Kocha
Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic alikuwa uwanjani wakati Coastal Union
ikiwakaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Katika
mechi hiyo ambayo Yanga ilishinda kwa bao 1-0, Kopunovic alikuwa
jukwaani akiwa ametulia na pembeni mdau Gazza ndiye aliyekuwa
akisaidiana naye kuchukua maelezo.
Simba itaivaa Coastal Union Jumamosi, wakati pia amefaidika kuuona Mkwakwani ulivyo mbovu katika sehemu ya kuchezea.
Pia amefaidika kuiona Yanga ikiwa inacheza mechi ya ugenini, kitu ambacho ni raha mustarehe na faida kwake.
No comments:
Post a Comment