Swansea City imemsajili
mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Andre Ayew aliyekuwa anakipiga
kunako klabu ya Marseille ya nchini Ufaransa.
Mchezaji huyo sasa anasubiri
kuidhinishwa kwa kibali cha Ligi Kuu ya England na cha kimataifa ili
aanze majukumu yake mara moja kwenye kikosi hicho cha Swansea.
Ayew mwenye umri wa miaka 25,
alikuwa akiwindwa na timu kadhaa za EPL na nyingine za ligi mbalimbali
za barani Ulaya, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya mkataba wake
na Marseille kumalizika.
Ayew atavaa jezi namba10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Wilfried Bony aliyejiunga na Manchester City mwezi Januari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment