Sunday, August 11, 2019

KCM: AS KIGALI TUNAMALIZANA NAO BONGO JUMLAJUMLA



JACKSON  Mayanja Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa sare tasa waliyoipata mbele ya AS Kigali ya Rwanda itajibiwa kibabe Dar.

Jana KMC, ilitupa karata yake ya kwanza kwa kucheza na AS Kigali na ubao kusoma 0 kwa wenyeji AS Kigali pamoja na wageni KMC.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuwa kati ya Agosti 23-25 jiji Dar.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa wachezaji walijituma kutafuta matokeo wamekutana na ushindani mkubwa hivyo wanajipanga mchezo ujao.

“Mchezo ulikuwa mgumu na kila mchezaji amefanya kile ambacho nimemuelekeza licha ya kutopata matokeo jambo jema ni kwamba hatujafungwa.

"Kwenye marudio tutapambana kupata matokeo chanya kwani tutakuwa nyumbani na sapoti kubwa ya mashabiki," amesema.

BADO MASHABIKI KUNA KAZI YA KUFANYA KWA TIMU YA TAIFA, WACHEZAJI KAZI BADO IPO



USHINDI ni matokeo ya juhudi na kujituma kwa wachezaji ambao wamepewa jukumu la kupeperusha Bendera ya Taifa kimataifa.

Timu ya Taifa ya Tanzania  ‘Taifa Stars’ imefikia hatua yake ya kwanza kwenye michuano ya Chan baada ya kupata ushindi mbele ya wapinzani wao wakubwa Kenya.

Haikuwa kazi rahisi kupenya hatua hii kwani mwanzo kwenye mchezo wa nyumbani hakuna ambaye alipata matokeo chanya hata mchezo wa marudio pia dakika tisini zilikamilika kwa timu zote kumaliza bila kufungana.

Ni dua za mashabiki na umakini wa wachezaji kutumia vema nafasi ya matuta kupata ushindi hatimaye wamepenya hatua ya kwanza kwenye michuano hii mikubwa.

Shukrani kubwa zinarudi kwa mashabiki ambao wapo bega kwa bega na timu licha ya kupitia changamoto za kutopata matokeo mchezo wa kwanza.

Mashabiki wamekuwa na timu kwa kuipa sapoti jambo ambalo limeongeza nguvu za kutosha kwa wachezaji kutimiza wajibu wao uwanjani.

Kitu cha msingi kwa wachezaji ilikuwa ni kutimiza majukumu yao uwanjani hicho ndicho wamekifanya na mashabiki wamekuwa wakiwapa sapoti wachezaji jambo ambalo limeongeza nguvu.

Ikumbukwe kuwa mashabiki wa timu ni muhimili kwa kupata matokeo kutokana na sapoti ambayo wanaitoa uwanjani.

Uwepo wao ni sawa na mchezaji wa 12 jambo ambalo linaongeza nguvu kwa wachezaji kupambana kwa ajili ya Taifa pia kuona ile shauku ya mashabiki inakatika.

Pongezi kubwa kwao licha ya wengi kushindwa kujitokeza nchini Kenya ila bado walikuwa wakiishi kwenye vichwa vya wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

Kwenye mchezo wa kwanza ambao ulichezwa uwanja wa Taifa mashabiki wengi kutoka pande mbalimbali za Tanzania waliwasili uwanja wa Taifa kuipa sapoti timu ya Taifa.

Licha ya kushindwa kupata matokeo chanya bado mashabiki waliendelea kuungana na timu hiyo mazoezini mpaka siku inaondoka kwenda Kenya ni moyo wa upendo.

Serikali pia haijaiacha timu ya Taifa kwenye mazingira ya unyonge kwani wamekuwa nao bega kwa bega kupitia viongozi ambao wametoa sapoti kubwa.

Hili ni jambo la kujivunia kwa hapa ambapo tupo kwa sasa kuna kitu ambacho ,mashabiki wanapaswa waongeze ni kushangilia hata pale timu inapokosa matokeo.

Kasumba hii imekuwa ikiwasumbua mashabiki wengi kwani wamekuwa wakitazama ni muda gani wa kushangilia mpaka mchezaji apige chenga ama awe na mpira hapo watashangilia ila kama hakuna tukio basi kushangilia kunakoma.

Kuna umuhimu wa kuwa na mabadiliko makubwa kwa upande wa ushangiliaji kwa mashabiki wakati ujao ili kuendelea kupata matokeo hata wakati ule timu inapokuwa nyuma kwa kufungwa.

Shabiki yeye ni mchezaji wa 12 hivyo kama atakaa kimya anamaliza nguvu za mchezaji wa 11 ndio maana kuna timu ambazo zimekuwa zikipewa adhabu kwa kutoruhusu mashabiki kuingia uwanjani zimekuwa zikishindwa kupata matokeo chanya.

Muda wetu sasa kubadilika huku tuliko na kufanya mengine makubwa kwenye masuala ya ushangiliaji pamoja na kutoa sapoti kwa timu zetu.

Stars bado kazi inaendelea kwani mchezo unaofuata ni dhidi ya Sudan hapo ni lazima kupambana kwa juhudi kabla ya kumenyana na Rwanda ndipo kuibukia kwenye michuano ya Chan.

Kila kitu kinawezekana kwa kujipanga na kujiamini wakati wa kufikia mafanikio ambayo tumeyakosa kwa muda mrefu ni sasa mashabiki enedeleeni kutoa sapoti bila kuchoka.

Kwa kufanya hivyo kutaongeza msukukumo kwa wachezaji kucheza kwa juhudi na kutimiza majukumu yao kwa wakati.

ZAHERA AFICHUA KINACHOIMALIZA YANGA, APANIA KUPETA UGENINI



KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa bado kikosi chake hakijawa na maelewano mazuri jambo ambalo liliwapa taabu kupata matokeo kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Township Rollers.

Yanga jana imelazimisha sare dhidi ya Township Rollers, mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa kwa kufungana bao 1-1.

Mchezo wa marudiano wa kimataifa unatarajiwa kuchezwa  kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana.

"Wachezaji wangu bado wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kuelewana wakiwa ndani ya uwanja jambo ambalo linaleta ugumu kwenye kupata matokeo uwanjani.

"Kwa sasa hesabu ni kuona kwamba tunakuwa na kikosi imara ambacho kitapata matokeo kwenye mchezo wetu wa marudio, mashabiki waendelee kutupa sapoti katika hili, nami nitafanyia kazi makosa yote," amesema

SIMBA WAIKOMALIA YANGA, WAIPA TANO KISHA KUICHANA KIMTINDO



UONGOZI wa Simba umesema kuwa Yanga wanastaihili pongezi ila wamewaangusha wananchi kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Township Rollers jana uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa, kazi kubwa ambayo Yanga walipaswa waifanye ni kupata matokeo chanya kwa kuwa walikuwa nyumbani.

"Hongereni Yanga kwa kupata sare ya nyumbani ila haijawa sawa kwa Wananchi kwa kuwa mlikuwa na sapoti ya mashabiki na imekuwa ngumu kuitumia.

"Raha ya mchezo wa nyumbani ni kuwa na mashabiki, hivyo tutawaonyesha namna ya kufanya kwenye mchezo wetu wa marudio," amesema. 

Simba jana ililazimisha sare tasa dhidi ya UD Songo ya Msumbiji mchezo wao marudio unatarajiwa kuwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Taifa na Yanga nao watakuwa ugenini nchini Botswana.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif