USHINDI ni matokeo ya juhudi na kujituma kwa wachezaji ambao wamepewa jukumu la kupeperusha Bendera ya Taifa kimataifa.
Timu ya Taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ imefikia hatua yake ya kwanza kwenye michuano ya
Chan baada ya kupata ushindi mbele ya wapinzani wao wakubwa Kenya.
Haikuwa kazi
rahisi kupenya hatua hii kwani mwanzo kwenye mchezo wa nyumbani hakuna
ambaye alipata matokeo chanya hata mchezo wa marudio pia dakika tisini
zilikamilika kwa timu zote kumaliza bila kufungana.
Ni dua za
mashabiki na umakini wa wachezaji kutumia vema nafasi ya matuta kupata
ushindi hatimaye wamepenya hatua ya kwanza kwenye michuano hii mikubwa.
Shukrani kubwa
zinarudi kwa mashabiki ambao wapo bega kwa bega na timu licha ya kupitia
changamoto za kutopata matokeo mchezo wa kwanza.
Mashabiki wamekuwa na timu kwa kuipa sapoti jambo ambalo limeongeza nguvu za kutosha kwa wachezaji kutimiza wajibu wao uwanjani.
Kitu cha msingi
kwa wachezaji ilikuwa ni kutimiza majukumu yao uwanjani hicho ndicho
wamekifanya na mashabiki wamekuwa wakiwapa sapoti wachezaji jambo ambalo
limeongeza nguvu.
Ikumbukwe kuwa mashabiki wa timu ni muhimili kwa kupata matokeo kutokana na sapoti ambayo wanaitoa uwanjani.
Uwepo wao ni sawa
na mchezaji wa 12 jambo ambalo linaongeza nguvu kwa wachezaji kupambana
kwa ajili ya Taifa pia kuona ile shauku ya mashabiki inakatika.
Pongezi kubwa
kwao licha ya wengi kushindwa kujitokeza nchini Kenya ila bado walikuwa
wakiishi kwenye vichwa vya wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Kwenye mchezo wa
kwanza ambao ulichezwa uwanja wa Taifa mashabiki wengi kutoka pande
mbalimbali za Tanzania waliwasili uwanja wa Taifa kuipa sapoti timu ya
Taifa.
Licha ya
kushindwa kupata matokeo chanya bado mashabiki waliendelea kuungana na
timu hiyo mazoezini mpaka siku inaondoka kwenda Kenya ni moyo wa upendo.
Serikali pia
haijaiacha timu ya Taifa kwenye mazingira ya unyonge kwani wamekuwa nao
bega kwa bega kupitia viongozi ambao wametoa sapoti kubwa.
Hili ni jambo la
kujivunia kwa hapa ambapo tupo kwa sasa kuna kitu ambacho ,mashabiki
wanapaswa waongeze ni kushangilia hata pale timu inapokosa matokeo.
Kasumba hii
imekuwa ikiwasumbua mashabiki wengi kwani wamekuwa wakitazama ni muda
gani wa kushangilia mpaka mchezaji apige chenga ama awe na mpira hapo
watashangilia ila kama hakuna tukio basi kushangilia kunakoma.
Kuna umuhimu wa
kuwa na mabadiliko makubwa kwa upande wa ushangiliaji kwa mashabiki
wakati ujao ili kuendelea kupata matokeo hata wakati ule timu inapokuwa
nyuma kwa kufungwa.
Shabiki yeye ni
mchezaji wa 12 hivyo kama atakaa kimya anamaliza nguvu za mchezaji wa 11
ndio maana kuna timu ambazo zimekuwa zikipewa adhabu kwa kutoruhusu
mashabiki kuingia uwanjani zimekuwa zikishindwa kupata matokeo chanya.
Muda wetu sasa
kubadilika huku tuliko na kufanya mengine makubwa kwenye masuala ya
ushangiliaji pamoja na kutoa sapoti kwa timu zetu.
Stars bado kazi
inaendelea kwani mchezo unaofuata ni dhidi ya Sudan hapo ni lazima
kupambana kwa juhudi kabla ya kumenyana na Rwanda ndipo kuibukia kwenye
michuano ya Chan.
Kila kitu
kinawezekana kwa kujipanga na kujiamini wakati wa kufikia mafanikio
ambayo tumeyakosa kwa muda mrefu ni sasa mashabiki enedeleeni kutoa
sapoti bila kuchoka.
Kwa kufanya hivyo kutaongeza msukukumo kwa wachezaji kucheza kwa juhudi na kutimiza majukumu yao kwa wakati.