani kama Emmanuel Okwi,Shomary Kapombe
ambao walikuwa tishio ligi kuu.
Kiungo nyota wa Simba, Muzamiru Yasin amegeuka lulu kwa baadhi ya timu za Afrika Kusini.
Muzamiru
yuko Afrika Kusini akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
katika michuano ya Cosafa ambayo imetinga nusu fainali kwa kuwatwanga
wenyeji Afrika Kusini.
Taarifa zinaeleza, mawakala kadhaa wameanza kumfuatilia kwa karibu baada ya kuwa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri zaidi.
Moja
ya magazeti ya Afrika Kusini yameeleza kuwa Muzamiru ni lulu kutokana
na uwezo aliouinyesha katika mechi zote hadi taifa Stars inafikia nusu
fainali ya michuano ya Cosafa.
Imeelezwa
moja ya timu zilizovutiwa ni Bidvest na Mpumalanga Black Ace lakini
wataalamu wanaofuatilia wachezaji au mawakala wanaweza kuwapeleka
wachezaji katika timu hata za nje ya Afrika Kusini.
Katika michuano hiyo Muzamiru amekuwa injini kuu ya kuendesha kiungo cha Stars na kusababisha mvuto huo.
Kauli
iliyotolewa na Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali kuwa wameachana
na kipa wao Deogratius Munish ‘Dida’ imeonyesha kuwashitua mashabiki
wengi wa klabu hiyo.
Wengi wamekuwa wakihoji sababu ya Dida kuondoka na wengine wakimtaka kuvuta subira.
Lakini wako mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiutaka uongozi wa Yanga kukaa na kumalizana naye vizuri.
Wengine wameshauri kama amepata timu nje aende lakini si hapa Tanzania.
Pondamali alisema Dida aliwaambia hatasaini mkataba na juhudi za kumbembeleza zimekwama.
Hivyo kips African Lyon waliyemsajili, Beno Kakolanya waliyenaye na watasajili kipa mwingine chipukizi.
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inakutana leo saa 7 mchana.
Inakutana kujadili suala la uchaguzi baada ya kamati ya uchaguzi kuahirisha mchakato wa uchaguzi.
Kamati hiyo iliahirisha mchakato wa
uchaguzi baada ya mwenyekiti wake kutofautiana na wajumbe waliokuwa
wakitaka Jamal Malinzi lazima afanyiwe usaili licha ya kuwa mahabusu.
Kama haitoshi, Mwenyekiti wake, Waikili
Revocatus Kuuli alisema wajumbe walitaka kuwakata baadhi ya wagombea
bila sababu za msingi.
Hivyo akaona hakukuwa na suala la weledi na kuamua kusimamisha mchakato wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.
Hivyo, kamati ya utendaji ya TFF italisikiliza hilo na kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kuamsha mchakato huo wa uchaguzi.
Everton
inayodhaminiwa na SportPesa imeonyesha imepania kujiimarisha msimu ujao
baada ya kumwaga pauni million 30 kumnasa beki kisiki Michael Keane kwa
mkataba wa miaka mitano.
Keane
alikuwa kisiki katika kikosi cha Burnley na klabu kadhaa kubwa
zilionekana kumtolea “mimacho” lakini Everton imefanya kweli mapemaa.
Maana
yake, Keane atakuwa kati ya wachezaji watakaotua nchini na kucheza
mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia Alhamisi ya Julai 13 kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.